NIWATAKIE HERI YA MWAKA MPYA 2017 WENYE BARAKA NA MAFANIKIO TELE- Peter Sarungi

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

Kwanza: kabisa, tumshukuru Mungu kwayote yaliyojiri mwaka 2016 yawe mabaya ama mazuri bado tuna wajibu wa kushukuru maana fikra na malengo yetu sio ya Muumba

Pili: Tumshukuru Muumba kwa kuendelea kutupa Uhai usiokuwa na upungufu hata kama upo kitandani ukiwa hoi kwa magonjwa na maumivu makali ama upo bar unakunywa pombe na kufanya starehe mbalimbali, wote yatupasa kumshukuru Muumba kwa huruma yake na upendeleo.

Tatu: Tupeane pole kwa wote tuliopatwa na kuguswa na misiba mbalimbali katika kipindi cha mwaka 2016, tuwaombe wapendwa wetu kwa mungu awarehemu na kuwahifadhi mahala pema mbinguni. Safari ni yetu sote, wao wametangulia tu.

Nne: Tusikate tamaa kwa matarajio tuliyoshindwa kufikia na wala tusibweteke kwa majarajio tuliyafikia katika kipindi cha mwaka 2016 maana Maisha ni mchakato. Ni harakati za kukusanya mambo manne (4) kwa pamoja ili kupata furaha (happy), mambo hayo ni pesa, heshima, afya na mapenzi. Hivyo jua kama wewe una afya njema jua kina mwenzako yuko maututi, kama wewe unapendwa kwa dhati jua kuna mwingine ana danganywa, kama wewe una pesa ya kukidhi mahitaji yako jua kuna mwingi ni fukara asiye na matumaini na kama wewe una heshimika basi jui kuna mwenzako amekuwa teja anayekosolewa mitandaoni. 

Tano na Mwisho, Niwatakie Mwanzo na mwendelezo mwema wa mwaka 2017 ukiwa na baraka, amani, furaha na mafanikio tele katika mipango yako ya mwaka mpya. Mungu akupe nguvu na ujasiri wa kutambua uwezo na karama yako ili uweze kufanya mambo makubwa na uyapendayo katika mwaka 2017. Mwaka 2017 uwe ni mwaka wa kujivunia tofauti na mwaka 2016 ingawa ni mwaka usio gawanyika kwa 2 kama tulivyo aminshwa na wakubwa zetu hapo zamani.

Mungu awa bariki sana na asanteni kwa kuwa mmoja kati ya marafiki wengi, ndugu wengi na jamaa wengi tulio shirikiana kipindi cha mwaka 2016.

Leave a Reply