*Kesha la Asubuhi* *Alhamisi, Tarehe 19/4/2018* *Kuongozwa kwa Njia ya Ushuhuda Ulioandikwa* ▶Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi. Isaya 8:20. ▶Daima Roho Mtakatifu anaongoza kwenye Neno lililoandikwa na huwa anavuta usikivu katika suala la kiwango kikuu cha maadili cha uadilifu. Kuheshimiwa na Mungu kwa namna hiyo kwa kupata fursa hii ya pekee kushuhudia ukweli ni jambo la ajabu. Kristo aliwaambia wanafunzi wake mara kabla ya kupaa juu na wingu la malaika kumpokea na kumwondoa machoni pao, “Mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi” (Matendo 1:8). Walifanywa wafae kumshuhudia Kristo kutokana na karama ya kimbingu ya Roho Mtakatifu. ▶Natamani kuwasisitizia ukweli kwamba wale ambao Yesu anakaa mioyoni mwao kwa imani kwa kweli wamempokea Roho Mtakatifu. Kila mtu anayempokea Yesu kama Mwokozi wake binafsi kwa uhakika pia anampokea Roho Mtakatifu kuwa Mshauri, Mtakasaji, Kiongozi na Shahidi wake. Kadiri muumini anavyotembea kwa karibu na Mungu, ndivyo ushuhuda wake unavyozidi kuwa wazi na kama matokeo yaliyo ya hakika, ndivyo mvuto wa ushuhuda wake utakavyokuwa wenye nguvu zaidi kwa wengine kuhusu upendo wa Mwokozi; ndivyo atakavyozidi kuonesha uthibitisho kwamba anathamini Neno la Mungu. Hiki ndicho chakula chake, ndicho kinywaji chake, kwa ajili ya kuridhisha nafsi iliyo na kiu. Anathamini fursa hii ya pekee ya kujifunza mapenzi ya Mungu kutoka katika Neno lake. ?Baadhi ya watu wanaodai kuwa waumini wameweka pembeni, wamegeukia mbali na Neno la Mungu. Wameipuuzia Biblia, Mwongozo ulio wa ajabu, kipimo cha kweli cha mawazo yote na wanadai kwamba wanaye Roho anayewafundisha, kwamba hili linafanya suala la kuchunguza Maandiko lisiwe la muhimu. Wote wa namna hii wanasikiliza hila za Shetani, kwani Roho na Neno wanakubaliana. Maandiko yanasema, “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” Yeye ambaye ukweli unamweka huru ndiye mtu ambaye yuko huru kweli. – Manuscript Releases, vol. 14, uk. 70, 71.
Joyce Kiria: Kila mtu ana njia yake …. Kila mtu kapewa msuli wa kupambana na matatizo yake
Regrann from @joycekiriasuperwoman - MAISHA YANGU BINAFSI NILIYAKUTA YAMEJAA CHANGAMOTO NYINGI, ELIMU SINA, FAMILIA YETU NI MASKNI, MIE NDO MTOTO WA KWANZA, YAANI MAISHA HAYANA HAMASA, HAYANA MATUMAINI, NOW NIKACHAGUA KUYAGEUZA NDO FURSA, YAANI NDO MTAJI WANGU... WEWE UNAONA NI MATATIZO MIMI NINAYAONA NI MGODI... NILIAMUA KUPAMBANA NA HAYA MATATIZO YANGU KWA STAILI HII YASINIUMIZE KICHWA, BALI YANAPOKUJA TUU NINAYATAZAMA KWA JICHO LA FURSA! NAYAKUMBATIA NAYAONGEA KWA NGUVU ZANGU ZOTEEEE, NAPATA NAFUU LAKINI PIA NAPATA KAZI HAHAHAHA. UJASIRI HUU NILIOJIPA NDIO UNAONIFANYA KUWA SUPER WOMAN, NANI ATAWEZA KUPITA HII NJIA?? UNADHANI WATU HAWANA MATATIZO? KWANINI WENGI WANAYAOGOPA?? KUKUBALI UKWELI WAKO BINAFSI SIYO JAMBO JEPESI, WENGI TUNAPENDA SANA KUJIONYESHA KWAMBA TUU WATAKATIFU... MIMI NASIMULIA MAISHA YANGU BINAFSI, SIYASIMULII YA MTU, NASIMULIA NJIA ZANGU ZENYE LADHA YA ASALI NA MWAROBAINI KWA PAMOJA KWA AJILI YA KUJIFUNZA NA KUFUNDISHA WENGINE.... THAT IS MY PATH ... NJIA ZETU HAZIFANANI ... KILA MTU ANA NJIA YAKE ... KILA MTU KAPEWA MSULI WA KUPAMBANA NA MATATIZO YAKE... PIGANA NA YAKO.... AM SUPER PROUD TO BE ME... I AM A SUPER WOMAN #SUPERWOMAN - #regrann
Dina Marious: Angalia ndoto yako
Regrann from @dinamarious - Usiangalie magumu yanayokukabili na changamoto unazokutana nazo Leo angalia NDOTO yako. Ndoto yako itatimia....... ndoto yako inawezekana.Kumbuka jinsi ulivyoiamini endelea kuiamini. Inawezekana Leo umeamka una stress,huna hela,huelewi mambo yanavyokwenda. Pamoja na yote endelea kuiamini NDOTO yako hata katika mazingira yanayokatisha tamaa. Kumbuka wewe ndio una hiyo picha ya Kesho yako naamini ni picha nzuri sanaa na amini utaifikia. Good morning! - #regrann
Kesha la asubuhi: KUTAKASWA KWA NJIA YA NENO
KESHA LA ASUBUHI JUMATANO 18 Apr 2018 *_KUTAKASWA kWA NJIA YA NENO_* ? *Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. Yohana 17:17.* ✍?Mzigo wa ombi la Yesu ulikuwa kwamba wale waliomwamini Yeye waweze kulindwa dhidi ya uovu wa dunia na kutakaswa kwa njia ya ile kweli. Yeye huwa hatuachi katika hali ya kubuni kusiko na uhakika kama ukweli ni nini, bali huongezea, “Neno lako ndiyo kweli.” ✍? Neno la Mungu ni njia ambayo kwayo utakaso wetu ni lazima ukamilishwe. Kwa hiyo, ni jambo la muhimu sana, kwamba tujifahamishe maelekezo matakatifu ya Biblia. Ni jambo la muhimu kwetu kuelewa maneno ya uzima kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa awali kufahamishwa kuhusu mpango wa wokovu. ✍?Hatutakuwa na udhuru ikiwa, kutokana na uzembe wetu wenyewe, hatutajua madai ya Neno la Mungu. Mungu ametupatia Neno lake, udhihirisho wa mapenzi yake naye amewaahidi Roho Mtakatifu wale wanaomwomba, ili awaongoze kwenye kweli yote; na kila nafsi ambayo kwa uaminifu inatamani kufanya mapenzi ya Mungu itayajua mafundisho. ✍?Dunia imejazwa na mafundisho ya uongo; na tusipochunguza Maandiko kwa ajili yetu wenyewe kwa makusudi, tutakubali makosa yake kana kwamba ndio ukweli, tutakubali mila zake na kudanganya mioyo yetu wenyewe. ✍? Mafundisho na desturi za dunia vinatofautiana na ukweli wa Mungu. Wale wanaokusudia kugeuka kutoka katika kuitumikia dunia ili wamtumikie Mungu watahitaji msaada wa kimbingu. Itawapasa kukaza nyuso zao kama chuma kuelekea Sayuni. Watahisi upinzani wa dunia, mwili na mwovu, nao itawapasa waende kinyume cha roho na mivuto ya dunia. ✍?Tangu nyakati Mwana wa Mungu alipokabiliana na chuki zisizo na sababu na majivuno na hali ya kutokuamini ya watu, hakujawa na badiliko katika mtazamo wa dunia kwa dini ya Yesu. Watumishi wa Kristo ni lazima wakutane na roho ile ile ya upinzani na shutuma na ni lazima kwenda “nje ya kambi, tukichukua shutumu lake” (Waebrania 13:13). ??♂```Utume wa Yesu ulidhihirishwa kwa miujiza ambayo haikuwa na mashaka. Mafundisho yake yaliwashangaza watu. Mafundisho yake hayakuwa lugha za kitaalamu zilizokinzana za waandishi, zilizokuwa zimejawa na imani za mafumbo, ambazo zilikuwa na mizigo ya mifumo ya kipuuzi na ulazimishaji usio na maana; ??♂ lakini ni mfumo wa ile kweli ambao ndio uliokutana na mahitaji ya moyo. Mafundisho yake yalikuwa wazi, bayana na yenye upana. Ukweli halisi aliousema ulikuwa na uwezo wa kusadikisha, nao ulivutia usikivu wa watu. – Review and Herald, Feb. 7, 1888.``` *MUNGU AWABARIKI NYOTE MNAPOTAFAKARI NENO LAKE.*
Family feud continues: The Kimambi
Naona mdogo wake Mange Kimambi ameamuwa kuweka roho yake huru kwa kuweka wazi kuwa anamsapoti RC Makonda na serikali ya awamu ya tano. Wiki iliyopita aliweka picha akiwa na RC Makonda ikiambatana na short caption "nikiwa na RC wangu" lakini leo naona kawa muwazi zaidi.... .... Well, this is not so good and very sad on Kimambi side But it's good kwa wanaopenda drama na wengine tunajifunza hapa jinsi ya kuhandle family issues especially when it played out on public....... Tutaendelea kuwafatilia mpaka mwisho. Regrann from @lord_supremo1 - Tanzania ni yetu na Amani ndio msingi wa umoja wetu!! Nimeamua kua mzalendo!! Nikiwa na RC wangu @paulmakonda ? - #regrann
Kesha la asubuhi: Kufurahi katika neno
*Kesha la asubuhi* _Jumanne Aprili 17, 2018_ *_Kufurahi Katika neno_* _Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu; maana nimeitwa kwa jina lako, Ee Bwana, Mungu wa majeshi. Yeremia 15:16._ ? Katika kutekeleza dini ya Biblia, kuna hitaji la subira, uungwana, kujikana nafsi na kujinyima. Lakini, kama Neno la Mungu litafanywa kuwa kanuni inayodumu maishani mwetu, kila linachotwambia inatupasa kufanya, kila neno, kila tendo lililo dogo, litadhihirisha kuwa sisi ni raia wa Yesu Kristo, kwamba hata mawazo yetu yamewekwa kwenye kifungo chake. Neno la Mungu likipokelewa moyoni, litaondoa nafsini hali ya kujitosheleza nafsi na kuitegemea nafsi. ? Maisha yetu yatakuwa nguvu kwa ajili ya kutenda mema, kwa sababu Roho Mtakatifu atajaza mioyo yetu kwa mambo ya Mungu. Dini ya Kristo itatekelezwa nasi; kwani nia zetu zipo katika upatanifu kamili na mapenzi ya Mungu. Baadhi ya wale wanaodai kuwa na dini ya kweli inasikitisha kwamba huwa wanapuuzia Kitabu kilicho Mwongozo utokao kwa Mungu ili kuelekeza kwenye njia ya mbinguni. Wanaweza kusoma Biblia, lakini kusoma tu Neno la Mungu, kama mtu asomaye maneno yaliyoandikwa kwa kalamu ya mwanadamu, kutampa mtu ujuzi wa juu juu tu. ? Kuuzungumza ukweli hakutatakasa wapokeaji. Wanaweza kudai kufanya kazi ya Mungu, wakati ambapo, kama Kristo angekuwa kati yao, sauti yake ingesikika, akisema, “Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu” (Mathayo 22:29). Watu wa namna hiyo hawataweza kujua kile dini ya kweli inachokimaanisha. ? Kristo alisema, “Maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima” (Yohana 6:63). Yeremia anashuhudia juu ya Neno la Mungu akisema, “Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu.” Kuna uponyaji wa kimbingu katika Neno la Mungu, ambao wale waitwao wenye hekima na busara hawawezi kuupata, lakini ambao unadhihirishwa kwa watoto. ? “Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga” (Zaburi 119:130). Kama Neno hili litahifadhiwa moyoni, litakuwa ni hazina ya moyo, ambako vitatoka ndani yake vitu vipya na vya kale. Hatutaendelea kufurahia kufikiria mambo duni ya dunia, bali tutasema, “Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu” (aya ya 105). – Review and Herald, Mei 4, Mei 4, 1897. _TAFAKARI NJEMA MWANA WA MUNGU_
Kuna watu ambao wapo hatarini kufutiwa uraia wa Tanzania!
Hii ni kwa wana Diaspora wenzangu tu wengine someni halafu mpite kimya! Kabla hamjaweka miguu yenu barabarani kwenda huko mnako kwenda naomba kwanza uhakiki uraia wako. Je, wewe bado ni Mtanzania au ulisha ukana uraia wako? Kumbuka Tanzania haina Dual citizenship! Na kama bado wewe ni raia wa Tanzania je, umeshaagana na ndugu zako kwamba hata kama hamta onana tena basi iwe hivyo na kuwa ni salama rohoni mwako?! Maana unaweza usiwaone tena, siyo kwasababu ya kifo hapana, kwasababu huwezi kukanyaga ardhi ya Tanzania!Kwanini nimesema haya niliyo yasema, ni kwasababu ninaona dalili za baadhi ya watu kuja kufutiwa haki yao ya kuzaliwa kama Mtanzania (uraia wao kufutwa kabisa) na wengine ambao walisha ukana Utanzania wanaweza kuwekewa "Red flag" na wasiruhusiwe kukanyaga Tanzania for a very long time! Sounds like a joke, huh! Wrong! This is not a joke so kindly take it very seriously!! Kumbuka ofisi ya Rais ni tasisi inayo jitegemea ambayo inauwezo na mamlaka ya kufanya hivyo pale watakapokuwa na sababu tosha kufanya hivyo! Vile vile kumbuka kuwa Rais ndio mtu peke anaweka signature kwenye Hati Miliki ya viwanja na pia anauwezo wa kuifuta na kuweka majina ya wamiliki wapya, hivyo kua muangalifu na maamuzi yako. Ukitaka kupambana na serikali lazima uwe umejipanga uwe na plan A to Z! Siyo plan A, B, sijui na C hapana! Uwe na plan zooote intact!! Nimewatolea siri tusije laumiana huko mbele ? Otherwise, nawatakieni matembezi mema kwa wale mtakao kwenda matembezi ? #NotWorthIt
Hujafa hujaumbika: Mariah Carey amegundulika na Bipolar disorder
https://youtu.be/j–hhDDo11w
Wahenga walisema hujafa hujaumbika hawakukosea bali walitaka watu wajifunze kuishi kwa unyenyekevu bila kudharau wengine kwani kama bado hatujakuchimbia kaburi lako tegemea kupatwa na kitu chochote kila kibaya au kizuri! Just be humble! Kuna watu wengi ukiwaona utadhani wapo vyema kabisa kiafya na kiroho, kumbe ni wagonjwa kama siyo kiroho, basi kimwili, au kiakili! Tena humu kwenye social media ndio nirahisi sana kuwagundua ?? Wewe angalia sana watu wanaofanya vitu extreme just to get attention fanya kuwachunguza utagundua kuna shida mahala! Siyo tu wanao post matusi au picha za uchi, hapana! Hata wale ambao kutwa picha zao lazima ziwe na muonekano fulani "perfectly put together" the "divaish" behavior. Au mwingine kazi yake ni kupiga picha na viongozi wa siasa na "celebrates" tu haonyeshi maisha yake halisi zaidi ya hizo picha yani watu kama hawa wengi ni wagonjwa! Wengine ni waongo spare zake hakuna!! Lakini hakuna haja ya kumcheka mgonjwa japo saa nyingine katika hali ya kiubinadamu wengi tumejikuta tukifanya hivyo haswa kwa wale ambao wameumiza roho zetu! Kumbuka 'hujafa hujaumbika'! Wewe ona mtu kama Mariah Carey uzuri na pesa zote alizo nazo bado amekutwa na huu ugonjwa! Bipolar siyo Ukichaa ila usipo tibiwa kwa muda mrefu unageuka kuwa kichaa kabisa. Mariah Carey aligundulika kuwa na huu ugonjwa mwaka 2011, ameficha kwa muda huo wote lakini sasa imefikia hali ambayo haufichiki tena. Kwa kuhofia kuwa ipo siku mtu angetoa hivyo siri kabla yeye hajasema imembidi sasa aende hadharani na kutangazia dunia kuwa yeye ni mgonjwa wa akili, hivyo dunia impokee na kumkubali jinsi alivyo!.....Kabla ya kuhukumu mtu jaribu kumjua kwa kiundani unaweza tena dhambi mbaya sana! #HujafaHujaumbika
LeMutuz: Mambo bado kabisa mpaka mtakapoelewa kuwa SERIKALI YA AWAMU YA TANO ni serious business
Regrann from @lemutuz_superbrand - FACT: Is walipokutana jana yaani ... Le Commandant Field Marshall RC @paulmakonda na KAKA YAKE NANILIHIU LE KIGAGULAZZZ Mama Maandamano Hewa waliongea kwa masaa 4 nonstop wakiwa wamejifungia ofisini kwa Le Commandant WAWILI TU! ....ni FACT ....swali la msingi hapa ni je WALIONGEA NINI MUDA WOTE HUO WA DAKIKA 240? ...Kwani Kaka anajua nini kuhusu Dada yake Mama maandamano Hewa? ....Kwanini Le Commandant hakukutana na ndugu wengine wa Mama Maandamano Hewa akakutana na huyu tu? ...Le Commandant na Kaka wameanza lini kufahamiana na je walikuwa na Mawasiliano siku zote au? ...au Kaka ametumwa na Dada? ...kwa nini Dada kalia sana kwa uchungu? ...Le Commandant alijuaje kukutana na Kaka italeta kilio cha damu kutoka kwa Dada kama ilivyotokea? ....I mean haya ni maswali muhimu sana ya kujiuliza na kujijibu kabla hujakurupuka na kuanza kuropoka ropoka kwa nyie Misukule ...mwenyewe Dada Mama Maandamano Hewa kakubali kuwa kaumia wewe Msukule unasema nini? ...tulieni mambo ndio kwanza yameanza mpaka Dada afikishwe kwenye mikono ya Sheria ya Tanzania na ni karibuni sana hana muda mrefu ....Rais wa zamani wa USA Reagan aliwahi kusema "YOU CAN RUN, BUT YOU CAN'T HIDE FOR GOOD" - HIROSHIMA"........INAITWA KUPATWA KWA JUA nyie Misukule na Minyumbu tulieni hii ni "OPERATION KIGAGULAZZZ ONE" ...habari kamili inakuja ...toeni mapovu, lien, rukeni hii hamchomoi mazafantazz...KIGAGULAZZZ kashikwa pabaya na bado subirini the next "OPERATION KIGAGULA TWO" ...ndio maana ya ...LE COMANDANT FIELD MARSHALL now U know ...mambo bado kabisa mpaka mtakapoelewa kuwa SERIKALI YA AWAMU YA TANO ni serious business kazi kazi na Bampa to Bampa ....wewe Kibibi Kigagulazzz hiyo ni rasha rasha tu HABARI KAMILI BADO INAKUJA ....mpaka utinge Mahakamani Kisutu kujibu mashitaka yako rasmi ya UHAINI....hahahaha....ok guys here is THE KING OF ALL BONGO SOCIAL MEDIA NETWORK & THE KING OF ALL MOTHERS OF FREEDOM OF SPEECH! ....nani anabisha hukooo? au nani mwenye tatizo hukooo?...KANYAGA! and THIS CASE IS CLOSED! - @lemutuz_superbrand - #regrann
Family feud: The Kimambi
Regrann from @mangekimambi_ - letter to my brother Anil..... Since baba amefariki in 2004 I have tried to be the best big sister I can be.Siku zote nimewaweka nyinyi mbele yangu mimi. Nimejaribu kufikiria kama you thought everything through kabla ya kwenda kwa Bashite. Remember hiyo mansion(nyumba) mnayoishi 25% ni yangu.Kumbuka hoteli inayowapa kula 25% ni yangu. Na sio yangu kwa maneno ila kwa judgement ya mahakama kuu. Judgement imetoka since 2006 na mpaka leo sijawasumbua muuze chochote mnipe changu. Since 2004 baba alivyofariki sijawahi kudai wala kupokea hata shingi 10 ya mapato ya hotelini sababu niliwaza nyinyi mnahitaji hizo pesa more than me.Nilitaka msim-miss sana baba sababu aliwaacha nyinyi wadogo sana. Nikaona nibusara niwaachie na share yangu ya hotel. For 14 years hamjawahi kunipa hata sumni. That’s how much I love you. Nahangaika kivyangu marekani ila hata siku moja sijawahi kuwaambia muanze kunipa asilimia 25 yangu ya mapato ya hoteli. Leo hii nikisema niwadai share yangu ya mapato ya hotel since 2004 mtakuwa na hali gani?? Au nikisema uzeni nyumba mnilipe changu mtaenda kuishi wapi? Na mmezoea kuishi kwenye mansion? Mnadhani sihitaji hizo pesa zangu ? Nazihitaji ili na mimi ninunue japo apartment hapa marekani ila sitaki kuharibu undugu sababu ya mali. Ila wewe umekubali undugu wetu kuharibu? 3 months ago mmeuza lile eneo la machimbo ya kokoto pale Tegeta kwa milioni 400 hamjanipa hata senti, hata kuniambia kama mmeuza hamjaniambia.Nafanya kuhadisiwa na mliowauzia. Mmegawana wenyewe wawili na mama enu. I’m sure mtapata shock kuwa najua hili. Na hata kuwauliza sijawauliza sababu nalinda undugu. Na nnalinda undugu sababu hakuna kitu baba alikuwa ananisihi kukifanya kama kuhakikisha hatufarakani. Kila siku aliniambia wewe ndio mkubwa, wewe ukiwapenda wadogo zako hamtokaa kutengana. Wewe ndio wakuwaunganisha. Niliwaachia mali ili kumuenzi baba yetu.Nikaona bora nyinyi muishi like kings mimi niishi kawaida. Mpaka hati zangu za shamba langu la Mbweni nilikubali mkazichue kwa lawyer wangu although jaji alinikabidhi mwenyewe. Kama isingekuwa Mama Tenga kukataa kuwapata bila mimi kuwepo leo mngekuwa nazo. that’s how much I don’t care abou mali but undugu. Nilikuwa tayari niishi vibaya ila nyinyi muishi vizuri ndio maana sikuwasumbua na mali za baba yetu. Nna uwezo wa kurudi mahakamani na kumwambia jaji yule yule alieamua kesi yetu ya mirathi in 2006 kuwa miezi mitatu iliyopita mmeuza machimbo ya kokoto ya Tegeta kwa milioni 400 bila kunitaarifu na mkagawana nyinyi wawili na mama yenu bila kunipa milioni 100 yangu au hata senti moja na hatua kali zikachukuliwa kwa kunitapeli, labda your new friend Bashite atakusaidia huko mahakamani ?? You have a big connection now ?? Share yangu ya machimbo ya kokoto mliouza muanze kunitafutia. Mlidhani sijui? Kweli mnadhani naweza kupewa habari nyeti za serikalini ila nisipewe habari za nyinyi kuuza machimbo yetu ya kokoto? Nilikuwa najua Ila niliamuwa kukaa kimya sababu nawapenda na bila nyinyi kwenye maisha yangu nahisigi siwezi kuishi ila labda nahitaji kujifunza kuishi bila nyinyi. Niliona kama ningewauliza kuhusu hayo machimbo tungegombana nikaona bora nisamehe hizo milioni 100 kuliko kupoteza ndugu zangu ila nyinyi hamnithamini ?. Mapenzi yangu kwenu yanafanya mnaniona zoba. I have tried my best to keep our family together. Na hayo machimbo mmeuza wa bei ya njaa sana, eti milioni 400 wakati yana thamani ya karibia 1 billion.Si mngesubiri mpaka uchumi u-pickup ndio tuuze? Anil, I just wanted to remind you of how easily I can fuck you guys over but I havent.Ila wewe leo you decided to fuck me over. Ukoo mzima unanishangaa how come sijachukua changu hadi leo, miaka 12 toka jaji ametugawanyishe in 2006. Ndugu wengi wanadhani mmeniloga nisichukue hata mauzo ya hotelini. Naamini hamjaniloga ila ni mapenzi yangu kwenu tu. Sorry guys, ilibidi nitoe hili kifuani ili niweze kuendelea na mambo mengine. Nisingemwambia ingeniuma zaidi. Haki leo Bashite kaniumiza.Yani leo Bashite kaniweza.But the struggle continues ?. I promise not to address this issue again. Kwahili mniombee maana limeniumiza haswa, worse than pain ya ndoa yangu kuvunjika.Na nimeumia kwasababu moja tu, my dad must be very disappointed huko aliko. I have failed him. Finally tumefarakana ?? **PS: Mnaoniambia nifute hizi posti nambloku. Mnataka nife na maumivu? I feel a little better now. - #regrann
Yes! Zari goes to church!
Regrann from @zarithebosslady – All my days are for God, but Sunday I go all out…. #Church – #regrann
Hayo ni maneno yake Zari Hassan the Bosslady kupitia Instagram page yake. I am happy for you Zari keep that spirit God is everything! I hope one day you will warship on Sabbath with me here in Houston or you want me to come to South Africa? I can ??…. Bwt, you look Amazing! ? Be blessed mama Tee ?❤
Mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu mchungu……. !
Kuna watu wanajifanyaga kuwa wao wanajua jinsi ya kufanya maamuzi mazuri kuliko wenzao, wako wepesi sana kusema matatizo ya watu na kuhukumu wengine kwa maamuzi wanayo fanya! Sasa ikatokea maamuzi uliyofanya hayakuzaa matunda mazuri mbona utakoma! Lakini ikiwa yeye ndio kafanya maamuzi ambayo siyo sahihi atatafuta kila njia ya Ku justify hayo makosa na kutumia gharama zote kuficha makosa yao. Sasa huyu Tamar Braxton ni mmoja ya watu wenye tabia kama hizo. Yani huyu alikuwa mwepesi sana kusema dada zake kuwa wamechagua wanaume wasiofaa na ndio maana ndoa zao zina matatizo. Msikilize hapa ?
Kuna siku pia alimuita Ex husband wa dada yake kuwa ni "baby sitter" kwamba hana faida yoyote kwa dada yake wala watoto zaidi ya kuwa kama mfanyakazi wa kulea watoto. Dada yake alichukia sana na kuwambia kuwa Andre anaweza asiwe mume mzuri lakini ni baba mwema sana kwa watoto wao na hato weza kumvumilia kuona anamdhalilisha baba wa watoto wake. Tizama hao ?
Sasa leo hii yamemkuta matatizo kwenye ndoa yake mpaka anadai talaka sasa amekuwa MBOGO! Hataki hata kuongea na familia yake kuwaelezea ukweli kuwa ndoa yake naye ilikuwa ni mbovu tu kama yao ila alikuwa anaficha. Yamemkuta yale yale aliyokuwa akiwaambia dada zake, kwa aibu anashindwa hata kuwaambia dada zake kuwa amekwenda mahakamani kudai talaka. Dada zake wamejua kuwa mdogo wao amekwenda mahakamani kudai talaka baada ya kusoma kwenye mitandao. Halafu dada zake wanapotaka kumuuliza ili wajue ukweli anakuwa mkali kama pili pili! Majibu ya shortcut huku akitumia Mic kama "defensive" mechanism! Embu mtazame hapo ?
Unajua kama hayajakufika kama hujui ku sympathize na matatizo ya watu basi ni bora ujifunze kunyamaza kuliko kuhukumu wenzio unafanya wajione like something is wrong with them! Wakati jambo kama hilo au tatizo lolote lile linapokukuta unakuwa mkali hutaki kuulizwa wala husikii kitu!
Nasikia Tamar amekuwa very sensitive na ame withdrawal kutoka kwa familia yake. Yupo very protective kulinda image ya mume wake.
Masikini Vince anatia huruma! Anataka ku fight for his marriage. Nafikiri ni vile anajiona yeye ni yatima na amekuwa kwenye Braxton family karibia miaka 20 na zaidi. Kumbuka Vince alikuwa Manager wa Toni Braxton kwa takribani miaka 10. Mkataba wake wa umeneja ulisitishwa baada ya kuamua kumuoa Tamar kwani Toni alisema hawezi kuchanganya undugu na kazi akimaanisha Vince amekuwa shemeji yake. Wakati huo huo kunatuhuma za domestic violence kati ya Vince na Tamar ambazo zimetolewa na mama yake Tamar. Kama asemacho mama mkwe wake ni ukweli basi nitakuwa nimeshangaa sana!! Kupiga mwanamke?! No! big No!
Mmh! Wishing her the best, nimefurahi sasa atajifunza kutokana na makosa. Maybe she will learn to put her ego down because she learned her lesson in a very hard way!
Zamaradi Mketema: Karibu tarehe 15th April ukumbi wa MAKUMBUSHO YA TAIFA
Regrann from @zamaradimketema - Tumejikuta tunatambua wanawake wengi ambao wamefanikiwa leo hii na kuwaangalia kama watu waliozaliwa wakawa tu hivyo walivyo kutokana na picha yao ya leo bila kujua struggles zao, machozi yao, mapito yao, kusota kwao, kushindwa kwao, kufeli kwao, kukataliwa kwao na hata mateso na changamoto nyingi zilizofunikwa na HALI ZAO ZA SASA. Katika safari ya maisha na utafutaji wengi huangalia CAPITAL kama ufumbuzi ama kitu pekee kinachotukwamisha kusonga kwenye NDOTO tulizonazo bila kujua kuna vingi huwa vinaturudisha nyuma wanawake na huenda ni matatizo makubwa kuliko kukosekana kwa capital ama vianzio, na hivyo vitu ndio vinafanya hata uwe na kazi ushindwe kuifanya ipasavyo ama hata kuichukia mara nyingine, ama kuna muda ujione huna tu thamani na kukufanya uogope na kunyong'onyea hata pale unapotakiwa kujitokeza na kutoa ulicho nacho, ama ushindwe kusimama vizuri kwenye biashara yako au kushindwa kabisa kuanzisha chochote kutokana na mengi yaliyokuelemea. Huenda kwasasa uko kwenye hii STAGE, na kuhisi mbele hamna maisha, jambo moja unalopaswa kujua ni kwamba HAWA WANAWAKE UNAOWAANGALIA KAMA MIFANO wengi wao wamepitia kwenye hatua ambazo upo sasa, kuna ambao waliwaza hata kujiua, kuna ambao waliwahi kukosa kabisa, kuna wale waliopoteza dira kiasi cha kutokujua cha kushika, na kuna kipindi walijiona hawana thamani kama ambavyo UNAJIONA SASA, lakini hawakukubali, WALIAMKA, na wakagoma kupelekwa na upepo huo, wakasimama imara na mpaka leo hii tunawapongeza na wengine kuwaita ROLE MODELS. Hivyo hata kwako, kwa hali yoyote unayopitia sasa, nataka nikwambie INAWEZEKANA!! nakuahidi utavuka na utaipita hiyo hali na kuwa mpya kabisa, na hakuna ajabu kesho tukakutolea reference kama mmoja wa mifano bora ya wanawake waliofanya maajabu. Amka kwenye huo usingizi, sio wewe peke yako unaeteseka, na hata kama unapitia manyanyaso, vikwazo, kutokuwa na Dira ya maisha ama changamoto yoyote iwe ya Kijamii, kihisia ama KIUCHUMI nakuhakikishia una nafasi kubwa ya kutoka huko na KUSIMAMA IMARA. Karibu tarehe 15th April ukumbi wa MAKUMBUSHO YA TAIFA POSTA opposite na IFM kwa mengi zaidi, The GOAL is to change LIFE. Na hii siku itakuwa mwanzo wa safari ya mafanikio kwa WENGI. NI BURE!!! - #regrann
Kesha la asubuhi: Tukiwa na vyombo vitupu
KESHA LA ASUBUHI ALHAMISI 12-04-2018 *TUKIWA NA* *VYOMBO VITUPU.* ? *Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu. 2 Wakorintho 4:7.* ✍? _Swali hili limeulizwa, “Ni aina gani ya vyombo ambavyo Roho huvitumia?” Kristo anasema nini? – “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi” (Mathayo 11:28-30). Ni aina gani ya vyombo vinavyofaa kwa ajili ya matumizi yake Bwana? – Vyombo vitupu. Tunapotoa kila uchafu moyoni, tunakuwa tayari kutumiwa._ ✍? _Je nafsi yetu tumeitoa? Je, tumeponywa kutokana na kupanga kibinafsi? Ah, natamani tungepunguza kuitumikia nafsi! Hebu Bwana asafishe watu wake, walimu na makanisa._ ✍? _Yeye ametoa kanuni iwe mwongozo kwa wote na katika hii hapatakiwi kuwa na namna yoyote ya kuiacha njia kizembe. Lakini huwa kumekuwa, na bado hili lipo, hali ya kuyumba kutoka kwenye kanuni za haki. Hali hii ya mambo itadumu kwa muda gani? Bwana atawezaje kututumia kama vyombo kwa ajili ya utumishi mtakatifu tusipoondoa vyote ndani yetu wenyewe na kutoa nafasi kwa ajili ya ya utendakazi wa Roho wake?_ ✍? _Mungu anawaita watu wake wamdhihirishe. Je, dunia itaonesha kanuni za uadilifu ambazo kanisa halishikilii? Tamaa binafsi za kuwa wa kwanza vitaendelea kuoneshwa na wafuasi wa Kristo? Kanuni zinazopendwa nao hazitawekwa kwenye msingi wa kweli, yaani Kristo Yesu? Ni vitu gani tutakavyoweka kwenye msingi, ili pasiendelee kuwa na uhasama, badala yake umoja, ndani ya kanisa?_ ✍? _Tutaweka kwenye msingi mbao, nyasi kavu au mabua? Je, badala yake si tulete vitu vya thamani - dhahabu, fedha, vito vya thamani? Hatutatofautisha kwa namna iliyo dhahiri kabisa kati ya makapi na ngano? Hatutatambua kwamba ni lazima tupokee Roho Mtakatifu mioyoni mwetu, kwamba anaweza kutuumba na kutengeneza maisha?_ ```Tunaishi nyakati za hatari. Kwa kumuogopa Mungu naweza kusema kwamba ufafanuzi wa kweli wa Maandiko ni wa muhimu kwa ajili ya maendeleo sahihi ya kimaadili kwa ajili ya tabia zetu.``` ```Mioyo na roho vinapokuwa vimefanyiwa kazi na Roho, nafsi inapokufa, ukweli una uwezo wa kudumu kupanuka na kuwa na maendeleo mapya. Ukweli unapoumba tabia zetu, utaonekana kuwa ukweli hasa. – Review and Herald, Feb. 28, 1899.``` *MUNGU AWE NANYI MNAPOTAFAKARI*
Mama’s trip to California
Mama yangu pamoja na mama Ruth wakiwa pembezo mwa daraja maharufu sana lijulikanalo kama The Golden Gate bridge huko San Francisco, California
Na hapa wapo kwenye mtaa mzuri uliotengenezwa kwa ustadi wa maua mazuri sana ujulikanalo kama Lombard street huko huko San Francisco, California
Kutoka kushoto ni Mama Otto, mama Igogo, mama Suleman Marando, na Mr and Mrs Apindi Adhero ?❤ Marafiki na majirani wa mama Apindi wakiwa wamekuja kujumuika nao kusalimia wageni wao Mungu ni mwema sana tuna kila sababu ya kumshukuru
Kwenye hili la Makonda na ‘watelekezwa’…….!
Regrann from @mutwiba - MJADALA Kwa wale wenye uelewa wa maswali yajayo naomba tusaidiane kuyatafakari na naamini tutapata majibu ama maswali zaidi yatakayohitaji ama kuleta majibu zaidi. Kwenye hili la Makonda na 'watelekezwa' nimejiuliza baadhi ya maswali. Na kwa kuwa penye wengi haliharibiki neno, wacha niulize hapa ili ukiweza jibu lolote kati ya maswali haya. MJADALA WA HESHIMA UTATHAMINIWA 1: Hili la wanawake kutelekezwa na watoto wao linatokea Dar tu ama hata mikoani lipo? 2: Wanaotajwa Dar wakikimbilia mikoani ambako mpango ama mkakati huu haupo, watasakwa ama? Na watakaotajwa kwa chuki na kuharibiwa mahusiano yao ya sasa watafidiwa? 3: Hili la kuwataja wanaume wanaoaminika kutelekeza watoto linatendeka kisheria ama ni ubunifu wa mkuu wa mkoa? Kama ni kwa mujibu wa sheria, si lifanyike nchi nzima? Kama ni ubunifu wa Mkuu wa Mkoa, akiacha ama kuachishwa kazi na ubunifu wake usio katika maandiko unakuwa umefia hapo? 4: Hudhani kwamba ingekuwa vema kuandaa workshop ama hata matangazo ya radio ya kuwafunza sheria za ndoa / mahusiano wanawake waliotelekezwa na wanaotaka kuingia kwenye mahusiano? 5: Mhe. Mkuu wa Mkoa akishakutana nao, wakishawataja watu waliowatelekeza, atawatatulia tatizo lao ama atawaelekeza Mahakamani ambako sheria ambazo zipo tayari zinastahili kuchukua mkondo wake? 6: kilichoonekana juzi ni kipi? (i) wanawake waliotelekezwa? (ii) wanaume waliotelekeza? (iii) mfumo wa sheria usiotenda haki kwa wanawake? (iv) wanawake wasiojua haki zao ambazo walistahili kuzisaka na kuzipata kabla ya kumfikia Mkuu wa Mkoa? Yaani kilichodhihirika leo ni jambo la kuihurumia jamii yetu kwa kutojua ama kupuuza sheria Na kwa kuwa na imani katika njia isiyotufikisha tunakotakiwa kwenda. My two cents. Na natunza haki ya kukosea na kukosolewa. Mzee wa Changamoto - #regrann
Kesha la asubuhi: Kwa Mioyo Minyenyekevu
*Kesha la asubuhi* _Kwa Mioyo Minyenyekevu_ *Jumanne Aprili 10, 2018* Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu. Isaya 57:15. ? Wale wote watakaolijia Neno la Mungu ili kupata mwongozo, wakiwa na akili za unyenyekevu zenye kupenda kujua, wakidhamiria kujua masharti ya wokovu, wataelewa kile yanachosema Maandiko. Lakini wale wanaokuja katika uchunguzi wa Neno wakiwa na roho isiyokubaliwa nalo, watachukua kwenye uchunguzi mwelekeo ambao uchunguzi huo haukuuweka. Bwana hatanena na akili ambayo haijali. Huwa hapotezi maelekezo yake kwa mtu ambaye kwa kukusudia kabisa hana kicho na amechafuka. ? Lakini mjaribu huwa anaelekeza kila akili inayokubaliana na mapendekezo yake, naye yuko tayari kuifanya sheria takatifu ya Mungu kuwa kama vile haina maana. Inatupasa kunyenyekeza mioyo yetu, tena kwa uaminifu na kicho tuchunguze Neno la uzima; kwani moyo ulio mnyenyekevu na wenye toba ambao ndio tu uwezao kuiona nuru. Akili, moyo, nafsi, ni lazima viandaliwe kuipokea nuru. Ni lazima pawepo ukimya moyoni. Ni lazima mawazo yasalimishwe na kuwekwa kwenye kifungo cha Yesu Kristo. ? Hali ya kujivunia ujuaji ya nafsi na kujitosheleza nafsi lazima vikemewe mbele za Neno la Mungu. Bwana huwa ananena na moyo unaojinyenyekeza mbele zake. Kwenye madhabahu ya sala, kiti cha enzi cha neema kinapoguswa kwa imani, huwa tunapokea mwenge wa kimbingu kutoka mkononi mwa Mungu unaoangazia giza letu na kutusadikisha juu ya umuhimu wetu kiroho. ? Roho Mtakatifu huchukua mambo ya Mungu na kumfunulia yeye aliye mwaminifu katika kuitafuta hazina ya kimbingu. Tukikubali uongozi wake, yeye hutuongoza kwenye nuru yote. Tunapotazama utukufu wa Kristo, tunabadilishwa na kufanana naye. Tunakuwa na ile imani inayotenda kazi kutokana na upendo na kusafisha moyo. Mioyo yetu hufanywa upya tena, nasi tunafanywa kuwa tayari kumtii Mungu katika mambo yote. –Review and Herald. *MUNGU AKUBARIKI MWANA WA MFALME*
Show me your friends
Kesha la asubuhi: Kuchimba Ndani Zaidi Kwenye Machimbo
*KESHA LA ASUBUHI* *JUMATATU APRILI 9, 2018* *Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. Matendo 17:11.* ?Ni sawa na sahihi kuisoma Biblia; lakini wajibu wako haukomei hapo; kwani inakupasa uchunguze kurasa zake wewe mwenyewe. Elimu ya Mungu haipasi ipatikane bila jitihada ya akili, bila maombi kwa ajili ya hekima ili upate kutenga nafaka ya kweli kutoka kwenye makapi ambayo watu na Shetani wamewasilisha mafundisho ya ile kweli visivyo. Shetani na muungano wake wa mawakala wa kibinadamu wamenuia kuchanganya makapi ya uongo na ngano ya ile kweli. Inatupasa tuchunguze kwa bidii hazina iliyofichwa na kutafuta hekima kutoka mbinguni ili tuweze kutenganisha uvumbuzi wa kibinadamu na maagizo ya Mungu. ? Roho Mtakatifu atamsaidia mtafutaji wa ukweli mkuu na wa thamani ambao unahusiana na mpango wa ukombozi. Ninawasisitizia wote ukweli kwamba kusoma Maandiko juu juu hakutoshi. Ni lazima tuchunguze na hii maana yake ni kutenda yale yote Neno linayomaanisha. Kama vile mchimbaji wa madini anavyochimbua ardhi ili kugundua mikanda yake ya dhahabu, wewe pia inakupasa uchunguze Neno la Mungu ili kupata hazina iliyofichika ambayo kwa muda mrefu Shetani amekuwa akitafuta kumficha mwanadamu. Bwana anasema, “Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo” (Yohana 7:17). ? Neno la Mungu ni ukweli na nuru na yapasa liwe taa miguuni pako, kukuongoza katika kila hatua kwenye njia iendayo kwenye malango ya mji wa Mungu. Ni kwa sababu hii, Shetani amekuwa akiweka jitihada za hali ya juu kuzuia njia ambayo imewekwa kwa ajili ya waliokombolewa na Bwana kuipitia. Haipasi uingie kwenye Biblia na dhana zako na kufanya mitazamo yako kuwa kiini ambacho kwa hicho ukweli yapasa uzungukie. ? Inakupasa uweke pembeni fikra zako kwenye mlango wa uchunguzi nawe ukiwa na moyo mnyenyekevu, nafsi iliyofichwa katika Kristo, na maombi ya dhati, inakupasa utafute hekima kutoka kwa Mungu. Inakupasa ujisikie kwamba ni lazima ujue mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa, kwa sababu yanahusu ustawi wako binafsi, wa milele. Biblia ni mwongozo ambao kupitia kwa huo unaweza kujua njia ya kufikia uzima wa milele. Kupita mambo yote, inakupasa ujue mapenzi na njia za Bwana. – Fundamentals of Christian Education, uk. 307, 308. *TAFAKARI NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI*
Toni Braxton akubali pete ya Mr Birdman
Je, wewe unampenda mtu kwa muonekano wake, taiba, familia aliyotoka, akili zake, sura, pesa, jinsi anavyokuonyesha heshima n.k? Mwanamuziki Brian a.k.a The Birdman anasema "so what? What that gotta do with love?" Hayo yalikuwa ni maneno yake baada ya Talk show host Wendy Williams kusema kuwa yeye alikuwa mtu wa kwanza kusema "hapana" aliposikia Toni Braxton ana mdeti The Birdman! Wendy amemueleza Mr Birdman kuwa muonekano wake na Toni ni tofauti sana hapo ndipo Mr "The Birdman" akasema vinahusiana nini na kupenda?! Yeye ni 'certified gangsta' ?? aliye kuzwa na street kwasababu mama yake alikufa akiwa na miaka miwili (2), baba naye japo hakuwa sana kwenye maisha yake naye alikufa, kaka, dada, bibi, babu wote wamekufa hivyo vitu hivyo vinemfanya asijue nini maana na thamani ya upendo lakini siyo kwamba hajui kupenda! "I’m just a gangster, that don’t mean nothing. Certified too. What that gotta do with love?" Wendy alishikwa na kigugumizi baada ya jibu hilo! Hilo nalo ni somo kwa wengi wetu tunaopenda kusema "kampendea nini?" Wewe ukiona watu wanapendana kama huna jema lakusema nyamaza lakini ukitaka kujua kampendea nini utaumbuka kwani hayo ni ya Ngoswe muachie Ngoswe mwenye! Kila mtu ana kitu chake ambacho anatafuta katika kumpenda mtu sasa mambo ya kujifanya mimi sijui "Engineer" ooh mimi "mfanya biashara" sijui msomi gosh!! What that gotta do with love?!! Kwani siku ukiwa huwezi kunyanyuka kitandani hizo degree zako zitakunyanyua kitandani? ?? Watu wanaangali potential ulizo nano! Unaweza ukawa mzuri na elimu nzuri lakini akili ya maisha hauna azidi ya kutaka kuwa "trophy wife" au "Mario" ulishwe na kuvishwa na mwanamke halafu bado utake uitwe mume ? anyway, Birdman amemvisha Toni pete yenye thamani ya $5,000,000
The Birdman siyo mwanaume pekee ambaye anatarajia kufunga ndoa na mtu ambaye watu wengi walidhani haiwezekani. Prince Harry naye mwaka jana mwishoni alimvisha pete ya uchumba muigizaji wa kimarekani ajulikanaye kama Megan Markle. Kwa hapa Megan ni mkubwa kwa Prince Harry kwa miaka mitatu (3yrs) na pia huko nyuma alishawahi kuolewa na kuachika. Ndoa yake ya kwanza ilidumu kwa miaka miwili (2 yrs) baada ya kudate kwa kwa muda wa miaka 6 ?? Hivi ndivyo vitu ambavyo sivielewi watu wadate kwa miaka sita halafu ndoa idumu kwa miaka 2 tu!! Tena hapo mpaka divorce imetoka ina maana atakuwa walitengana at least miezi 6 kabla ?♂️?♂️ Haya huyu Prince Harry ame mvika pete baada ya kumdate kwa muda wa miezi 15 (sawa na mwaka mmoja na miezi 3). Je, nitakuwa sahihi kusema ngoja tuone hii itadumu kwa muda gani au tuwatakie kheri tu ?
Btw, hata Toni Braxton hii itakuwa ndoa yake ya pili! Ndoa yake ya kwanza ilikuwa na mwanaume mwenye asili ya ngozi "nyeupe" ilidumu kwa muda wa zaidi ya miaka kumi na mbili (12 yrs) na alizaa watoto 2, Toni ana miaka 50 sasa.....Haya wale tunao pendeza hii show ya Braxton Family Values ndio tutakao faidi uhondo wote ? Siamini siku hizi nimemuambukiza mama yangu kupenda hizi show ?? anajua mpaka ratiba zake ??