Hot shot of the day

FB_IMG_1447083368859-1Ma watatu katika ubora wake! Nimependa kila kitu. Really hot!! FB_IMG_1447083376718-1Be blessed!

Je wewe ni “Nyumbu?”

Hii nimeipata  mahala fulani nikaona ni share nanyi kwani kunaujumbe fulani kama ukiondoa mtazamo wa kisasa ukaangalia katika maisha yako ya kawaida utaelewa vizuri huu ujumbe. Soma mwenyewe….. FB_IMG_1447084101361“By kababu:

Mafuriko yameelekezwa baharini! Upinzani umefanya makosa mengi ya msingi na wengi wameshaandika haya – kuna kupokea makapi, kuna kuweka mayai yote kapu moja (kuachiana), kuna kushindwa kutangaza sera hata siku ya ufunguzi wa kampeni, kuna kudhulumiana ndani ya ushirika, kuna kutowafikia wananchi wengi vijijini kwa kupenda starehe na misifa ya helikopta, kuna kutokujibu tuhuma nzito dhidi ya afya ya mgombea wao, kuna kutojibu tuhuma kuhusu chama kikuu ndani ya Ukawa kununuliwa, kuna kudharau mpinzani wao mkuu kana kwamba kazeeka au kachoka sana, kuna kudharau umuhimu wa watumbuizaji katika jamii ya kiafrika na kuwaita fiesta, n.k. Makosa ni mengi mno. Ila hii ilitokana na nini? UNYUMBU!

Nyumbu inasadikika ndiye mnyama mwenye IQ (ufahamu) mdogo kuliko wanyama wengi mbugani. Ni mnyama ambaye mwindaji hasumbui akili yake sana japo nyumbu ana maguvu na mapembe makali! Kichwani hamna kitu! Nyumbu hujihami kwa kuotea! Huota kuwa simba au mwindaji mwingine yeyote akija atamla jirani yake na si yeye! Kwa hiyo aendapo nyumbu mwenzie na yeye huenda! Nyumbu mwenzie akipiga kona na yeye hupiga kona! Nyumbu mwenzie akisimama na yeye husimama! Nyumbu mwenzie akiruka na yeyehakawii!

Ndio maana katika lile ajabu mojawapo la dunia litokealo mtoMara kule Serengeti mamba hujilia nyumbu hadi wanakinai! Akitokea nyumbu mmoja akaruka mtoni au akamsukuma mwenzie basi nyumbu wote watarukia mtoni au watasukumana hadi wadumbukie mtoni.

Tabia hii ya nyumbu tumeiona katika kampeni za Ukawa! Wenyewe kwa vinywa vyao tumewasikia wakijinadi ALIPO NA SISI TUPO! Yaani hata akitumbukia mtoni na wao watajiloweka humo! Hata pale ilipokuwa dhahiri kipenzi chao ni mgonjwa taabani tumewasikia wakisema TUTAMPA KURA HUYOHUYO HATA KWA MACHELA TUTAMPELEKA IKULU! Ni unyumbu ulikuwa upo kazini! Ndioo! Nyumbu hawanamuda wa kufikiri hata kidogo! Husukumana na huigana matendo! 

Ni katika unyumbu huu watu walishindwa kufanya tafakuri yakina! Hata pale nyumbu mkuu aliposema atawaachia watu waliohukumiwa na mahakama ya juu kabisa nchini kwa makosa mazito kabisa bado nyumbu wadogo walirukaruka kushangilia!Si nyumbu? Hata pale wawindaji walipotuhumu kuwa nyumbu mkubwa nimgonjwa badala ya kuweka mkakati wa kuwaaminisha wapigakura kuwa nyumbu mkuu yuko ngangari wao ndio kwanza wanasema TUNATAKA HUYO HUYO MGONJWA! 

Tabia hii ya unyumbu imesababisha anguko kuu nililolitabiri liwe kweli! Hili ni anguko kuu kwa kuwa hakika mwaka 2020 watu watasita kugeuka nyumbu! Bahati mbaya sana barani Afrika ili upinzani uweze kushika dola unyumbu unahitajika.  Kwa kawaida huwa anatokea almaarufu (celebrity) ambaye anatengeneza manyumbu wengi! Huyu Almaarufu akijua kucheza politics of wildbeasts anawashangaza watawala. Akishindwa huwa anatoweka kama alivyochomoza! Ni kwa kuwa kwa bahati mbaya zaidi unyumbu haujirudii! Ukipita umepita.”FB_IMG_1447084057928Kama nilivyo sema hapo juu kuwa tuondoe huu ujumbe kwenye mazingira ya kisiasa na kuweka mazingira ya maisha yetu ya kawaida. Je wewe ni “Nyumbu?” Wewe ni wale watu ambao wanashabikia vitu bila hata kujua ukweli  au  undani wa jambo? Je wewe ni mmoja wa watu ambao wanashabikia ugomvi na kusambaza chuki juu ya mtu fulani kwasababu tuu rafiki yako au mtu fulani kasema au mtu fulani naye yupo kwenye hilo group basi nawe unafuata tuu bila kufanya uchunguzi wowote? Je wewe ni “Nyumbu” wa kuiga style fulani ya maisha just because so and so are living that life style? Binadamu wakaida mwenye akili zake zote timamu huwa lazima anamisimmo yake au muongozo yake inayo ongoza maisha yake. Sio kufanya ushabiki tuu wa kufuata mkumbo! Siyo kila kitu kizuri ni kwaajili yako au kinakufaa vingine unatazama halafu unageuza shingo upande wa pili na kuendelea na maisha yako! Acha ushabiki usio na tija! Acha kuwa “Nyumbu!”

Kutoka Facebook

FB_IMG_1446747037129Nimependa sana hizi picha ya Mh. ShyRose Bhanji na mrembo Wema Sepetu. Yani tazama nyuso zao inakuonyesha furaha fulani “amazing” hivi ambayo hata wewe kwa kuangalia tuu unapata tabasamu fulani hivi. Hii ilikuwa siku ya kuapishwa Rais Dr. Magufuli. Yani hawa ni warembo halafu ni wazalendo which makes them really hot! FB_IMG_1446761247444Hadi raha yani!  Yani mie napenda sana watu kama dada yangu huyu ShyRose Bhanji yani watu ambao wako free to express their feelings wanapokuwa na furaha au huzuni, dada fulani very down to earth kichizi yani! Japo kila mtu anauhuru wa kuishi anavyo taka lakini mie huwa damu yangu haiendani na watu wanaojiona wako juu ya wengi “Diva” just because za sababu zao ambazo wao wanaziona kuwa zinawafanya wao ni bora kuliko wengine! Watu wenye ‘nyodo’ fulani za kishamba yani! Anyway Mungu awabarikiwa sanaaaaaa warembo wetu wote wawili.

 

 

Mahojiano maalum: Zawadi Kakoschke

Naomba utueleze Historia yako kwa ufupi:FB_IMG_1446687026185Naitwa Zawadi Owitti Kakoschke. Mama wa watoto wawili Amani na Malaika na mke wa Bart Kakoschke. Nimezaliwa miaka 39 iliyopita huko Songea, Tanzania. Ni mtoto wa pili wa marehemu Fatuma ambae anatokea mkoani Iringa.

Zawadi na baba yake mzazi; mzee Owitti.
                                                 Zawadi na baba yake mzazi; mzee Owitti.

Mimi ni mjaluo baba yangu anatokea Shirati Rorya mkoani Mara. Kwa sasa makazi yangu yako kwenye nchi za kiarabu ambapo mume wangu anafanyia kazi. DSCN7873Wewe ni mmiliki wa blog ya maisafari.com, ambayo hata mimi ni shabiki mkubwa sana wa blog yako. Je nini haswa kilipelekea wewe kuanzisha blog yako? FB_IMG_1446687035620Nilitaka kuhamasisha watanzania wenzangu kupenda mambo ya utalii na kwa kiasi kikubwa nimefanikiwa kwa hilo. Nitatoa mfano nchi yetu ya Tanzania ina vivutio vingi sana lakini sababu hatuna utamaduni wa kupenda utalii watu wengi hawajaribu hata kwenda kuangalia ni kitu gani haswa kinawafanya watu watoke nchi mbali mbali kuja kutembelea nchi yetu. Mimi kama mtanzania ambae napenda sana mambo ya utalii nikaona kuna haja ya kuwahamasisha watanzania wenzangu kwa njia ya blog ambapo huwa naweka picha na maelezo mbali mbali ya nchi ambazo nimefanikiwa kutembelea.  FB_IMG_1446686789165Kusafiri ni moja ya mambo ambayo unapenda sana, unaweza kutuambia mpaka sasa umesha safari inchi ngapi duniani? Na inchi gani ambayo ungependa kufika lakini bado haujafika? Mpaka sasa nimebarikiwa kutembelea nchi kama thelathini na tano na miji mingi zaidi. Nchi ambazo nimefanikiwa kuzitembelea ni Tanzania, Kenya, Oman, Italy, Thailand, Cambodia, Australia, Singapore, Hongkong, Malaysia, UAE, England, France, Iceland, Switzerland, Qatar, Spain, Vatican City, America, Mexico, Cayman Island, Bahama, Jamaica, Colombia, Panama, Aruba, Portugal, St. Maarten, Malta, Us Virgin Island, Bonaire, Puerto Rico, Sri Lanka, Maldives and Holland, n.k. FB_IMG_1446686730179-1Zawadi, kusafiri kunahita fedha za ziada, je waweza kutueleza ni jinsi gani unaweza kumudu safari zako, nini haswa chanzo cha mapato yako kama utapenda kutuambia? Utalii unafanya kutokana na uwezo wako na si lazima uwe na pesa nyingi ndio uweze kutalii. Mimi kabla sijapata nafasi ya kutembelea nchi mbali mbali nilianza na utalii wa ndani kwanza ambapo nilifanikiwa kutembelea karibu mikoa yote ya Tanzania. Cha muhimu ni kujipanga tu kama vile unavyoweza jipanga kwa mambo mengine. Sisi huwa tunadunduliza kidogo kidogo mpaka pale tunapata pesa za kutosha na kuzitumia kwa ajili ya safari. Mimi na mume wangu tunapenda sana kusafiri kwa hiyo hatujisikii vibaya kutumia hizo pesa kwa ajili hiyo. Tunaamini pesa tunazotumia kwenye utalii hazipotea bure bali tunapata faida zaidi. FB_IMG_1446686604048-1Historia yako inaonyesha wewe ni dada wa Kitanzania ambaye umeolewa na mtu mwenye asili ya kizungu, je ilitokea tuu au ulikuwa na ndoto za kuolewa na mzungu siku zote? Nilikutana na mume wangu ambae anatokea Australia mwishoni mwa mwaka 2001 na mwanzo wa mwaka 2002 tulianza kuishi pamoja. Miaka miwili baadae tulifunga ndoa huko Sydney, Australia. Kusema ukweli siku ya harusi yangu ilikua ni siku ya furaha ya ajabu kwa sababu ndoto yangu imekua kweli.

Zawadi siku ya harusi yake
                                                 Zawadi siku ya harusi yake

Nimekua na ndoto ya kuolewa na hawa wenzetu toka nikiwa mdogo, nina sababu nyingi lakini kubwa sikutaka kuolewa na kuishi maisha ambayo mama yangu alikua anaishi ya UKE WENZA. Niliona kama nikitaka maisha ya ndoa yenye furaha basi ni mzungu tu ambae anaweza nipa hayo maisha ingawa kipindi hicho ilikua nayaona hayo maisha kwenye movie tu ha ha haaaa. Kitu kingine niliona wenzetu wazungu wamejifunza kuwa wakweli nami napenda sana watu wakweli. DSCN7906Unawatoto wazuri sana Amani na Malaika. Ilikuwaje ukawapa hayo majina ikizingatiwa umeolewa na “mzungu” wengi wangetarajia majina ya watu wenye asili hiyo? Asante, watoto ni zawadi kubwa namshukuru mungu kila siku. Nilitaka kuwaachia watoto wangu kumbukumbu ya nchi yangu Tanzania. Nilikua najua kila mara majina yao yatakapokuwa yanatamkwa lazima watu watakua wanauliza asili yake na hapo ndio habari ya mama yao inakuja katika picha. Namshukuru mume wangu alikubali kuwapa watoto wetu majina ya kwetu. FB_IMG_1442849273617Je, unawafundisha watoto wako Kiswahili na natamaduni zingine za Kiafrica haswa Tanzania? Pili huwa unapika vyakula vya kiafrika kwa familia yako? Ni chakula gani cha kiafrika ambacho wanapenda? Nasikitika kusema nimefeli kidogo katika suala la kiswahili mpaka sasa bado hawajui. Ni kosa langu mimi mama yao sikulichukulia kwa nguvu zaidi ambapo sasa ndio naona makosa yangu maana jinsi wanavyokua ndio inakua vigumu zaidi. Ila sijakata tamaa bado naendelea nao kuwafundisha maneno mawili matatu kila siku. Najitahidi sana kuwafundisha utamaduni wangu na mara kwa mara najitahidi pia kupika chakula cha kikwetu. Napenda sana chakula cha kitanzania na watoto wangu wanapenda sana nikipika chapati, maandazi, wali na maharage. Ukiwauliza wanapenda chakula gani cha kitanzania basi nina uhakika watakwambia chapati.

Amani (kushoto) na Malaika
                                                                   Amani (kushoto) na Malaika

Wewe binasfi unaamini majina ambayo wazazi wana wapa watoto wao yanachangia katika mafanikio yao kiuchumi, kielimu, na tabia zingine? Kwa mfano majina kama Amani anaweza akawa mtu wa kupenda amani siku zote, au majina kama Tabu, Sikujua yanaweza yaka changia mototo kuwa na matatizo katika maisha yake? Majina yanachangia sana katika maisha ya watoto wetu. Ndio maana mimi nilijitahidi sana kukaa na kufikiria majina ya kuwapa watoto wangu. Nimekua naamini hili kwa miaka mingi sana kuwa majina yana nguvu sana katika kujenga au kubomoa maisha ya muhusika. Huwa nashukuru sana kwa wazazi wangu kuamua kunipa jina la Zawadi nina imani kubwa hili jina limenisaidia kwa namna moja ua nyingine.

Kama mama mwenye watoto wenye asili mbili tofauti, ni changamoto gani unapata katika malezi yao, haswa katika maswala ya maadili, na utowaji wa adhabu pale mototo anapo kosea? Changamoto ni kubwa sana kwa kweli na hapa ndio unaweza kuona kuna utofauti mkubwa sana kati ya utamaduni zetu mbili. Nina imani waafrika wengi walioolewa na wazungu wanakumbana na ili tatizo. Mvutano wake ni mkubwa hasa kwenye maswala ya maadili na utoaji wa adhabu kila upande unaamini wenyewe ndio wanajua jinsi ya kulea zaidi.

Sisi tumeaumua kuchukua maadili mazuri toka pande zote mbili na kuacha mabaya. Ila bado wakati mwingine tunavutana maana watoto wanafurahia zaidi maadili ya wenzetu maana yako malaini na ya kudekeza sana. Mimi nachofanya ni kusimama na msimamo wangu wa kuunganisha mazuri toka pande zote mbili kwa namna hii nina imani tutafanikiwa kulea watoto wenye tabia nzuri na watakaua wamefaidika kutoka pande zote mbili.

Zawadi na familia yake
                                                                             Zawadi na familia yake

Unasafiri sana na mara zote huwa upo na familia yako yote (mmeo na watoto). Je nichangamato zipi huwa unapata maana nafikiri ni ngumu sana? Au huwa unakuwa na msaidizi (dada wa kazi)? Changamoto haziwezi kukosekana hasa ukiwa unasafiri na watoto wadogo. Ila faida zake ni kubwa ambapo hata hizo changamoto hazina nguvu tena. Mimi na mume wangu tunapenda kulea watoto wetu wenyewe kwa hiyo hatuna msaidizi wa watoto. Msaidizi tulie nae ni wa kusafisha nyumba tu ambae anakuja mara mbili kwa wiki. FB_IMG_1446686812537Ni ushauri gani ungependa kuwapa wakina mama ambao wanapenda kusafiri lakini wanaogopa kwa sababu ya watoto? Faida ya kusafiri na watoto ni kubwa kuliko matatizo. Sidhani kama mama ambae amezoea kulea watoto wake anaweza ogopa kusafiri nao. Hata unapokua safarini watoto unawalea kama ulivyozea kuwalea kinacho badilika ni mazingira tu ambapo kwa watoto ni rahisi sana kubadilika na kufuata mazingira waliyopo.

Tena unakuta wao ndio wanafurahi zaidi kuliko hata sisi wakubwa. Nawashauri wamama wenzangu tafadhali usiwaache watoto nyuma beba watoto wako nenda kawape kumbu kumbu na nafasi ya kujifunza mambo mapya yatawasaidia sana kwenye maisha yao ya baadae. Pia ni faida kubwa kwako mzazi maana ukiwa holiday unatumia muda wote kuwa pamoja na watoto wako na unajenga familia iliyokomaa na yenye kumbukumbu nzuri pia unawajengea watoto wako sifa ya kujiamini.

Unawezaje kumudu majukumu yako kama mama, mke, na kuendesha mambo ya kiuchumi ndani ya familia? Ni mgawanyiko unachagua kipi muhimu kwako kwanza. Mimi nimechagua kuwapa watoto wangu muda wangu zaidi kipindi hiki wakiwa wadogo kwa kuamua kua mama wa nyumbani ili nipate muda mzuri wa kuwalea. Kwa kukaa nyumbani napata muda wa kujihusisha na shughuli mbali mbali za maendeleo ya watoto wangu, na uamuzi huu umeniwezesha kujenga familia yangu na kuwa yenye furaha sana. Pia nipatapo muda najitahidi kujishughulisha na shughuli za kiuchumi za familia.

Zawadi, wewe ni mama ambaye unawatoto wawili lakini bado uko vizuri kabisa kama mdada ambaye hana watoto. Ni nini unafanya kujiweka katika hali hiyo? Hii ni changamoto kubwa nadhani sio kwangu tu ila kwa wamama wengi, hasa sisi tunaokua nyumbani unaweza kujisahau kabisa. Kwangu mimi changamoto niliyonayo ni mwili wangu ni rahisi sana kuongezeka kwa hiyo mara kwa mara lazima niwe kwenye diet na mazoezi maana bila hivyo naweza kuongezeka kupita kiasi, nikiongezeka nakosa raha kabisa maana napenda utanashati.

Nashukuru kwa namna hii inanisaidia kunikumbusha kuwa kuzaa isiwe sababu ya kuharibika na kwa sababu napenda kupendeza basi najikuta lazima nitafute muda wa kujipenda mimi. Weekend ni muda wangu mimi siku hizi mbili ni jukumu la mume kuangalia familia na mama huwa napumzika kabisa kama nikiamua kukaa nyumbani nawaachia mume na watoto wanilee mimi. Nikiamua kutoka basi utakuta naelekea shopping au spa au kutembelea marafiki, kwa staili hii najikuta napata muda wa kupumzika na kuwa na furaha muda wote.

Zawadi katika wedding Anniversary yake. Dubai-2014
                                          Zawadi katika wedding Anniversary yake. Dubai-2014

Siku hizi tunasoma kwenye blogs mbali mbali na kusikia baadhi ya wakina dada wa Kitanzania wana amini kuwa kuolewa na “mzungu” au mtu mwenye ngozi nyeupe ndio njia pekee ya kujikwamua si tuu kiuchumi bali hata kimapenzi. Je wewe unalionaje swala hili? Na nini ushauri wako kwa wadada hawa? Hili ni swali ni gumu kwa kweli ila nitajitahidi kujibu kwa mtazamo wangu ambao kwa kiasi kikubwa umechangia kwenye maisha yangu. Mimi binafsi naamini kuwa kuolewa na mzungu asilimia kubwa una nafasi ya kujikwamua kiuchumi pia kupata mapenzi ya dhati. Sisemi kama watu weupe pekee ndio wanaweza kukukwamua kiuchumi hata pia watu weusi. Ila kwenye mapenzi ya dhati nadhani kura zangu zote napeleka kwa wazungu. Wenzetu wanaheshimu mwanamke na akipenda amependa yuko tayari kufanya chochote kuonyesha upendo wake. Hapo ndio tunakuja kwenye suala la uchumi mzungu akikupenda yuko tayari kukufanyia chochote kile utakacho, anachojali yeye ni furaha yako.

Ushauri wangu ni kwamba kila kitu kina pande mbili nzuri na mbaya. Wazungu pia nao ni binadamu kama binadamu wengine wana mabaya na mazuri yao. Nawashauri kabla hawajajitumbukiza kwenye maisha ya hawa watu kwanza wachunguze je watawezana nao hasa kwenye upande wa pili ambao si mzuri? Maana naona wengi wanaangalia upande mmoja tu ambao ni mzuri. Inachukua muda mrefu kwa wazungu kutuamini sisi Waafrika maana wengi wanaamini kuwa Waafrika hatuna mapenzi ya kweli na wengi wetu ni waongo sana na hakuna kitu ambacho mzungu anachukia kama uongo.

Zawadi na mumewe
                                                              Zawadi na mumewe

Hata kama anakupenda kiasi gani akishagundua tu kuwa wewe una vitabia vya uongo lazima atakukimbia tu. Kwa hiyo ushauri wangu mwingine kwa kina dada ambao wanapenda kuolewa na hawa watu kuwa wakweli kuanzia mwanzo, hata kama una vitabia vibaya wewe usijali mzungu akikupenda amekupenda yuko tayari kukusaidia kubadilisha hivyo vitabia au hata kuvumilia kuishi navyo maana wenzetu wana mapenzi ya dhani na ikitokea kama hatoweza au ajapendezwa na hivyo vitabia basi atakwambia ukweli mapema. Asilimia kubwa ya wazungu akikupenda amekupenda na yuko tayari kusimama kwa ajili yako kwa jambo lolote ila lazima uwe mkweli. Kwa kina dada wote ambao ndoto zao ni za kuolewa na hawa wenzetu mimi nasema usikubali mtu yoyote akukatishe tamaa, endeleza ndoto yako maana faida yake ni kubwa kuliko hasara.

Marehemu mama yake Zawadi.....R.I.P
                                                      Marehemu mama yake Zawadi…..R.I.P

Zawadi, wewe ni dada ambaye mzazi wako mmoja (mama mzazi) hayupo nawe tena. Uliwezaje kupata nguvu ya kuendela na maisha bila kukata tamaa, maana kuna watu wengi ambao wameshindwa kuendelea au kukata tama ya maisha baadaya ya kuondokewa na mzazi au wazazi wao? Kwa kweli nimepitia matatizo mengi sana namshukuru Mungu hakuweza kunitupa alinilinda na kufanikiwa kuvuka vikwazo vingi sana katika maisha yangu. Usiombe ufiwe na mama hasa ukiwa na umri mdogo maana nguzo kubwa ya familia Afrika ni mama. Mimi nilipoteza mama nikiwa na miaka kumi na tano huku nikiwa na wadogo ambao walikua wadogo zaidi, mdogo wangu wa mwisho aliachwa akiwa na miezi kumi tu. Kusema kweli nimepitia kipindi kigumu sana mapaka kufikia hapa nilipo ila namshukuru mwenyezi Mungu hakuweza kunitupa.

Zawadi na mdogo wake aitwaye Tina
                                         Zawadi na mdogo wake aitwaye Tina

Hili swali hili huwa linanipa wakati mgumu sana maana kumbu kumbu zote huwa zinarudi mtanisamehe kama nitakua nimejibu kwa kupitiliza maana kuna mengi sana ila nitajitahidi kujibu kwa ufupi zaidi. Hakuna kitu kibaya hapa duniani kama dharau, usimdharau mtu hata siku moja maana uwezi jua huyo mtu siku moja atakua wapi. Pale mama alivyofariki tu ndio tulianza kujua rangi halisi ya ndugu zetu na zinasikitisha kwa kweli.

Namshukuru Mungu alinipa ujasilia wa hali ya juu na kuweza kusimama na kusaidia wadogo zangu pia. Ilibidi nikue kwa kasi ya ajabu ili niweze kuwasaidia wenzangu ambapo kwenye umri wa usichana badala ya kufurahia maisha mimi nilikua najiuliza nitawalishaje wadogo zangu, vipi wana nguo za kuvaa, je school fees safari hii nitaipata wapi. Kwa namna hii sikuweza kupata bahati ya kuendelea na elimu ya juu na kuamua kutafuta kozi fupi fupi ambayo ingeniwezesha kumaliza mapema na kupata ajira ili niweze kupata mshahara ili niweze kuwasaidia wadogo zangu. Na kwa bahati mbaya mpaka leo bado sijaweza kukamilisha hii ndoto ya kupata elimu ya juu ila bado naamini kuwa kila kitu na wakati muda muafaka utafika ambapo kutakua hakuna kipingamizi kitakachosimama kati yangu na ndoto yangu ya mwisho. Nina imani lazima nitalikamilisha sababu ni kitu ambacho napenda. FB_IMG_1446692135293-1Mimi ni mpiganaji na ambae sikati tamaa kirahisi na hiki ndicho kimenisaidia kufika hapa nilipo. Nilikua najua nataka nini na sikuacha kutafuta nachokitaka. Nilipitia vizingiti vingi lakini havikunikatisha tamaa kabisa na pale nilipoona karibu naanza kukata tamaa nilisali sana maana mwenyeji Mungu pekee ndio alikua anaujua moyo wangu, kwa asilimia mia nilikua nina uhakika siku moja atanisaidia tu na kunipa maisha ambayo nayataka, imani hii iliendelea kunipa nguvu kwa kiasi kikubwa sana.

Kitu kingine ambacho kilinisaidia ni kuthamini watu wa aina yote, nilijitahidi kuwa na upendo kwa watu wote, kwa namna hii iliniwezesha kuishi na watu wa aina tofuati ambao wengi walinisaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha maisha yangu. Yaani siwezi kuwasahau watu wote ambao walinisaidia kipindi hicho wengi ni watu baki ambao hatuna uhusiano wowote. Kitu ambacho hawakuja ni kwamba msaada wao ulikua ni mkubwa sana kwangu.

Nachofanya siku hizi kila nipatapo nafasi ya kukutana na hao watu nawakumbusha na kuwashukuru ambao karibu wote wameshasahau hata kama waliwahi nisaidia nini. Kutokana na msaada wao walionipa enzi hizo umenifanya hata mimi pia kuwa na tabia ya kupenda kusaidia watu wa aina tofauti bila kujali wanatokea kwenye mazingira ya namna gani. Pia huwa najitahidi kusaidia pale ninapoombwa msaada hasa kwa watu ambao nina uhakika msaada wangu utawasaidia kwa kiasi kikubwa.

Huwa naamini msaada ni msaada hata uwe mdogo kiasi gani kwenye macho yako lakini kwa anayesaidiwa ni kitu kikubwa sana kwake. Nakumbuka kuna siku nilisaidiwa na mtu nauli tu ya daladala ya kwenda kazini hapo nilikua sina pesa hata ya nauli ya kwenda kazini. Msaada wake uliweza nifikisha ofisini na hapo niliweza pata pesa ambazo ziliweza kusaidia kupata chakula cha wadogo zangu siku inayofuata pia nauli yao ya kwenda na kurudi tution. 2015-11-05 07.25.45Mtu gani ambaye wewe unamuangalia kama kioo chako (your role model), na kwanini? Huwa navutiwa sana na watu ambao wana moyo wa kusaidia wengine kwa namna moja au nyingine. Na Oprah ana sifa hiyo kubwa. Nimejikuta najifunza, nacheka, nasikitika, nalia na hata kupata nguvu mpya kipindi chote nilichokua naangalia show zake.

Pia nimejifunza mengi kutoka kwenye magazeti yake kwa miaka mingi nimekua msomaji wake mkubwa. Napenda karibu kila kitu kuhusu Oprah kasoro kwenye suala la mbwa tu lol! Mimi ni mmoja wa wale watu wanaoamini kuwa mnyama ni mnyama na alelewe kama mnyama na sio kama binadamu, mtanisamehe kwa wale ambao nime wakwaza naelewa maana mume na watoto wangu hawakubaliani nami kwa suala hili.

Zawadi Kakoschke Blogger was www.maisafari.com
                                Zawadi Kakoschke Blogger wa www.maisafari.com

Ujumbe au ushauri wowote kwa wamama wenzako: Tupendane! Hakuna kitu kizuri maishani kama upendo maana upendo unajenga heshima, furaha, amani na mengine mengi. Sisi kama kina mama tunajukumu la kulea watoto wetu ambao baadae wataongoza taifa letu. Sasa kama sisi kina mama hatutakua na upendo ina maana tunawajengea watoto wetu taifa ambalo litakua na majanga huko mbeleni.

Ushauri au ujumbe kwa wadada au wanawake ambao hawajaolewa na wangependa kuolewa: Kwanza kabisa jiheshimu na jitambue wewe ni nani na unataka nini. Baada ya hapo mtangulize Mungu mbele ili aweze kukuchagulia mume mwenye upendo. Ila usiache kutafuta kile unachotaka hata Mungu nae anakubali kubembelezwa hasa pale anatakapokua amekuletea mume ambae humtaki ni ruksa kuomba kubadilishiwa.

Mimi pia nilimbembeleza Mungu anitafutie mume mwema mwenye upendo ila sikuacha kuweka kwenye sala zangu na kusema tafadhali naomba awe mzungu maana nilikua najijua nisingeweza kuwa na furaha ya ndoa kama angeniletea mume wa kutoka kwetu. Ingawa wanasema kuwa si vizuri kumchagulia Mungu yeye anajua zaidi, lakini pia Mungu ni mwenye upendo wa dhati angependa kukuona ukiwa na furaha. Kwa hiyo wapendwa usiache kumbembeleza ili aweze kukupa kile unachotaka. Kwangu mimi kanipa kile nilichoomba kabisa kwa kweli mwenyezi Mungu yupo na anasikiliza maombi yetu siku zote.

Na mwisho, ujumbe kwa Watanzania wenzako: Tuache tabia ya kupenda kuhukumu watu hasa tusio wajua na tuache chuki zisizo na msingi. Utakuta mtu hata hakujui lakini utakuta ameshakupa hukumu ya hatari utadhani anakujua, hiyo yote ni chuki ambayo ni mbaya sana. Tupendane jamani upendo ni kitu cha bure na chenye mafanikio makubwa.

Asante sana Zawadi.

Source: Mahojiano haya yamefanywa na Alpha Igogo

Hot shot of the day

DSCN6469-1-1O’my gosh! What a pretty natural looking lady! Praise the Lord! DSCN6470-1 Tina Owitti from Bongoland. She’s Hotttt! Vitu toka kanda ya ziwa hii ??? jamani msinune nafurahisha genge tuu. Wanawake wote ni wazuri.

Kwaheri ya kuonana mama Salma Kikwete!

phoca_thumb_l_salma-kikweteKwaheri mama Salma Kikwete. Asante sana mama yetu kwa kuliwakilisha vyema taifa letu na wanawake wa Kitanzania kwa ujumla. BarackObamaJakayaKikweteSep242013Umekuwa mfano bora kwa wanamama wenzio, wanawake wadogo, na mabinti zetu ndani na nje ya Tanzania. Sisi hatuna chakukulipa zaidi ya kusema asante sana mama. Kazi umefanya vizuri na sasa tunakutakia mapunziko mema. FB_IMG_1446730522248Wewe ulikuwa mama ambaye hauna makuu, hauna makeke wala mawenge. Mama mwenye staha unayejua kujishusha! Salma+Kikwete+Camilla+Prince+Charles+Visit+owBbwbefbdfl-2Tuta  ku-miss na mavazi yako ya vitenge. Uliweza uzalendo mbele ukapenda na kutukuza vya kwetu. Wewe unajitambua na kujikubali ndio maana haukuwa limbukeni. Mfano nzuri umeonyesha! 1468740_635714213159231_1778663487_n-1 Najua wewe sasa ni “kungwi” hivyo umemfunda vyema ‘mwali’ wako mama Janeth Magufuli! Tunatumaini naye atafanya vyema napengine  zaidi yako wewe. BveaAMmIQAAl0BM-1 Asante sana, na kwaheri ya kuonana tena. Ubarikiwe siku zote!

Hot shot of the day

FB_IMG_1446565532087-1Beuty runs in our family blood ?? Nimependa hii picha ya my cousin-sister May C. Igogo. Huyu ni binti wa baba yangu mkubwa. Baba yake na baba yangu ni brothers wa baba mmoja mama tofauti. Bibi yake May alikuwa ndo alikuwa mke mkubwa wa babu. Bibi yangu mimi alikuwa mke wa tatu kati ya watano ??? “welcome to the Luo land” ??? Anyway, she is hot!

Kandi Burrus real talk!

“Hey ya’ll, serious talk. In life we all have struggles and nobody’s struggle are worse than others – if they were measured in value that would mean people would be measured in value. We are all of the same, living breathing. Please support each other. Uplift each other. Give praise to each other. If someone TRIES, congratulate them. Life is no competition in itself. It is fun to compete, sure, but we are all here to love and and experience love to the fullest. If there is anything about me that I hope stands out is that I SUPPORT YOU MY LOVES. #RealTalk. Love ya girl, Kandi. ” FB_IMG_1446563906858I love  the message,  I decided to share with you!

Kutoka Facebook

FB_IMG_1446561012745Muda mrefu nilikuwa sija muweka huyu mrembo wetu humu ? kapendeza sana. Majira ya baridi yameanza kunukia kwahiyo makoti yanahusika sana wakati huu!

Kitchen party ya bure kwa ‘single’ men!

1. Mwanangu, mwanamke anaweza kuwa mkeo, mwingine anaweza kuwa mama wa watoto wako, lakini ukipata mwanamke ambae atakuwa kama mama kwako, mama kwa wanao na mama kwa familia, tafadhali mwanangu usimuache huyo!

2. Mwanangu, usimfanye mwanamke wako kuwa ndio wa kupika na kufanya kazi zote za jikoni peke yake, tabia hiyo sio nzuri Kwani hata nyakati zetu, mashamba yetu yalijulikana kwa majina yetu wanaume lakini tulifanya kazi pamoja!

3. Mwanangu, nikikwambia wewe ni kichwa cha familia, simaanishi kutuna kwa pochi lako, usiangalie kabisa pochi yako, angalia kama utaona tabasamu usoni kwa mke wako. Pesa sio kila kitu katika ndoa na haileti ukuu wa familia!

4. Mwanangu, ukitaka kuwa na maisha marefu na ukapunguza misongo ya mawazo, ongea na mkeo pangeni bajeti ya mahitaji yenu, kisha mwache mkeo awe na jukumu la kuratibu mahitaji ya kila siku ya familia kwa kumkabidhi fungu husika hata kama limetokana na michango yenu wawili. wanawake wanajua sana kupanga bajeti na hii haitakuwa rahisi kwa yeye kutumia hela hovyo wakati akijua kuwa nyumbani kuna mahitaji ya msingi, lakini hela zikiwa mikono mwako ataendelea kuomba hata kama utakuwa umeishiwa!

5. Mwanangu, Usithubutu kumpiga mkeo, maumivu ya kipigo hukaa ndani ya moyo wake kwa muda mrefu sana na huacha kidonda ambacho hukawia sana kupona. Ni hatari sana kuishi na mwanamke mwenye majeraha moyoni!

6. Mwanangu, sasa unaamua kuoa,kama bado utaendelea kuishi maisha kama ya ubachela na mke wako, sio muda mrefu utakuwa bachela tena. ukioa Badilika anza kuishi maisha ya mke na mume!

7. Mwanangu, zamani,tulikuwa na wake wengi na watoto wengi kwa sababu tulikuwa na mashamba makubwa na mavuno yalikuwa makubwa, lakini kwa sasa maisha yamebadilika, kwa hiyo mkumbatie mwanamke wako peke yake kwani hakuna ardhi tena na mahitaji ya watoto ni makubwa sana. Angalia ukubwa wa familia yako!

8. Mwanangu, chini ya mwembe ambao nilikuwa nikikutana na mama yako inaweza kuwa ni hoteli kubwa kwa nyakati zenu,lakini kumbuka, kitu pekee tulichoweza kufanya chini ya mwembe ilikuwa ni kukumbatiana pekee.nakushauri ukikutana na marafiki wa kike kikubwa unachoweza kufanya nao ni kupeana mikono na ikizidi ni kukumbatiana hadharani sio vinginevyo!

9. Mwanangu, usibadilike mara utakapoanza kupata mafanikio Zaidi, kuliko kuwahudumia hao viruka njia wa mtaani ambao hawajui mmetoka wapi na mkeo, nakushauri utumie na kufurahia mafanikio yako na mkeo ambae aliweza kusimama imara wakati wote wa mapito yenu magumu.

10. Mwanangu, kumbuka unapoanza kusema au kuona mke wako kabadilika, ujue kuwa kuna kitu ambacho ulikuwa ukikifanya umeacha kukifanya. Jitathmini na anza kufanya au kutimiza wajibu wako.

11. Mwanangu, usijaribu kumfananisha au kumlinganisha mke wako na mwanamke mwingine wa nje, kwani hata yeye anakuvumilia sana na hajakufafanisha na mwanaume mwingine yoyote huko nje na ndio maana aliamua kuwa na wewe.

12. Mwanangu, sasa hivi kuna hiki kitu kinaitwa haki za wanawake, sawa,kama mwanamke anasema ana haki sawa na wewe katika nyumba, basi gawanya mahitaji yote ya ndani kwenu katika sehemu mbili zilizo sawa,halafu timiza nusu yako na mwambie atimize nusu iliyobaki.

13. Mwanangu, nilimuoa mama yako akiwa bado kigoli (bikra) na nilikuwa naenda sana kwao kabla sijamuoa, lakini kutomkuta mkeo bikra kusikufanye umlaumu kuwa alikuwa muhuni, kumbuka wanawake wa enzi zetu na wasasa ni tofauti, ulimchagua mwenyewe na ukigoli wake hukuujua kabisa. Usiingize mambo ya kabla ya ndoa kwenye ndoa yenu.

14. Mwanangu, sikuwapeleka dada zako shule kwa kuwa nilikuwa mjinga kama wazee wengi wa hapa kijiji wasemavyo, tafadhari usifanye ujinga huu, kwani kiwango cha mafanikio ya wanawake sasa kimefanya wanaume waonekane ni watu wa kawaida sana na sio muhimu kama enzi zetu. Ukijaliwa watoto wape elimu.

15. Mwanangu, zamani enzi za ujana wetu, wanawake walikuwa na urembo wa asili, ingawa siwezi kukudanganya, wengine waliongeza urembo kwa kujichora hina na hata kutoboa pua na masikio lakini usisahau hawakuonyesha maumbile yao nyeti hadharani kama sasa. Hakikisha mkeo analijua hili!

16. Mwanangu, mama yako na mimi hatuna hisa katika kila kitu kinachoendelea kwenye maisha yenu, jaribuni kutatua changamoto zenu wenyewe bila kila mara kuja kwetu kuomba usuluhishi. Ndoa ni pamoja na ukomavu wa kutatua changamoto zenu bila kuziuza kama gazeti kwa kila mtu.

17. Mwanangu,nilimnunulia mama yako kifaa cha kupikia vitumbua ili aanzishe mradi wa kuuza vitumbua, pia nilimsaidia kununua cherehani yake ya kwanza, tafadhari msaidie mke wako kutimiza ndoto zake kulingana na uwezo wako kama ambavyo unahangaika kutimiza ndoto zako.

18. Mwanangu, usiache kutusaidia mimi na mama yako, utu uzima una changamoto nyingi sana na Mungu akikujalia utaziona muda ukifika. Pamoja na kutimiza majukumu yako kama baba wa familia kumbuka pia bado tunaishi na wewe ni mtoto wetu.

19. Mwanangu, kila upatapo muda wa kusali, Sali na familia yako, kuna kesho ambayo huijui, ongea na MUNGU wako ambae anajua kila kitu kila siku!

20.NAKUTAKIA MAISHA MEMA YA NDOA MWANANGU….NAKUPENDA!  FB_IMG_1446564022249

N.B: Ujumbe huu nimeupenda nikaona ni share nanyi. Nimeutowa Facebook na nafikiri huyu kwenye picha ndiye aliye andika maana ujumbe umeambatanishwa na hii picha. Natumaini kuna kitu mtu ataambulia. Hata kwa wanawake pia.

Happy birthday “Ma Watatu”!

FB_IMG_1446495921228A very happy birthday wishes to mama wa jeshi la mutu 3! Mama wa mahanjumati ?? Wajina wa mama yangu! Ubarikiwe sanaaaaaa, wewe na familia yako yote. Happy birthday darling, enjoy it!

Happy 72nd birthday greetings to Mamkubwa!

FB_IMG_1442162911883-1Napenda salamu hizi za kheri ya siku ya kuzaliwa zimfikie mama yangu mkubwa Mrs. Musira, aishie pale maadadui wa Kamnyonge, ndani ya jiji la Musoma. Miaka 72 katika duniani hii ya Musa si mchezo ati! Mungu aendelee kukulinda, akupe nguvu, afya tele, na furaha moyoni mwako. Happy 72nd birhday to you! Ubarikiwe sana mama!

Family time-sisters sisters!

FB_IMG_1446388980579Sisters sisters!  Wamependeza sana. Hawa ni cousin-sisters wanaishi New York State. FB_IMG_1446388940141Hawa upendo wao ni original kabisa siyo manufactured from China ? yani wanapendana ile yenyewe ya kweli kabisa ? FB_IMG_1446388945409Mbarikiwe sana wapendwa!

Hongera sana Bernard Chisumo!

FB_IMG_1446389276131-1Hongera sanaaaaaa Bernard Chisumo kwa kwa kimaliza masomo  yako ya degree ya kwanza na pass with flying colors “Honors” Mungu azidi kukubariki sana wewe na familia yako, akakujalie zile ndoto zako zote zitimie . Amani, upendo, na furaha vikatawale  nyumba yenu siku zote. Hongera sana shemeji yake na mimi ?? FB_IMG_1446389269691Bernard amehitimu degree yake  ya Computer Science in Software Engineering  kutoka katika chuo kikuu cha Surrey kilichopo katika inchi ya Malkia Elizabeth! Familia yake nao walikuwa kumpa  hongera baba kwa hatua aliopiga kama wanavyo onekana kwenye picha. Kwenye picha ni Bernard, mke mwema, na watoto wake Bernard. FB_IMG_1446389250260Binti kipenzi, naye alifuraha sana, kwa kusema ‘congrats dad, you made me proud’!  FB_IMG_1446389304414Like father like son! Naye ametoa ahadi za kufuata nyao za baba yake. Kwamba nayeye lazima siku moja alivae hilo John na kofia kama baba alivyofanya. FB_IMG_1446389321417Hongera sana shemeji yangu, ubarikiwe sanaaaaaa milele zote!

Family time-the Mabadas’

FB_IMG_1446389191805Baba, mama, na mtoto wa kiroho furahia weekend pamoja. Mbarikiwe sana. FB_IMG_1446389211387Baba na bintie, wamependeza sana. FB_IMG_1446389230398Mbarikiwe sana wapendwa.

Happy birthday Mama Ngonyani!

FB_IMG_1446259691945Kheri ya siku ya kuzaliwa kwako dada yangu mama Ngonyani. Mungu akulinde, akupe afya njema, upendo, amani, na furaha nyingi mno. Ukaishi  maisha marefu, ufanikiwe kuwaona wajukuu na vitukuu vyako! FB_IMG_1446259714497Upendo na Amani vizidi kutawala katika ndoa yenu. Mimi nashukuru sana kwa Mungu kwa kuniwezesha kufahamiana na nyinyi. Upendo wenu kwangu mimi na mwanangu  ni mkubwa sana. Na nasema asante kwa upendo wenu mbarikiwe mara dufu! FB_IMG_1446259577709Mkabarikiwa sana nyinyi  na uzao wenu wote. Happy birthday Mama Magreth and Cynthia. Enjoy your day!

Hot shot of the day

FB_IMG_1446233146359Mtani wangu (kushoto) na rafiki yake kutoka New York City. Wamependeza sana. Love everything! Mbarikiwe.

A million dollar smile!

FB_IMG_1446214162776What a beautiful smile from a beautiful lady! Yani hii ni tabasamu lakutoka chini ya “sakafu” ya moyo wake (in Lowassa’ voice) ?? kwakweli amependeza sana na hilo tabasamu ndio limemfanya a onekana mrembo mara 1000! Heshima inahusika sana, mke wa mtu huyu!

Mjane wa Deo Filikunjombe awashukuru Watanzania!

Screenshot_2015-10-29-19-57-27-1Kwakupitia account yake ya IG mjane wa Filikunjombe ametoa shukran zake za dhati kwa Watanzania wote walioguswa (kuna wengine hawakuguswa kama Joyce Kiria) na msiba wa mumewe. Amesema yeye hana chakuwalipa kwa upendo na ukarimu walio muonyesha. Pia wale ambao hawakuguswa na kifo cha mumewe nao amewashukuru. Na wale ambao hawakuguswa nawakaona njia pekee ya kumfariji ni kumuongezea machungu kwa kumuongelea mme wake vibaya nao amewashukuru kwa kusema amemuachia Mungu! Soma ujumbe wake hapa chini ?      Screenshot_2015-10-29-17-41-44-1 Mjane wa Filikunjombe ameumizwa sana na maneno ambayo Joyce Kiria wa Wanawake Live Show aliyasema kwenye social media kuhusu nyumba ya marehemu. Joyce bila huruma wakati watu wakiwa wanakusanyika kwa msiba wa Deo pale nyumbani kwake Mtomi Kijichi aliandika post ambayo ilikuwa ikionyesha nyumba ya marehemu na nyumba mbovu ya manyasi kama mfano wa maisha ya mwanasiasa wa CCM na maisha ya Mtanzania wa kawaida! Hiyo post aliandika kama ifuatavyo:- ? Screenshot_2015-10-26-19-29-34Joyce Kiria, wewe unajiita “Super Woman” kwakweli mimi nakuita ‘Super Mchawi!!’ kwani uliyo yatenda ni uchawi mtupu!! Yani wewe mwenzako kafiwa na mumewe katika ajali mbaya namna ile, kaachwa mjane wakati angali “mdada mbichi” kabisa na watoto wadogo watatu wote wakiwa chini ya miaka kumi na nane!! Lakini hayo yote hukuona cha kuongelea isipokuwa nyumba yao?! Kweli?? Unajua mchawi si lazima atembee na hirizi na tunguli shingoni bali matendo na maneno yake yanatosha kuwa mchawi!! Na wewe ume-qualify kuitwa Mchawi!! Jifunze kufurahia maendeleo ya wengine, bariki wengine nawe utabarikiwa. Kila mtu anafungu lake ambalo Mungu amemuandalia; lini na wapi atakupa hiyo ni siri yake Muumba! Kwahiyo usiumie sana kuona wenzako wamebarikiwa sasa kama nawewe ungeacha roho ya kichawi labda Mungu naye angekubariki wakati huu. Lakini kwa roho hii utangoja sanaaa!! Halafu hujui watu wamepitia wapi mpaka kufika hapo walipo ‘when you see the glory ask for their story!’ Shame on you!!

Pole sana mjane na watoto wako, pamoja na ndugu, jamaa, marafiki, na Watanzania wote. Mungu awape faraja na nguvu ya kuhimili kipindi hiki kigumu. R.I.P Mh. Deo Filikunjombe.

Mrs Nyongo!

image-2Mrs Nyongo katika ubora wake! Japo hajasimama lakini bila shaka hata wewe ni shahidi kuwa vazi lipo mwake ati! Kapendeza sanaaaaaa! Ubarikiwe mke mwema ??

Blog