Happy 2nd birthday Georgina Faith

FB_IMG_1457923372146-2Wishing my cute girl, baby Georgina-Faith a very happy 2nd birthday. May Almighty God continue to protect you, bless you with long happy and healthy life………..imageMama Georgina-Faith looking great…….here’s her wishes to her beautiful daughter Screenshot_2016-03-13-23-18-45-1

FB_IMG_1457929351887-1
Screenshot_2016-03-13-23-22-01-1Happy birthday sweetie, we all love you ?❤❤❤

“Mashujaa hawa hatuwasikii kabisa”-Zitto Kabwe

Mwanamke Shujaa wangu siku ya Wanawake Duniani nimemkuta Zahanati ya Dutwa Halmashauri ya Wilaya Bariadi nikiwa kwenye ziara ya Taasisi ya Benjamin Mkapa. Mama huyu ni Mhudumu wa Afya Mkuu (Medical Attendant). Anaitwa Amina Makaja. Ameajiriwa kama mhudumu wa Afya toka mwaka 1977. Katika utumishi wake amewahi kujikuta peke yake kwenye zahanati na kufanya kazi za Mganga, Nesi na Mhudumu. Ameokoa maisha kwa kutibu watu na kuzalisha kina mama wenzake. Hii ndio hali Halisi ya Sekta ya Afya Nchini. Ukosefu wa watumishi sekta ya Afya maeneo mengi vijijini husababisha kuwa mama wa aina hii wengi sana. Mashujaa hawa hatuwasikii kabisa. Lakini tunasikia malalamiko tu dhidi ya Manesi na wahudumu bila kujali ugumu wa kazi zao. Siku ya Wanawake Duniani itazame wanawake katika nyeti kama hizi. Mwanamke wangu wa Siku kama ya leo mwaka huu ni Mama Amina Makaja wa Zahanati ya DutwaFB_IMG_1457914757649-1Asante sana Mh. Zitto Kabwe kwa kuliona hilo! Mimi naamini mashujaa wakweli ndani ya Tanzania wapo vijijini lakini hawapewi nafasi ya kusikika kwenye jamii!! Lakini muda umefika na mabadiliko ya kweli yanakuja. Nani alijua mtu kama Dr. John Pombe Joseph Magufuli angeweza kuwa Rais wa Tanzania bila yakuwa na “connection” za kimjini?! Pamoja tunaweza!!………ubarikiwe sana mama shujaa

Pumzika kwa amani ya Bwana!

2016-03-12 10.03.40Pumzika kwa amani ya Bwana kaka Jamoko. Sisi tulikupenda lakini Mungu amekupa zaidi. IMG-20160312-WA0000Wapendwa wasomaji wangu, sija blog toka Thursday na sita blog mpaka Juma Tatu ili kuonyesha heshima zangu za mwisho kwa my cousin-brother na Mwenyekiti wa ukoo wetu (Kama ulipitwa na tangazo soma Hapa). Leo hii ndio atazikwa. Hivyo sasa hivi yani mida hii ibada ya mazishi inaendelea huko kijijini Utegi, wilaya ya Rorya, mkowa wa Mara. Nami naungana nao katika maombolezo hayo kiroho……….Pia siku ya jana bibi yangu mzaa mama alitimiza miaka 2 tangu kufariki kwake. Naamini tutaonana tena katika inchi mpya. ?

https://youtu.be/iiGan-NRy3w

https://youtu.be/pyhQDV9S5sw

R.I. P brother!!

‘Mi mjaluo bwana, nasema Mi mjaluo’

Screenshot_2016-03-09-01-22-59-1‘Mi mjaluo bwana, nasema Mi mjaluo! Nikitu najivunia ujaluo ni fahari yangu’ ???……….. Akothee  unenifurahisha sana!! Ngoja ninikusindikize na wimbo huu kutoka kwa Owino Misiani. Kitu “authentic” Luo ???

https://youtu.be/Hr26mIFnWHE

NINAWATAKIA WANAWAKE WENZANGU‎ ULIMWENGUNI KOTE, HERI YA SIKU YA MWANAMKE-MJ

Monica Joseph  Mmiliki wa  Kampuni ya Monfinance Investment  Group na Muwakilishi  wa Philips Tanzania.
Monica Joseph Mmiliki wa  Kampuni ya Monfinance Investment Group na Muwakilishi  wa Philips Tanzania.

Tuesday, March 8, 2016

Ningependa kutumia fursa hii kama Dada, Mke, Mama, mfanyakazi, Mwanaharakati na mjasiliamali kuwapongeza wanawake wote kwa kuadhimisha siku hii muhimu ya kuwaenzi wanawake wote ulimwenguni. 

Historia ya Maisha yangu, ni kielelezo cha maisha ya wanawake wengi ulimwenguni wanaopitia changamoto mbalimbali.‎ Nililelewa katika mazingira kandamizi ya Jinsia ya kike-kwenye jamii ambayo mtoto wa kiume alipewa nafasi ya kipekee katika masuala mbalimbali dhidi ya mtoto wa kike…Kwa mfano kipaumbele cha kupata elimu walipewa watoto wa kiume wakati watoto wa kike wakitarajiwa kushughulika na kazi za nyumbani, kupika,kuchota maji na kusaidia shughuli za kilimo na hatimaye kuolewa. _MG_3500-1Bibi yangu (Apumzike kwa Amani) alikuwa mhanga wa mfumo huo kandamizi. Kwa taabu alizopita Bibi yangu alijiwekea nadhiri kwamba Mjuu wake, hatopitia shida alizopitia yeye…na hivyo siku zote alikuwa akiniasa kwamba “Niyu (jina langu la nyumbani),Unaweza kila kitu kinachofanywa na mtoto wa Kiume”. Aliniimarisha kifikra na kiakili. 

Na siku zote alikuwa na msemo wake “Niyu Kasome, Ukasome umshinde Babu yako, Usije kuwa unanyanyasika kama sisi”- ushauri wake ndio ulikuwa dira yangu ya maisha ambapo nilisoma kwa bidii na kufanikiwa kuhitimu shahada ya uzamili katika masuala ya fedha kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde cha Uingereza. 

Hadi hivi leo, sauti ya Bibi haijakoma masikioni mwangu, sijaacha kutafuta elimu na maarifa ya masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo katika jamii…ni kwa sababu hiyo nilipata mafunzo ya muda mfupi ya uongozi na majadiliano kutoka Chuo kikuu cha Harvard cha nchini Marekani. Nitaendelea kuitafuta Elimu na pia kusaidia wenzangu, sababu naamini moja ya njia ya Mwanamke kujikomboa katika ukandamizaji wa kijinsia ni kuongeza kiwango cha elimu kwake mwenyewe na kwa wanawake wenzake.

Waswahili wana msemo usemao maisha ni shule…..msemo huu nimeuishi katika maisha yangu ya baada ya masomo. Nimefanya kazi katika mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali na sekta binafsi. nimefanya kazi na taasisi ya ISHI iliyokuwa inashughulikia masuala ya Ukimwi, baada ya hapo nimefanya pia katika kampuni‎ ya Philips Medical Systems ya Uholanzi na baadaye nimefanya kazi kampuni ya mawasiliano ya Maktech. Kwote nilipopita nimekumbana na changamoto mbalimbali zilizohusiana na jinsia yangu.

Utekelezaji wa majukumu yangu ulinilazimu kuwa na mikutano na watu mbalimbali Serikalini na kwenye taasisi za fedha ambapo watu niliokuwa nakutana nao ni wanaume ambao baadhi yao wamekuwa na mawazo ya mfumo dume yaliyojaa dharau na manyanyaso. Wengine kwenye fikra zao wanadhani mwanamke yeyote mwenye mafanikio, iwe kwenye biashara, siasa, ajira, lazima anabebwa na wanaume.‎ Wakiona mwanamke amefanikiwa tu, utasikia..huyu ‘hawala wa fulani’. hii ni dhana potofu na inayolenga kumdhalilisha na kumnyanyasa mwanamke. Mimi binafsi sikukubali kuyumbishwa na watu wenye mawazo ya aina hiyo.

Kila nilipokumbana na changamoto za aina hiyo nilipata hamasa ya kufanya kazi kwa bidii zaidi na kuwadhihirishia kwamba NINAWEZA, ilee sauti ya bibi ndioa ilikuwa ikinitia hamasa zaidi na zaidi na hatimaye kuniwezesha kufanya vizuri hadi kufikia kuaminiwa kupewa majukumu makubwa zaidi kama vile Mkurugenzi Mkuu katika kampuni ya Mokasi Medical Systems ambayo ni wakala wa kampuni ya Philips ya Uholanzi. Hasama hiyo iliniwezesha pia kuanzisha kampuni yangu inayotoa Huduma za kifedha – Monfinance Investment Group Ltd.

Mbali na shughuli hizo nimeweza pia kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya FINCA Microfinance Tanzania. Kwa ujumla siku zote za maisha yangu nimejihusisha na harakati za kupigania haki za wenye shida na mahitaji katika jamii kutokana na msingi niliojengewa na bibi yangu wa kukataa unyonge na kusaidia wanyonge. Hurka hiyo ndio ilipelekea ajira yangu ya kwanza kuwa kwenye taasisi ya uhamasishaji wa masuala ya ukimwi ya ISHI. Niliguswa kujihusisha na kampeni hizo kwasababu binafsi nimepoteza ndugu, jamaa na marafiki kutokana na ugonjwa huo. Mbali na ISHI,nimekuwa nikijihusisha na kampeni ya kuzuia mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) iitwayo IMETOSHA.

Ni jambo la udhalilishaji uliopitiliza kuwakata binadamu wenzetu viongo vyao kwa imani za kishirikina. Pia nimeshiriki kwenye uhamasishaji wa magonjwa yasiyojulikana (Rare diseases).‎ Tunaposherehekea siku ya Mwanamke duniani rai yangu kwa wanawake wenzangu, tushirikiane, tusaidiane, tupeane moyo na tuwezeshana ili tufikie lengo letu la usawa 50/50 kufikia mwaka 2030. Kila mwanamke atimize wajibu wake kwa kujitambua na kuhakikisha haki yake hainyongwi.

Mimi nimejitambua, ninasimamia haki yangu, na wala siipiganii, ni yangu, Jinsia yangu hainitofautishi kiutendaji na jinsia ya kiume. Ninachoangalia ni Mchango wangu katika maendeleo ya Uchumi, jamii na familia na sio Jinsia yangu. Ninachotambua katika jinsia yangu ni kuwa mimi ni Dada, Mama, rafiki, na Mke. Mengine yote,nipo sawa na wote, wanaume na wanawake.‎ Happy Women’s Day 2016. a7caeb96fbdcd21385508290de4f359f“Wanawake Tunapashwa Kuona Jinsia yetu kama rasilimali na sio Dhima”.  Women should view their gender as a resource rather than a liability”.

Credit: Vijimambo blog 

 

Fahari ya Tanzania!

FB_IMG_1457274730551FB_IMG_1457503631025FB_IMG_1457503927572Welcome to Tanzania the land of Zanzibar, Serengeti, and Kilimanjaro…..!!

Womens Day messages

Screenshot_2016-03-08-21-29-51-1

Womens Day messages

Screenshot_2016-03-08-21-22-15-1

Womens Day messages

Screenshot_2016-03-08-23-46-40-1

Womens Day messages

Screenshot_2016-03-08-21-22-39-1

Womens Day messages

Screenshot_2016-03-08-23-43-51-1

Womens Day messages

Screenshot_2016-03-08-21-20-23-1

Womens Day messages

Screenshot_2016-03-08-21-18-40-1Screenshot_2016-03-08-21-18-40-1-1-1Screenshot_2016-03-08-21-24-26-1

Womens Day messages

Screenshot_2016-03-08-21-23-51-1

Womens Day messages

Screenshot_2016-03-08-21-28-34-1Screenshot_2016-03-08-21-21-13-1

Womens Day messages

Screenshot_2016-03-08-21-21-53-1Screenshot_2016-03-08-21-19-59-1

Womens Day messages

Screenshot_2016-03-08-21-27-44-1

Happy International Womens Day

international-womens-day-2015-serenata-flowers

114IMG-20160308-WA0001Screenshot_2016-03-04-10-12-25-1https_proxyFB_IMG_143800237812212855402International-womens-day-images-2016

Happy birthday Sir. O.O Igogo

IMG_20160306_142940Before the sun goes down  (In Tanzania) let me take this time to wish this wonderful, amazing human being I call him father a very happy birthday! May Almighty God continue to protect you, bless you with countless blessings, grant you long happy-healthy life full of joy …IMG_20160306_144714it’s nice to see the “evolution” of human being through my very own father ?? Happy birthday Jategi, uwod Olung’a Ja’Kodol, owadi Gi Suzana Mauwa …..love you mingi mingi! ❤❤❤ IMG-20160307-WA0000This evening, family having dinner together in Dar es salaam, Tanzania enjoying  dad’s birthday.2016-03-07 14.14.46I am always happy to see my mama’s face ❤❤❤

Pumzika kwa amani kaka Jamoko!

FB_IMG_1457324639104-1Pumnzika kwa amani ya Bwana kaka yangu Mwl. Jamoko Laurent  Kateti Sarungi. Najua nipigo kubwa sana kwa familia yako na uchungu mwingi kwa ukoo wote wa Sarungi / Igogo; sisi tutalia na kuhuzunika kama wanadamu kwani myoyo yetu hii dhaifu lakini Mungu yeye ametenda kama Mungu hivyo jina lake lihimidiwe milele zote! FB_IMG_1457324626704Poleni sana watoto wa kaka yangu pamoja na wifi yangu. Mungu awe nanyi katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. FB_IMG_1457324610420Felista naweza hisia tuu machungu uliyo nayo sasa kwani baba yako alikuwa ndio rafiki yako mkuu! Mungu akupe moyo wa uvumilivu, akufariji kwa njia ya pekee ukamtegemee yeye siku zote. Akupe uwezo wa kufurahiya maisha tena bila uwepo wa baba. Pole sana mtoto wa kaka. FB_IMG_14573245657472 Timoth 4:3-7………… 3. nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. 4. Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako. 5.   Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. 6. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; 7. Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.

 

Until the morning glory comes R.I.P kaka yetu na Mwenyekiti wa  ukoo wetu! ?

Blog