Aren’t they cute?! Wamependeza sana halafu wazurije! Regina umebarikiwa watoto wazuri sanaaaaaa na familia nzuri mno, hongera! Nyie ni warembo sana ? safi sana, mother and son ?Dada na kaka, wazurije sasa. Wamependeza sana ? Mbarikiwe sana wapendwa ??
Happy 4th birthday to my darling niece -Essy
Napenda kumtakia mpwa wangu kipenzi cha roho yangu kheri ya siku ya kuzaliwa. Essy ametimiza miaka 4 siku ya leo. Naomba Mungu ajalie maisha marefu na mazuri, awe na afya njema, amlinde na maadui na mapepo yote ya dunia hii. Essy ni mtoto wa mdogo wangu anaye nifuata. Hapa nilikuwa nimekwenda kuwasalimia kwao mwaka 2013 akawa ameamka na kuni kiss kama unavyo muona. Ma’am I need to visit Bongoland ASAP ? Hapa ni Essy na wazazi wake walikuwa nyumbani kwa kaka yangu mkubwa (first born) huko Kunduchi Beach. Siku hii kaka yangu alinichinjia Mbuzi na Kondoo na kuita familia yote kwenda kula kwake. Ni kawaida kwa kaka yangu kunichinjia na kufanya family dinner kwakuwa mie sikai Tanzania hivyo atuonani mara kwa mara. Wazazi wa Essy wanakaa Mbezi Africana hivyo wao hutembeleana mara kwa mara na kula BBQ mara nyingi.Hapa Essy na wazazi wake pamoja na mdogo wake Evin. Walikuwa Serena hotel for some family dinner. Once again Happy 4th birthday my cutie pie, aunt Alpha miss you and love you so very much ????
Family time -the Lyimos’
Hot shot of the day
Isn’t she gorgeous! Aika you are very-very beautiful my dear! You’re becoming a ‘min Regina’ ? I need to search for em old photos that we took together wayyyyy back and throw them back one day ? Such a gorgeous yound girl! May God continue to bless you, protect you, and guide you to become the best woman that He wanted you to be! Much ? from aunt Alpha.
Kutoka Facebook
Nimependa sana hii picha ya Mr and Mrs James Chanda. Wamependeza sana.
BTW, James ni kaka ambaye tumefahamiana kwa miaka mingi sana. Tulikutana mara ya kwanza Buttler Community College, Andover, Kansas. Nikiwa nasubiria ride from my cousin brother China Igogo naye alikuwa anasubiri kuona adviser basi katika kuongea ndiyo tukajuana wote wa Tanzania na pia wanafahamiana sana na kaka yangu. Basi akampigia na kumwambia asije kunifuata yeye atanirudisha kwani ilikuwa inachukua kama saa moja hivi kutoka Wichita mpaka hapo college. Natoka hapo tukawa marafiki akawa siku ambazo anaenda shule huwa ananipitia na mimi kwa wakati huo nilikuwa sijajifunza kuendesha gari na ilikuwa msimu wa snow. James Asante sana. Uzidi kubarikiwa sana wewe na familia yako yote.
Father’s Day wishes
Leo ni siku ya kinababa huko Australia. Hivyo napenda kuwatakia wale wote wanao ishi maeneo ya huko (wababa na wababa watarajiwa) kheri ya siku ya kina baba haswa kwa mume wa rafiki yangu Aidan Nyongo. Mungu awabariki sana.“Happy Father’s Day to my amazing husband” hayo ni maneno ya mke mwema Fina Nyongo………….mbarikiwe sana wapendwa!
#FBF
Nini faida za hirizi wanazo fungwa watoto?
Jamani kama kuna mtu anajua naomba kuelimishwa kuhusu hizi hirizi ambazo wanafungiwa watoto. Nimesha ona wengine wanafungiwa shingoni kama cheni na kunawanao valishwa mkononi kama Princess Lattifa (mtoto wa Diamond na Zari). Naamini hizi huwa zinatoka kwa waganga wa kienyeji wale wanao roga watu (siyo wanao uza madawa ya kienyeji). Kama nitakuwa nimekosea basi nielimishe tafadhari. Sasa naomba kuliaza inamaana mtoto huwa anapelekwa kwa waganga na kufungiwa au zinauzwa tuu mahala fulani na watu wanaweza kununua? Na nini haswa faida zake katika ukuwaji wa mtoto.
Naomba uwelewe kuwa na heshima sana imani za watu na uhuru wa kuabudu kitu wanacho kiamini. Hivyo nataka kuelimishwa tuu na siyo kumkashifu mtu. Asante.
Hongera sana Mariam Kimesera
Hongera sanaaaaaa Mariam Kimesera kwa nafasi uliyopata toka Georgia Music Awards. Mungu akubariki na huu uwe mwanzo tuu wa mambo mengi mazuri na makubwa zaidi ya hapa. Mariam alichagulia kuwa mmoja ya watu waliokuwa waki-present zawadi za washindi katika sherehe au tukio la GA Music Awards iliyofanyika tarehe 21 / 08 / 2015 katika jiji la Atlanta, Georgia, USA. Mariam alipata nafasi ya kuwakilisha / kukabidhi zawadi kwa watu watatu tofauti. Mariam ni mtoto wa tatu wa mwanamitindo aliyetukuka Missy LB (Linda Beuzenhount). Hapa akiwa na mama yake pamoja na International model Renee Norris tayari kwa kuingia kwa red carpet. Wote watatu walikuwa wamevaa nguo zilizo shonwa na LB……Hongera sana Mariam.
Hot shot of the day
Huduma ya haraka kwa upungufu wa sukari mwilini
Ubongo wa binadamu unahitaji sukari ( glucose) kwa mda wote kama gari inavyohitaji mafuta.Sukari hiyo itokanayo na vyakula aina ya wanga, huingia katika mzunguko wa damu na kuzipatia chembechembe za ubongo sukari ya kuendeleza utendaji. Hivyo ni vyema kusema ubongo hauna uwezo wa kuzalisha au kuhifadhi sukari ya kutosha matumizi ya baadaye.
Kutokana na hitilafu ya kingosho (dysfunctional pancreas) wagowja wa kisukari huwa na hali ngumu ya kuthibiti sukari katika kipimo kinachohitajika na hivyo hujikuta sukari kuwa juu kupita kiasi (Hyperglycemia) au chini kupita kiasi(Hypoglycemia). Japo hali zote huhitaji huduma, leo tutazungumzia Hypoglycemiaambayo huhitaji huduma ya haraka ili kuokoa maisha. Soma zaidi hapa
Birthday wishes
Kheri ya siku ya kuzaliwa kaka yangu kipenzi Noah Manongi! Niseme nini mimi Alpha?! Baba wa Mbinguni anajua yote yaliyopo ndani wa moyo wangu jinsi ninavyo kushukushuru kwa uwepo wako katika maisha yangu huku nilipo mbali na familia yangu! Umekuwa Nami kaka yangu katika tabu na raha, umekuwa nami hata pale ambapo mimi mwenyewe nilikuwa sina imani nawe. Umesimama nami bila kutetereka hata pale baadhi ya marafiki zako walipo geuka na kunijengea chuki ambazo hazielezeki! Kaka yangu wewe hukuniacha kwani wanijua mimi jinsi nilivyo na hukuogopa wala kuona haya kusimamia ukweli! Niseme nini kaka yangu? Kwakweli sina cha kusema zaidi ya Asante! Katika siku hii ya leo, siku ya kuzaliwa kwako kaka yangu, namwomba Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa rehema azidi kukulinda, siyo akubariki bali azidi kukubariki kwani wewe teyari ulisha barikiwa! Mungu akupe afya bora, amani, furaha, na upendo ndani yako na ndani ya familia yako. Hekima yako na upendo wako vikapate kuongezeka maradufu! Ukaguse na kubariki maisha ya watu wengine kama ulivyo fanya kwangu mimi. Happy birthday my brother. Love you deep!
Hot shot of the day
#TBS
Hotuba ya Mwalimu Nyerere kuhusu vyama vingi
Embu msikilize marehemu Mwl. Nyerere halafu wewe mwenyewe utafakari na kutafsiri ulivyo elewa!
“Double Life”
Watu ambao wamesomea na wanafanya kazi za upelelezi wa hali ya juu ndio tumezoea kusikia au kuwaona wakiishi maisha ya siri ambayo hayatoi huwasilia wa yeye ni nani. Hii nikutoka na sababu za kiusala wa maisha yao pamoja na kupata ukweli halisi wa jambo wengi inabidi wa-prented maisha yao. Kwamfano; mtu anaweza akaishi maisha ya chini sana (low profile) siyo kwamba hana uwezo ila nikwasababu hatakiwi kuwapa watu matamanio ya kumjua na kuanza kumfuatilia; hivyo hawa tunasema wanaishi “double life.” Lakini vile vile kuna watu ambao wanaishi “double life” siyo kwasababu ya kazi wanazo zifanya bali wanakuwa na maisha fulani ambayo si mazuri labda kwa familia yake, marafiki, ndugu, wafanyakazi, na jamii inayomzunguka. Maisha ya “double life” siyo tatizo la njisia moja tu, la hasha! Ni tatizo kubwa ambalo lipo kote kwa wanaume na wanawake hambao huficha siri za ajabu kutoka kwa wake walio karibu nao. Katika kundi hili tunaweza kuligawa katika sehemu kuu tatu:- Continue reading “Double Life”
Kutoka Facebook
Nimependa sana hii picha ya Tabu Obago. Huyu ni binamu yangu binti wa marehemu shangazi yangu. Navivile tuliishi wote ndani ya himaya ya mzee Igogo. Nampenda sanaaaaaa!
Usije ukakosea ukanichokoza nitakusemea kwake atakukuchambuaje sasaa? ?? Yani atakunyambua kama mchicha vile utajuta kwanini ulinichokoza?? halafu yeye anachanganya Kiswahili, Kijaluo, na English mtamkoma ???
Jana tulikuwa tuna text akaniambia kuna “house gal mmoja kwenye Facebook ananiudhii” (Akimaanisha Joyce Kiria) yani hii sentence hadi leo bado nacheka ??? Mambo ya team Magufuli na team Lowassa hayo
Mother and Son moment
Manhood
(audio): “Muumbaji wa ndoa ni Mungu peke yake…..Hakuna mwalimu wa ndoa hapa duniani” – Tumaini Kilangwa
Tumaini Kilangwa au da Tuma, yeye ni mama wa watoto wawili, mke, na mfanyabiashara. Katika mahojiano haya ambayo yote amerekodi na unaweza sikiliza ameongelea mambo mabali mbali kuanzia alipotokea, maisha yake ya elimu, maisha kama mama, maisha kama mke, na maisha kama mfanyabiashara. Ni mahojiano mazuri sana ambayo yanafundisha na kutia moyo kuwa hakuna lisilo wezekana kwa Mungu (kama unaamini kuna Mungu). Tafadhali chukua muda wako umsikilize wala hutojutia kamwe!Elimu na kazi alizofanya
Dada Tuma kwa sasa ameamua kuachana na kazi za kuajiri hivyo yeye ni mfanya biashara anaye miliki mgahawa ujulikanao kama Eastern Cuisine. Uliopo Wichita Kansas.
Pichani ☝ ni watoto wa da Tuma wakiwa wamevalia Tshirt za mgahawa huo….
Katika swala la uzazi na malezi ya watoto wake mpaka hapa walipofika japo safari bado inaendelea Tumaini anashuhudia kwa kusema “tumeuona mkono wa Mungu na tunaendelea kuuona ukuu wake siku hadi siku.” Ni ushuhuda wa kusisimua na unatoa faraja kwa wale ambao wanapitia changamoto kama hizi katika malezi au jambo lolote lile. Embu msikilize wewe wenyewe…….
Kuna changamoto nyingi katika malezi haswa ukizingatia tupo katika inchi ya ugenini ambapo mila na desturi zetu nitofauti na tulizo lelewa ameeleza da Tuma……
Dada Tuma ametoa ushauri au ujumbe kwa Watanzania wote waishio nje ya Tanzania na hata wale waliopo nyumbani kwamba wawe na moyo wa kupenda kujaribu vitu na wasikate tamaa, kuwa na plan na mipango kwenye maisha. Utambuwe karama yako ili uweze kuweka mipango yako vizuri. Pia ameshauri watu kumtegemea Mungu sana kwani Mungu wetu ni Mungu wa upendo na anasikia sala za watu wote!
Maisha ya ndoa yanahitaji uvumilivu na maombi ya kila siku. Da Tuma amewasihi wanandoa haswa wadada kuacha tabia ya kuiga iga mambo ambayo wanayaona au kusikia kutoka kwa watu wengine hususani kwenye “kitchen parties” kwani kitu ambacho kimewezekana kwenye ndoa ya mwenzako siyo lazima kifae kwenye ndoa yako! Hakuna Mwalimu wa ndoa hapa duniani ni Mungu peke yake……!
Napenda kutoa shukran zangu za dhati kabisa kwa dada Tumaini, pamoja na kubanwa sana na kazi na misha ya familia lakini kwa upendo kabisa ameweza kuchukua muda wake wa pekee na kukubali kufanya mahojiano haya na mimi. Ubarikiwe sana da Tuma.
Pia shukran kwa wote ambao wamejitolea kwa njia ya pekee kabisa kuweza kushare picha zao, mawazo yao, na pia ku-share maisha yao kwa njia ya mahojiano na hii blog. Wote naomba Mwenyezi Mungu awabariki sana kwani mimi binafsi sina cha kuwalipa!
N.B: Kama unataka ku-share nasi kitu chochote au unaswali wasiliana nami kwa [email protected] Pia naomba nikumbushie kuwa huitaji kuweka email wala jina lako unapotaka ku-comment japo fomu ya comment inaonyesha hivyo lakini si lazima. Asanteni wote!
Mahojiano haya yameandaliwa na Alpha Igogo