Jamani-Jamani! Nyumbani kumenogaaa! Kama ilivyokua kawaida yao basi wametia timu tena!?? Mashangazi kwa wajomba, mama wadogo kwa wakubwa, baba wadogo kwa wakubwa, makaka kwa madada, bila kusahau mashemeji.
Si wengine bali ni familia ya marehemu Mzee William Olung’a Igogo wa Utegi, Rorya leo wamejumuika nyumbani kwa mzee O.O Igogo huko Segerea, Dar es salaam kwa maandalizi ya ndoa ya kijana wao ambaye ni mmoja wa wajukuu wa marehemu mzee William Olung’a Igogo ajulikanaye kama Isaka Alexander Igogo itakayo fanyika siku ya Jumosi tarehe 05 /08 / 2021, Dar es salaam, Tanzania.
Pichani juu ni maharusi watarajiwa bwana Isaka na Bi. Sarah katika pozi!
Basi, nami dada mtu napenda kuwatakia ndugu zangu kila la kheri katika hatua zilizo baki katika kutengeneza historia nyingine tena ya kuanzishwa kwa familia ya Bwana Isaka na Bi Sarah! Mungu awe azidi wabariki na atembee nanyi mpaka mwisho wa jukumu hili muhimu sana la kuunganisha koo mbili kua kitu kimoja! …. Nasikitika sijaweza kushiriki nanyi lakini nipo nanyi kiroho na kifikra! …. BTW, kwa msiofahamu udugu wangu na bwana harusi mtarajiwa ni hivi; Isaka ni mdogo wangu, yeye ni mtoto wa marehemu baba yangu mkubwa Alexander Olung’a Igogo. Baba yake ni mtoto wa pili kuzaliwa kwenye tumbo la bibi yangu akifuatiwa na baba yangu. Isaka alizaliwa na ulemavu wa kusikia na kuongea (kiziwi na pia ni bubu), hivyo kutoka na changamoto hizo baba yangu alimchukua na kumleta kuishi nasi Dar es salaam toka akiwa na miaka 5! Hiyo ilikuwa kwa madhumuni ya kumsaidia aweze kukaa karibu na wataalamu wenye ubobezi wa matatizo yake pia aweze kupata elimu stahiki!. Wengi wasiotufahamu vizuri huwa wanafikiria ni mtoto wa baba yangu kwasababu amekulia kwetu toka akiwa na umri huo. Ukweli ni mtoto wa kaka yake baba.
Mbarikiwe wote!