? *KESHA LA ASUBUHI*? Alhamisi Mei 17, 2018 *ANA SHAUKU YA KUWASAIDIA WALIMU* *_______________________________* ? Fungu kiongozi ?? ?2 Wafalme 2:15. _*"Na hao wana wa manabii, waliokuwako Yeriko wakimkabili, walipomwona, walisema, Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha. Wakaja kuonana naye, wakainama kifudifudi mbele yake".*_ ?➖➖➖??➖➖➖? ✅ Roho Mtakatifu alikuja katika shule ya manabii, akileta hata mawazo ya wanafunzi katika upatanifu na mapenzi ya Mungu. Kulikuwapo na muunganiko hai kati ya mbingu na shule hizi, na furaha na shukurani za mioyo yenye kupenda ilidhihirika katika nyimbo za sifa ambazo malaika walijiunga kuimba. ✅ Iwapo walimu wangelifungua mioyo yao kumpokea Roho huyu, wangelikuwa tayari kushirikiana naye katika kutenda kwa ajili ya wanafunzi wao; na pale anapopewa njia huru, atasababisha mabadiliko ya ajabu. Atafanya kazi katika kila moyo, akirekebisha ubinafsi, kuumba na kusafisha tabia, na kuleta hata mawazo kuwa mateka kwa Kristo. … ✅ Badala ya kunyamazishwa na kurudishwa nyuma, Roho Mtakatifu ingelifaa akaribishwe, na uwapo wake kuhimizwa. Wakati walimu wanapojitakasa wenyewe kupitia katika utii wa Neno, Roho Mtakatifu atawafanya kuona kidogo mambo ya mbinguni. Watakapomtafuta Mungu kwa unyenyekevu na bidii, maneno ambayo wameyazungumza kwa msisitizo thabiti yatachoma mioyoni mwao; ndipo ukweli hautafifia katika ndimi zao. ? ```Uwakala wa Roho wa Mungu hauondoi kutoka kwetu umuhimu wa kutumia akili na vipawa vyetu, bali hutufundisha jinsi ya kutumia kila uwezo kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Akili za mwanadamu zikiwa chini ya uongozi maalum wa neema ya Mungu zinakuwa na uwezo wa kutumiwa kwa ajili ya kusudi lililo bora duniani. Kutokujua hakuongezi unyenyekevu au kumfanya mtu ye yote anayekiri kuwa mfuasi wa Kristo kuthamini zaidi mambo ya kiroho. Kweli za Neno takatifu zinaweza kufurahiwa vyema zaidi na Mkristo mwenye akili. Kristo anaweza kutukuzwa vyema zaidi na wale wanaomtumikia kwa akili. Kusudi kuu la elimu ni kutuwezesha kutumia uwezo ambao Mungu ametupatia kwa namna ile itakayowasilisha dini ya Biblia na kukuza utukufu wa Mungu.``` ?? - North Pacific Union Gleaner, May 26, 1909. *UWE NA TAFAKARI NJEMA MTOTO WA MUNGU* _______________________________
Pastor Caleb Migombo: PUMZIKA KIDOGO / GET SOME REST
PUMZIKA KIDOGO Kwanini Yesu, katikati ya siku yenye shughuli nyingi, aliwataka wanafunzi wake kuuacha umati wa watu na kwenda naye mahali pa faraga kupumzika? Alifahamu kuwa kadri walivyokuwa na kazi nyingi za kufanya ndiyo walivyohitaji kuweka muda wa kupumzika na kuwa pamoja na mwokozi wao. Kutofanya hivyo mwisho wake kungewaumizi wao wenyewe na wale wote waliokusudia kuwahudumia. Sisi nasi leo, ni muhimu kuzingatia ukweli huu. Mungu anajua shughuli zako na changamoto za Maisha yako ya kila siku – Iwe ni nyumbani, kazini, au Kanisani. Mungu anajua pia kuwa unahitaji hekima yake ili uweze kuwa na mtizamo sahihi wa kila shughuli na namna inavyopaswa kufanywa- na unahitaji pia nguvu kutoka kwake ili uweze kufanya kila jambo kwa usahihi. Kama hutapanga kuwa na muda wako wa kupumzika na kupata nguvu mpya (kimwili na kiroho)- upo uwezekano mbeleni wa wewe na wote uwapendao kuumia. Uchovu unaathiri kufikiri kwetu, namna tunavyowasiliana, na uwezo wetu wa kupenda wanaotunzunguka. Yesu akawaambia, “Twendeni peke yetu mpaka mahali pa faragha mkapumzike kidogo.” Alisema hivyo kwa kuwa kulikuwa na watu wengi mno waliokuwa wanafika hapo na kuondoka hata Yesu na wanafunzi wake hawakuweza kupata nafasi ya kula chakula" Marko 6:31 GET SOME REST Why, in the midst of such a busy day, did Jesus insist His disciples leave the crowds to rest and be alone with Him? He knew that the busier they were, the more they need to make time to rest and be alone with Him. If they didn’t, eventually they would hurt both themselves and those who they were seeking to help. The same is true for us God knows the demands and responsibilities you face-at home, on the job, even in your church. But God also knows you need His wisdom to keep those things in perspective, and you need His strength to get them done rightly. Then, because so many people were coming and going that they did not even have a chance to eat, he said to them, “Come with me by yourselves to a quiet place and get some rest.” Mark 6:31
Zari Hassan: Success is not sexually transmitted
Wow! Word of centuries!! "Success is not sexually transmitted" kila mtu apambane na hali yake!! Hata ukiwa na mwanaume au mwanamke mwenye akili ya maendelo kama kichwa chako hakipo sawa yani hata ulale naye huyo mtu miaka na miaka hauta kuwa yeye!! Kama uwamini kamulize Gardner Habbash ??? (just kidding)...... Jamani ukimpata mtu mwenye akili ya maendelo basi nawe unaongezea na zako!! Chuki wala roho mbaya haisaidii!! #SucessIsNotSexuallyTransmitted ? ? ? ? Regrann from @zarithebosslady - I repeat, success is not sexually transmitted!!! - #regrann
NITABAKI NA MAMA YANGU
NITABAKI NA MAMA YANGUKijana mmoja daktari alikwenda kuposa kwa familia moja yenye uwezo wa kifedha na Mali zao . Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Baada ya kujua kwamba daktari alimchukua mama yake aishi naye kwake baada ya kuona mama yake amekuwa ni mzee Sana. Yule Binti Akamwambia chagua mawili kunioa mimi au kukaa na mama yako pale kwako ?? , kwa sababu ukinioa mimi sitokubali kukaa na mama yako pale kwako maana itakuwa ni kwangu sasa mama yako akae pale ili iweje?? ! Yule kijana daktari alimuelemewa. Hakujua la kufanya Kuhusu maisha yake na yeye yule Binti , Mke mtalajiwa , Uku akitafakari Binti anampenda Sana lakini mama yake pia anampenda. Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu kwakuwa alikuwa wanatoka wote kijiji kimoja pia Ndio kiongozi wake wa maisha yake. Daktari alimwambia mwalimu :- Mwalimu kama nilivyokueleza awali kwamba nitaenda kuposa kwa yule kwa wazazi wa yule binti niliyekuambia yaani kwa Kweli moyo wangu unampenda mno yule binti siwezi Fikiria Mwanamke mwingine zaidi yake , lakini masharti aliyonipa ya yule Binti mke mtalajiwa ni kwamba nimfukuze mama yangu pale nyumbani kwangu ,, kitendo ambacho kinaniumiza Sana Kichwa, mimi siwezi kuishi mbali na mama yangu maana amekuwa mzee. Mwalimu sasa Nifanye nini na yule Binti nampenda vibaya mno ? Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa yule kijana daktari , alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao wa kukaa naye nyumbani kwako fanya mambo yafuatayo , Kwanza kabisa rudi nyumbani kwako , na leo usifanye chochote, ila Ukifika tu kosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya wasiwasi wowote. Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa, mikono kama mgongo wa kenge sasa ya kufanya kazi za sulubu wakati wa ujana wake.. , mama yake akamwambia mwanangu mikono yangu imegutaa kwasababu ya kufanya vibarua Ya kulima viazi na kupalilia mipunga ktk Mashamba Ya watu , Kwaajili Ya kutafuta Ada yako ya shule na uniform , Baba yako alifariki ukiwa mdogo Sana... Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kufanya kazi ngumu kwa ajili ya mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, mashambani, kulima viazi, kukosha nguo, kufyeka barabarani na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea fedha ya halali bila ya kujali ugumu hiyo Kwaajili Ya kumtunza Mwanae . Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana maendeleo mzuri. Yule kijana Daktari alilia sana akamwangalia viganja vya mama yake, akasema nakupenda mama yangu, nitakutunza kwa hali yoyote. . Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, Mwalimu siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya huyo Binti msomi asiyejua thamani ya mama yangu. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi Mwalimu ! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya Mwanamke msomi ambaye hajali thamani Ya mama yangu .. wakati mama yangu ameteseka maisha yake yote kwa ajili ya yangu. Mwacheni aende tu akaolewe na mwanaume yeyote ampendaye mimi nitabaki na mama yangu **Hadithi hii nimesoma kwa Ayo TV Facebook page**
Photo of the day: Emelda Mwamanga
Kesha la asubuhi: Anaongoza Utakaso wa Familia
*KESHA LA ASUBUHI* _ALHAMISI MEI 10, 2018_ *Anaongoza Utakaso wa Familia* _Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. Mithali 22:6._ ? Ninawasihi wazazi kujiweka tayari wao wenyewe na watoto wao kujiunga na familia ya juu. Kaa tayari, kwa ajili ya Kristo, kaa tayari kukutana na Bwana wako kwa amani. Anza kufanya kazi katika familia yako kwa namna itakayoleta matokeo mema. Anza katika mzizi wa jambo lenyewe. Leteni ukweli katika nyumba zenu, ili kuwafanya kuwa watakatifu na kuwatakasa. Usiuache katika ua wa nje. Ni vipofu kiasi gani wale wanaodai kuwa Wakristo kuhusu maslahi yao wenyewe! Ni kiasi gani wanashindwa kabisa kuona kile ambacho Kristo angeliwatendea iwapo angeliruhusiwa kuingia katika nyumba zao. ? Hebu Wakristo na watende kwa bidii ili kupata taji ya uzima kama vile walimwengu wanavyotenda ili kupata manufaa ya kidunia, na kanisa la Mungu kwa hakika litasonga mbele likiwa na nguvu. Roho Mtakatifu hutoa matendo ambayo yanapatana na sheria ya Mungu. Kazi ya kuhuisha ya Roho itaonekana katika familia zenye kujitahidi ili kuonesha wema, uvumilivu, na upendo. Uwezo wenye nguvu zote uko kazini, ukiandaa akili na mioyo ipate kujisalimisha kwa uwezo unaoumba wa Roho Mtakatifu, ukiwaongoza wazazi kujitakasa wao wenyewe, ili watoto wao pia wapate kutakaswa. ? Nyumba ambayo washiriki wake ni Wakristo wapole, waungwana huweka mvuto wenye ushawishi mwingi kwa ajili ya wema. Familia zingine watazingatia matokeo yaliyopatikana na nyumba kama hizo, na watafuata mfano uliowekwa, kwa upande wao wakilinda kaya zao dhidi ya mivuto ya kishetani. ? Malaika wa Mungu mara nyingi watatembelea makazi ambayo ndani yake mapenzi ya Mungu yanatawala. Chini ya nguvu ya neema ya Mungu kaya kama hiyo inakuwa ni mahali pa kuburudisha kwa wasafiri dhaifu na wachovu. Kwa kulinda kwa uangalifu, nafsi inazuiwa kujionesha kuwa na haki. Mazoea sahihi yanatengenezwa. Kuna utambuzi makini kuhusu haki za watu wengine. Imani itendayo kazi kwa upendo na kuitakasa roho inashikilia usukani, na kuitawala kaya yote. Chini ya mvuto mtakatifu wa kaya kama hiyo, kanuni za udugu zilizowekwa katika Neno la Mungu zinatambuliwa kwa upana zaidi na kutiiwa. - Southern Watchman, Jan. 19, 1904. *MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI*
The Lawyer herself in Songea!
Kesha la asubuhi: Anajibu maombi ya kutaka msaada wa Mungu
*KESHA LA ASUBUHI* JUMATANO 09/05/2018 *_ANAJIBU MAOMBI YA KUTAKA MSAADA WA MUNGU _* ? _Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. Kumbukumbu 6:6, 7_. ✍?Akina baba na akina mama, nitawezaje kupata maneno ya kuelezea jukumu lenu kubwa! Kwa tabia mnayoidhihirisha mbele ya watoto mnawafundisha kumtumikia Mungu au kuitumikia nafsi. Basi toa maombi yako ya dhati kwa mbingu kwa ajili ya msaada wa Roho Mtakatifu, ili mioyo yenu ipate kutakaswa, na kwamba njia mnayoifuata iweze kumheshimu Mungu na kuwavuta watoto wenu kwa Kristo. ✍? Inapasa kuwapa wazazi hisia ya umakini na utakatifu wa kazi yao, pale wanapotambua kuwa kwa mazungumzo au matendo ya kizembe wanaweza kuwapoteza watoto wao. ✍?Wazazi wanahitaji uongozi wa Mungu na Neno lake. Wasipoyasikiliza mashauri ya Neno la Mungu, wasipofanya Biblia kuwa mshauri wao, kanuni ya maisha, watoto wao watakua wakiwa wazembe na watatembea katika njia za kutokutii na kutokuamini. ✍? Kristo aliishi maisha ya kazi na kujikana nafsi, na alikufa kifo cha aibu, ili apate kutoa mfano wa roho ambayo itawachochea na kuwatawala wafuasi wake. Kadiri ambavyo wenzi wa maisha wanajitahidi nyumbani kwao kufanana na Kristo, mvuto wa mbinguni utaenezwa katika maisha ya familia yao. ??♂```Katika kila nyumba ya Kikristo Mungu anapaswa kuheshimiwa kwa dhabihu za asubuhi na jioni za sifa na maombi. Kila asubuhi na jioni maombi ya dhati inabidi yapande kwa Mungu kwa ajili ya baraka na uongozi wake. Je Bwana wa mbingu atapita katika nyumba kama hizo na asiache baraka hata moja pale? Hapana, kwa kweli. ??♂ Malaika wanasikia utoaji wa sifa na maombi ya imani, na wanabeba maombi kwenda kwake yeye anayehudumu katika patakatifu kwa ajili ya watu wake, na kukiri ustahili wake kwa niaba yao. Maombi ya kweli hushikilia nguvu za Mungu na kuwapa watu ushindi. Juu ya magoti yake Mkristo anapata nguvu ya kupinga jaribu. - Review and Herald, Feb. 1, 1912.``` *MUNGU TUWEZESHE KUTAMBUA KIMBILIO LETU NI WEWE TU*
Huwezi copy personality ya mtu!
Regrann from @mspaulsen – You can copy everything about a person but not her personality its a God given. Just be yourself ??utachekesha…….. – #regrann Mmesikia hayo maneno toka kwa Madam Rita? Personality ya mtu ni kama DNA huwezi iga wala huwezi kuwadanganya watu! Acha maisha ya kuiga iga kuwa wewe, acha watu wakujue, wakupende, na kukuheshimu kwa kuwa authentic best version of you na siyo kujifanya wewe fulani wakati watu wanakuona ni kitu kingine!
Kesha la asubuhi: Kando ya akina mama akiwaongoza watoto wao
*KESHA LA ASUBUHI* _JUMANNE MEI 08, 2018_ _Kando ya Akina Mama Akiwaongoza Watoto Wao_ _Naliomba nipewe mtoto huyu; Bwana akanipa dua yangu niliyomwomba; kwa sababu hiyo mimi nami nimempa Bwana mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa Bwana. Naye akamwabudu Bwana huko. 1 Sam 1:27, 28._ ? Akina mama Wakristo wanapaswa kutambua kuwa wao ni watendakazi pamoja na Mungu wakati wanapowafundisha na kuwaadabisha watoto wao katika namna ambayo itawawezesha kuakisi tabia ya Kristo. Katika kazi hii watakuwa na ushirikiano wa malaika wa mbinguni; lakini ni kazi ambayo kwa masikitiko imepuuzwa, na kwa sababu hii Kristo ananyang’anywa urithi wake-washiriki walio wadogo wa familia yake. Lakini kupitia kwa ukaaji ndani wa Roho Mtakatifu, ubinadamu unaweza kutenda kazi pamoja na uungu. ? Somo la Kristo wakati wa kuwapokea watoto, linapaswa kuacha alama yenye kina juu ya mioyo na akili zetu. Maneno ya Kristo yanawahimiza wazazi kuwaleta watoto wao kwa Yesu. Wanaweza kuwa wakaidi, na kuwa na hisia kali kama zile za kibinadamu, lakini hii haipasi kutukatisha tamaa ya kuwaleta kwa Kristo. Aliwabariki watoto waliopagawa na hisia kali kama yake mwenyewe. ? Mara nyingi tunakosea kuwafundisha watoto. Mara nyingi wazazi wanawaendekeza watoto katika kile kilicho cha kibinafsi na chenye kuharibu maadili, na, badala ya kuwa na uchungu wa roho kwa ajili ya wokovu wao, wanawaacha kuzurura bila malengo wala mwelekeo, na kukua wakiwa na tabia potovu na mienendo isiyopendeza. Hawakubali wajibu wao waliopewa na Mungu kuwaelimisha na kuwafundisha watoto wao kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Hawaridhishwi na tabia za watoto wao, na kuvunjwa moyo wanapotambua kuwa makosa yao ni matokeo ya uzembe wao wenyewe, na kisha wanakatishwa tamaa. ? Lakini ikiwa wazazi wangelihisi kwamba kamwe hawawekwi huru kutokana na mzigo wao wa kuwaelimisha na kuwafundisha watoto wao kwa ajili ya Mungu, iwapo wangelifanya kazi yao kwa imani, wakishirikiana na Mungu kwa maombi na kazi ya dhati wangelifanikiwa katika kuwaleta watoto wao kwa Mwokozi. Hebu akina baba na akina mama wajitoe wao wenyewe, roho, mwili, na nafsi kwa Mungu kabla ya kuzaliwa kwa watoto wao. - Signs of the Times, Apr. 9, *TAFAKARI NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI*
Mwanaume kuwa na nyumba peke yake si tija…..!
Nakubaliana na Lemutuz kwa maneno aliyo andika hapo chini lakini naomba niongezee kwa kusema kwamba; mwanaume kuwa na nyumba peke yake si tija bali kuwa na mji wako ndio mambo yote! Mwanaume sharti uwe na mji wako ndio utaheshimika! Hili hata kwenye Bible (kwa site tunao amini Bible) imesema. Siyo tu kufanya starehe halafu una lala na kuamka kwenye mji wa mwanaume mwenzio, kwani wewe unamatatizo gani?! Mwanaume kuuza sura hakukupi heshima au kukyongezea thamani yoyote bali kunaonyesha jinsi gani ulivyo na Itilafu kuchwani au mahala "fulanai" mwilini mwako!! Napia kuwa na nyumba nyingi kuna kufanya kuwa "baba mwenye nyumba" lakini hakukufanyi kuwa Baba Mwenye Mji (home)!! Kwa mwanaume kupata uwezo wa kusema nina kwangu au nina mji wangu lazima uwe na MKE!! Sijasema Kimada au Vimada hapana! MKE! Mwanamke uliyemuoa kihalali kwa kufata taratibu halali za kidini au lisheria! Nawala siyo mwanamke wa kufichia status kwa social media. Lasivyo hizo nyumba zako zinakuwa hazina uzito sana!! Nyumba hata Kunguni wanazo ?? Hivi bado kuna ndoa za kimila karne hii ??Just asking ??Regrann from @lemutuz_superbrand - FACT: Hapa mjini kuna Baba mwenye nyumba ...sio Baba mwenye wabebez au magari na nguo ...hahahahahahaha.....NI BABA MWENYE NYUMBA TU! .....tuleni Batazzz lakini TUJENGE...Case Closed ....U know! - @lemutuz_superbrand - #regrann
Kesha la asubuhi: Mwenye Wazazi Wanaojali
*KESHA LA ASUBUHI* _JUMATATU MEI 07, 2018_ *Mwenye Wazazi Wanaojali* _Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usini-ondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi. Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako. Zaburi 51:11-13._ ?Ni ombi la namna gani hili! Ni dhahiri kiasi gani kuwa wenye dhambi walioko nyumbani hawapaswi kutendewa kwa kutokujali, bali kwamba Bwana anawaangalia kama walionunuliwa kwa damu yake. Katika kila kaya ambamo ndani yake wamo ambao hawajaongoka, inapaswa kuwa kazi ya wale ambao wanamjua Bwana kutenda kwa hekima kwa ajili ya wongofu wao. Bwana kwa hakika atabariki juhudi za wazazi, wakati ambapo kwa kicho na upendo watajitahidi kuokoa roho za walio katika kaya zao. Bwana Yesu anasubiri kuonesha neema. ? Kwamba kazi ingelianza moyoni! “Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa, Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa. Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.” (Zaburi 51:16, 17). Basi hebu na ifahamike na wanakaya wote kwamba kazi hii lazima ianze moyoni. Moyo lazima utiishwe na kufanywa kuwa na toba kupitia katika uwezo wa Roho Mtakatifu unaoumba, na kufufua. Kwa kutambua msaada wa wakala huyu mwenye nguvu, je wazazi hawawezi kufanya kazi kwa ari na upendo zaidi kwa ajili ya wongofu wa watoto wao kuliko walivyowahi kufanya hapo nyuma? ?Ahadi ya Bwana ni kwamba “Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.” (Ezekieli 36:25-27). ? Roho wa Bwana anapofanya kazi katika mioyo ya wazazi, maombi na machozi yao yatakuja mbele za Mungu, watasihi kwa bidii, na watapokea neema na hekima kutoka mbinguni, na watakuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa ajili ya watoto wao ambao hawajaongoka. Kadiri Roho huyu anapodhihirishwa nyumbani, ataletwa kanisani, na wale ambao ni wamisionari wa nyumbani nao pia watakuwa mawakala wa Mungu kanisani na katika dunia. Taasisi ambazo Mungu amezipandikiza zitabeba tabia tofauti kabisa. - Review and Herald, March 14, 1893. *TAFAKARI NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI MTOTO WA MFALME*
Matukio katika picha
Hili nitukio la harusi limetokea jana huko Tabata, Dar, Tz . Nawafahamu vizuri sana wazazi wa bwana harusi lakini sina maelezo mazuri ya kuwapa kuhusu maharusi kwani siwafahamu na picha nimetumiwa tu! Hivyo naomba niwakilishe kwa kuwapongeza maharusi....... Nawapongeza maharusi kwa kufunga pingu za maisha na nawatakia maisha mema. Mrs Awiti L.C. and Ms Doreen L.C. Awiti dancing their heart off at the wedding ceremony of Wasongas son. This night of 6.5.018. Tabata Dar. Jamani hawa ni ndugu zangu kabisaaa sijikombi ?? Mrs Awiti L.C au mama Awiti ni shangazi yangu mke wa mjomba wangu Leo Awiti. Mzee Awiti ni kaka yake mama yangu mzazi tumbo moja! Hivyo Doreen Awiti ni cousin yangu kabisaaa! Bwana harusi ni mjukuu wa Mrs Awiti L.C na baba mzazi wa Bwana harusi ni former employee wa Utegi Tech...... si mshanipa mpaka hapo?! ?
International Day, 2018
International Day ni siku ambayo makanisa ya Wasabato hapa Marekani wanasherekea au unawezasema wana enzi uwepo wa "diversity" (uwepo wa mataifa mbali mbali na tamamaduni zao) ndani ya makanisa na haswa ndani ya nchi. International Day haifanyiki siku moja yani hakuna siku maalumu iliyotengwa kuwa leo ni International Day bali husherekewa kuanzia mwezi wa Nne mpaka mwishoni mwa mwezi wa Tano, anywhere kabla ya sherehe za makambi. International Day nikama siku ya wageni inavyofanyika Tanzania, wale Wasabato wenzangu waliopo Tanzania wananielewa. Tofauti huko Tanzania naona mnasahau kuwa siyo wageni wote ni Watanzania (hawaongei Kiswahili) hivyo kungekuwa na umuhimu wa kuwatambua kwa mataifa yao.Anyway, siku hii kwa hapa kwetu ilifanyika jana May 5th, 2018. Tulifurahi sana kwa kula vyakula vya mataifa tofauti tofauti. Haya nawe enjoy picha hizo na ubarikiwe sana. Pichani ni First Lady wa kanisa letu (Mke wachungaji wetu) pamoja na mama yangu mzazi. Mtanzania mwenzangu na mshiriki wa kanisa letu pamoja na mama yangu. A sister from Kenya and our church members Another sister from Kenya, I real do love Kenyans! Ni watu ambao wako straight to the point kama hataki kitu anasema wazi kuwa sikitaki kwasababu hii! Ule unafiki wa "Kibongo" kwakweli hawana au mimi sijakutana na Wakenya wenye unafiki wa level yetu sisi Wabongo! Napia wanaelewa kuwa to agree to disagree ni jambo lakawaida siyo chuki! Mimi ninaugonjwa wa kuchukia WANAFIKI NA WAONGO!! Jamani siwape watu wenye tabia hizo!! mniombee tu kwakweli maana only God knows how much I hate watu wa sampuli hiyo!! Anyway, tuendelee na story yetu ??? Wanawake wa Kitanzania wakiwakilisha ?
Mother’s Day 2018: Je, ungependa ku-share nasi hadithi / shukrani ya mama yako mpenzi?
Mother and daughter moment: Mother's Day inakuja ni jumapili ijayo, je umepanga kufanya nini au kumfanyia nini mama yako? Mimi binafsi nitakuwa Washington, DC niki enjoy kidogo na mama yangu! Kwani hii itakuwa Mother's Day ya kwanza kabisa kwa mama yangu kuwa hapa Marekani pamoja nami; hivyo nitaitumia nafasi hii vyema. Sasa basi tuambie kuhusu wewe. Je, ungependa kuShare nasi stori ya mama yako au kutoa shukrani zako kwa mama ukiambatanisha na picha ya mama yako? Basi wasiliana na alphaigogo.com kwa kutuma ujumbe kwa njia ya blog, Instagram DM, au Facebook nasi tutaweka ujumbe wako. **Zoezi hili linaanza rasmi leo hii mpaka JumaMosi.** Asanteni Pichani ni mdogo wangu Janeth na binti yake Essy. #TBS 2017
Kesha la asubuhi: Bado tunapendwa ijapokuwa tunakosea
*KESHA LA ASUBUHI* _JUMAMOSI MAY 5, 2018_ *Bado Tunapendwa Ijapokuwa Tunakosea* _Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki. 1 Yoh. 2:1._ ✍? Wale ambao wako katika muunganiko na Mungu ni mifereji kwa ajili ya nguvu ya Roho Mtakatifu. Iwapo mtu ambaye kila siku anawasiliana na Mungu atakosea njiani, iwapo atageuka hata kidogo na kuacha kumtazama Yesu kwa uaminifu, hiyo si kwa sababu anatenda dhambi kwa makusudi; kwa kuwa anapoona kosa lake, anarejea tena, na kukaza macho yake kwa Yesu, na ukweli kwamba amekosea haumfanyi kuwa na thamani pungufu moyoni mwa Mungu. ✍? Anafahamu kuwa ana mawasiliano na Mwokozi; na anapokemewa kwa ajili ya kosa lake katika jambo fulani la hukumu, hatembei kwa kinyongo, na kumlalamikia Mungu, bali huligeuza kosa lile kuwa ushindi. Anajifunza somo kutoka katika maneno ya Bwana, na kuchukua tahadhari asije akadanganyika tena. ✍? Wale ambao wanampenda Mungu kwa kweli wanao ushahidi wa ndani kuwa wao ni wapendwa wa Mungu, kwamba wana mawasiliano na Kristo, kwamba mioyo yao inachochewa kwa upendo motomoto kwake. Ukweli kwa ajili ya wakati huu unaaminiwa kwa imani hai. Wanaweza kusema kwa uhakika wote, “Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake. … ✍? Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.” (2 Petro 1:16-19). Maisha ya ndani ya roho yatajidhihirisha yenyewe katika mwenendo wa nje. Hebu acha Neno la Mungu libebe ushuhuda wake badala ya mjumbe ambaye kupitia kwake Mungu ametuma ujumbe katika siku hizi za mwisho ili kuwaandaa watu waweze kusimama katika siku ya Bwana. ✍? “Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!” (Isaya 52:7). Hekima ya wale wanaoitwa wasomi haiwezi kutegemewa, isipokuwa wamejifunza na kila siku wanajifunza masomo kutoka katika shule ya Kristo. Wanadamu, katika hekima yao ya kudhaniwa, wanaweza kupanga na kubuni nadharia na mifumo ya falsafa, lakini Bwana anawaita bure na wapumbavu. Bwana anasema, “Upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.”(1 Wakorintho 1:25). - Review and Herald, May 12, 1896. *MUNGU AKUBARIKI MTOTO WA MFALME*
Where is my babysister?
Yuko wapi Jokate wangu? Jojo, where are you at? Hope all is well with you, don't let those haters take you down baby gal! Just give me some days I will destroy them like tornado ? Seriously nawauliza waungwana where is my babysister at? Sipendi! Sipendi! @ brother Paul Makonda can you kindly check on my babysister please? Kamanda Sirro, where is Jokate Mwegelo?? Jamani this ain't funny! Jojo, just know I love and missing you. Come back please! ??
Kesha la asubuhi: Kuzungukwa na ngao ya Mungu
*KESHA LA ASUBUHI*
*Alhamisi 03/05/2018*
*Kuzungukwa na Ngao ya Mungu*
Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza. Zaburi 50:15.
?Majaribio yanapoinuka ambayo yanaoelekea kutoku-elezeka, hatupaswi kuruhusu amani yetu kuharibiwa. Hata tutendewe isivyo haki kiasi gani, hebu hasira kali isiinuke. Kwa kuendekeza roho ya kulipiza kisasi tunajidhuru sisi wenyewe. Tunaharibu imani yetu wenyewe kwa Mungu, na kumhuzunisha Roho Mtakatifu. Kando yetu yuko Shahidi, Mjumbe wa mbinguni, ambaye atainua kwa ajili yetu bendera dhidi ya adui. Atatufungia ndani kwa miale angavu ya Jua la Haki. Shetani hawezi kupenya ndani ya miale hii. Hawezi kuipita ngao hii ya nuru takatifu.
?Wakati dunia ikisonga mbele katika uovu, asiwepo hata mmoja kati yetu atakayejidanganya kwamba hatutakuwa na magumu. Bali ni magumu haya haya ndiyo yanayotufikisha katika chumba cha uwapo wa Mungu. Tunaweza kutafuta ushauri wa Yeye asiye na kikomo katika hekima.
?Bwana anasema, “Ukaniite siku ya mateso” (Zaburi 50:15). Anatualika kumpelekea matatizo yetu pamoja na mahitaji ya lazima, pamoja na hitaji letu la msaada wa Mungu. Anatuambia omba haraka. Mara tu tatizo linapoinuka, tunapaswa kumtolea maombi yetu ya uaminifu na ya dhati. Kwa kuombaomba sana kwetu tunatoa ushahidi wa imani yetu kubwa kwa Mungu. Hisi ya uhitaji wetu hutuongoza kuomba kwa bidii, na Baba yetu wa Mbinguni anaguswa na kusihi kwetu. Mara nyingi wale wanaoshutumiwa au kuteswa kwa ajili ya imani yao wanajaribiwa kufikiri kwamba wameachwa na Mungu. Katika macho ya wanadamu wako upande wa wachache. Katika mwonekano wote adui zao wanaonekana kushinda juu yao. Lakini hebu na wasikiuke dhamiri yao. Yeye aliyeteseka kwa niaba yao, na kubeba huzuni na mateso yao, hajawaacha.
?Watoto wa Mungu hawajaachwa peke yao na kuwa bila ulinzi. Maombi hugusa mkono wa Mwenyezi. Maombi “hushinda milki za wafalme, kufunga vinywa vya simba, kuzima nguvu ya moto” – Tutaelewa kinachomaanishwa pale tutakaposikia taarifa za wafia dini ambao walikufa kwa ajili ya imani yao- “walikimbiza majeshi ya wageni” (Waebrania 11:33, 34). – Christ’s Object Lessons, uk. 171, 172.
*MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI*
why so many people like to talk down on the teaching profession?
I don't get why so many people like to talk down on the teaching profession. It baffles me because teaching is no different than being a doctor, an engineer, a lawyer, all the other jobs that are deemed more important to society. These careers are seen as practices and people forget that Teaching is also a practice. It's a learning experience just like those other jobs. You see teachers literally everywhere. I always ask myself ...without teachers would we have doctors, lawyers, and engineers? People aren't born with all that knowledge they are TAUGHT it by TEACHERS. So, why the bad rep? Teachers are the backbone of all society and yet...never get that recognition. (Yes there are bad teachers, but there are far more good ones. But one should also research why there are bad teachers, what is so messed up about the education system that even ALLOWS bad teachers?) Of course many people who go into education don't do it to be noticed. But is it wrong to want to be respected? Is it wrong to want to know that your community understands your importance and impact on a student's life? Is it wrong to ask to be provided with resources needed to help reach student's success without having to constantly prove that they are essential? It seems like many people forget that it's not just the teachers but it's the students who also are affected. And how can a teacher do their job of educating these students when most of them don't even have the tools,support etc to achieve this goal? Everyone has a story about a teacher who has helped them, gone the extra mile, simply been there for them. Who would you be without them? - Rant ended***by Sarah, teacher to be***
Jukwaa langu: Mahojiano yangu na Mange Kimambi
Regrann from @mutwiba – Katika kipindi cha JUKWAA LANGU Jumatatu hii ndani ya Kilimanjaro Studio, utaanza kwa kusikiliza mahojiano yangu na Mange Kimambi.
Kisha tujadiliane kuhusu “Diaspora Connect” / ama Diaspora Disconnect”
* Kwanini wapo Diaspora wanaoamini kwamba Diaspora ndio suluhisho la matatizo Tanzania?
* Kwanini wapo Diaspora wanaoamini kwamba Diaspora ndio tatizo Tanzania?
* Ni kweli kwamba walio nyumbani hawatuelewi ama ni kwamba kuna Diaspora wasiojielewa wanapoamini kwamba walio nyumbani hawajielewi?
****Haya ni kati ya maswali mengi tutakayoulizana hapa**** Pia tutapata mrejesho kuhusu Tanzania Day 2018 iliyokamilika Dallas. Kisha mgeni wangu ni Boniface Makulilo.
*Navy Veteran
*Fulbright Alumni
*Mwalimu
*Mwandishi
*Mshauri mtandaoni.
*Mmoja wa wakurugenzi katika NGO moja inayohudumu mataifa 18.
Ana mengi ya kujadili nasi katika saa la pili.
Si ya kukosa
Ni kipindi cha JUKWAA LANGU, Jumatatu hii (Aprili 30, 2018) na kila Jumatatu kuanzia saa 12 kamili jioni mpaka 2 kamili usiku kwa saa za Marekani Mashariki (6:00 – 8:00pm ET). Ni kupitia Facebook live (Mubelwa Bandio na Kwanza Production) ama Kwanza Radio kwenye TuneIn
http://tun.in/sfwyf ama piga simu 202-683-4570 *******************************
PRODUCER: Mubelwa Bandio – #regrann