USISAHAU MALIPO NI HAPAHAPA!!Hivi unanini wewe? umeolewa kama wanawake wengine, umemkuta mumeo anawatoto unaanza kuwa adui kwao na kuwatenganisha na baba yao. Au umeolewa baada ya mumeo kuachana na mke wa awali sasa umeanza kumwambia mumeo kila mabaya ya hao watoto wake na mazuri ya hao wakwako. Kiu yako ni kumweka mbali na wanae na kumfanya awapende wakwako. Kibaya zaidi unawashawishi wanao wawachukie hao watoto wa mumeo, eti unawaambia kuwa wao wanashea baba ila mama ni tofauti na kwamba wajiepushe nao sio watu wazuri. Hivi nia yako hasa ninini? Haujui kwamba kila ulipandalo utalivuna? Hujui kwamba “what goes around comes around?”. Usijefikiria ndio umefika, hujui hata kwanini mwenzako alitoka, nawewe unaweza kutoka vilevile – Chris Mauki
Picha nilizopenda siku ya leo
Tafadhali tumuunge mkono Miriam Mchirwa!
“We should all be feminists”!
Ni aibu sana kuona kuwa tupo 21st century na bado haya mambo yanatendeka! Kwamba wanawake hawatakiwi kuwa na ndoto za kufanya vitu vikubwa kisa hato olewa??!! Really! Asipo olewa anakuwa si mwanamke kamili!! Akiolewa hajazaa basi ndoa yake batili!! Akiolewa , kazaa watoto wa kike tupu bado anaonekana hajazaa!! ……….Akifanya mambo makubwa eti huyo uhuni ndo umemsaidia!! Kwakweli sauti ya mwanamke wa Kiafrica bado haina nguvu kabisa siyo tu katika jamii bali hata ndani ya familia nyingi!! Na hili swala halitaisha kama bado familia hazijatambua na kuona thamani ya mtoto wakike kuwa ni sawa na ya mtoto wa kiume! Haya matatizo yote yanayo husiana na mambo ya jamii huwanzia ndani ya nyumba na tiba yake huanzia nyumbani! Pia vile vile ni ngumu sana kukabiliana na hizi changamoto kama bado tunawachagua viongozi wakiume kusimamia mambo ya wanawake!!………Tafakari, fanya mabadiliko!
Happy birthday my sister!
Hot pic of the day
Sisterhood!
Strong walls shake but never collapse!
Hakuna kitu au jambo jipya hapa duniani! Vitu vingi tunavyo viona au mafundisho mengi tunayoyasikia huwa yanakua yalishawahi tokea na kusemwa huko nyuma na watu fulani! Tofauti inakuwepo kwenye namna ya usemaji au style ya maneno yanayo tumika kufikisha huo ujumbe mpaka kuonekana kama kitu kipya au kugusa hisia za watu……. Hivyo nimependa sana ujumbe hapo juu ? hasa sehemu hiyo ya mwishoni “strong walls shake but never collapse”!! Ni ujumbe ambao nimekuwa nikiusikia katika maneno tofauti tofauti lakini haya ya leo yamenigusa zaidi!……….. anyway, duniani kuna mambo mengi na watu waaina tofauti tofauti. Wengine wabaya, wengine wapo sawa kiasi, na wengine ni watu makatili wenye roho za Farao! Katika hao watu wapo watakao kupa furaha, wapo watakao kupa huzuni, na wapo watakao taka kukuangamiza kabisa kwasababu tu ya udhaifu wao na chuki walizo nazo juu ya nafsi zao lakini kwakuwa hawawezi jibadilisha hivyo wanaona kuumiza wengine ndio njia pekee ya wao kupata faraja! Katika hayo yote mema, mazuri, na mabaya tambua tu kuwa wewe ni ukuta imara ambao kamwe hauto anguka! Unaweza yumba kwa mtikisiko lakini hauto anguka kamwe!
Hongera sana Frank!
Naomba nichukue nafasi hii kumpa pongezi my cousin-brother Frank Laurent Sarungi wa Mbagala, Dar es salaam kwa kufunga pingu za maisha.
Nawaombea kheri, ndoa yenu idumu katika Bwana siku zote! Upendo, amani, vitawale daima ndani ya nyumba yenu.
Kwa faida ya wale msiomjua Frank: Ni mtoto wa marehemu baba yangu mkubwa. Yeye alizaliwa na ulemavu wa kuto sikia (kiziwi) na pia ana ongea kwa tabu labda niseme ni bubu kwa kiasi fulani ila anaeleweka…….Frank aliamia nyumbani kwetu baada ya kumaliza darasa la saba. Kwasababu ya upungufu wa shule nzuri za secondary na elimu ya juu kwa watu wenye aina ya ulemavu kama Frank, basi aliamua kujiunga na English course kwa muda wa mwaka mmoja na baada ya hapo alijiunga na chuo cha viziwi kilichopo Baltimore, Maryland, U.S.A ambapo alisoma hapo na kuhitimu degree yake ya Theology. Kwani nia yake ilikuwa awe Pastor kwa watu wenye ulemavu kama wake. Alijaliwa kumaliza chuo na kurudi nyumbani Tanzania ambapo amefanikiwa kufungua kanisa la watu wenye ulemavu wa kutokusikia. Na siku ya jana alifunga pingu za maisha.
Blessing naye alikuwepo kushuhudia
cake ikikatwa na Blessing naye hakutaka kupitwa ??
Nifuraha sana
Wifi mtu Maseline Obago akifungua champagne kwa madaha kabisa
Si kwa kucheza huko ???? Mzee Igogo na mama Igogo wakikumbushia enzi zao ……..yani hapo ilibidi mama Igogo aweke mambo ya usabato pembeni ?? ……. mzee Igogo na mama Igogo ndio wazazi walezi wa Frank toka alipo malizia darasa la saba na kuhamia kwenye himaya yao. Wao ndio walio msomesha Frank hapa Marekani na kumsaidia kuanza maisha alivyo rudi nyumbani Tanzania.
nafikiri hapa ulikuwa ni mwendo wa Arutu (Luo dance) nahisi ulikuwa ni ule wimbo wa “???bilima Cecilia, jaber osekao pacha?? bilima Cecilia awinjo chunya gombi ndi” ???……..Congratulations Frank. All the best!
Kutoka Facebook
Hot pic of the day
#FBF #Mahojiano na Linda Bezuidenhount
Leo nimeamua ku “Flash Back” videos za interview ambazo nilifanya na mwanamitindo wa kimataifa Ms. Linda Bezuidenhout mnamo mwezi wa Pili mwaka jana 2015!
https://youtu.be/7tmJgxbmB1A
Hapo juu ?nisehemu ya kwanza ya mahojiano. Na hapa chini ? nisehemu ya pili au ya mwisho ya mahojiano yetu.
https://youtu.be/rELfTBwva9g
Haya yalikuwa ni mahojiano yangu ya kwanza kabisa kufanya huku nikirekodiwa. Nilipewa hii nafasi ghafla, yani nilijua nataka kufanya mahojiano na Linda lakini sikujua lini yatafanyika. Mara ilikuwa siku ya juma Tatu napigiwa simu na kaka yangu Dj Luke wa Vijimambo blog nakuambiwa kuwa Linda ametukaribisha kwake siku ya Juma Mosi na yupo teyari kufanya mahojiano nami! Nilisita, lakini kaka yangu akasema nitaweza nisiogope! Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa. Kama hujawahi yaona basi nakuomba uyatazame na niruhusa kutoa maoni yako! ……….Kwakweli siku zote nitamshukuru sana Linda kwa nafasi hii aliyonipa na pia sito choka kuwashukuru kaka yangu Dj Luke wa Vijimambo blog pamoja na mtani wangu Mubelwa Bandio wa Kwanza Production kwa kunisaidia kufanikisha hii ndoto. Sina chakuwalipa bali nawaombea baraka siku zote! ??
Hoja: Ni laana au?!
Katika pita pita yangu huko Facebook nikakutana na huu mjadala ambao ulianzishwa na Stephen Mndalila kuhusu njinsi wenzetu (Wakenya) wanavyo waza mambo makubwa ya maendeleo na kuyatekeleza wakati sisi mambo tunayo yawaza na kutafakari ni aibu tupu……..! stephen alitoa hiyo comment ?baada ya kuona picha ya Mark Zuckerberg (Facebook owner) akiwa Nairobi, Kenya kwenye mazungumzo ya mambo ya maendeleo ya technology! …….embu jisomee mwenyewe halafu utafakari kwa kina ni nini wewe kama Mtanzania utafanya kusaidia nchi yako isonge mbele!
Mungu ibariki Africa. Mungu ibariki Tanzania ?
Hot Pic of the day: Mmiliki wa Facebook akila ugali na Samaki!
Kutoka Facebook
Historia imeandikwa: Kupatwa kwa jua, Rujewa, Mbeya, Tanzania
Siku ya leo (masaa ya Africa Mashariki) tarehe Mosi September, 2016 historia imeandikwa ndani ya Rujewa, Mbeya, Tanzania ambapo tukio kubwa duniani la kupatwa kwa jua (Sun/Solar eclipse) limetokea. Soma ? KupatwaKwaJua2016 ili ujifunze zaidi!
Watu wengi sana walijitokeza kushuhudia. Nitukio la kisayansi lenye faida nyingi kwa nchi yetu kihistoria, kiuchumi, na kiutalii! Tuna kila sababu ya kujivunia! ??
Picha shukrani kwa Clouds FM
HolleyPharm (T) LTD board meeting
Siku ya jana August 31st, 2016 HolleyPharm (T) Ltd walifanya mkutano wao mkuu unao fanyikaga kila mwaka (Annual Board Meeting). Mkutano huo huwa unahusisha all board members ambao ni shareholders, Directors, legal team, na top management kama wanavyo onekana hapo juu. Mkutano huo ulifanyika Slip Way Hotel, Dar es salaam, Tanzania.
Kushoto ni Mrs. Cecilia Igogo ambaye ni mmoja wa shareholders na Deputy Director wa HolleyPharm (Tanzania) akiwa sambamba na binti yake Mrs. Janeth O.O. Igogo-Nyagilo ambaye ni mmoja wa board members na mwanasheria wa HolleyPharm (Tanzania).
Mr and Mrs O.O Igogo ambao ni shareholders wa HolleyPharm, board members na majority shareholders wa HolleyPharm (Tanzania)
Hapa ni top Directors wakiwa na Mwanasheria Janeth Igogo-Nyagilo
Waliokaa ni shareholders, kushoto ni top management team, na kulia ni legal team ya HolleyPharm
Mr O.O Igogo (shareholder), Mrs Janeth O.O Igogo-Nyagilo (Lawyer, board member), Mrs Cecilia O.O Igogo (Shareholder, Deputy Director, and board member)
Mr and Mrs O.O Igogo
Mother and daughter
Maoni ya baadhi ya Watanzania baada ya #UKUTA kuhairishwa
Manhood!
“Ningekuwa mimi Mbowe” na Peter Sarungi

**Sehemu ya Kwanza**
WAKATI NI UKUTA: Katika Dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia ya habari na mawasiliano, WAKATI(Time) ni jambo la kuwekewa umakini mkubwa kupitia tafiti na uchunguzi wa jambo lolote lile unalotaka kulifanya. Wakati una tabia mbilimbili. Wakati haurudi nyuma wala hauna haraka, Wakati hunena na kuamua jambo, Wakati hutibu na kuzalisha vidonda, Wakati huishi na kufa, Wakati huelezea historia na kutunza, Wakati hutabiri yajayo na kutimiliza, wakati ni kipimo cha udhaifu na uimara, Wakati hutenganisha watu na kuunganisha, Wakati ni kiungo kwa mambo makubwa na madogo.
Wakati una nyakati nyingi na kila nyakati una zama zake na kila zama zina mambo yake. Leo naomba nivae viatu vya Mtu Huru kumwambia Mbowe kama Mkuu wa Chama mbadala (CHADEMA), Ni kweli kazi mliyoifanya kwa miaka zaidi ya 20 ya kujenga fikra mbadala katika siasa za Tanzania ni kubwa na yenye kuhitaji kupongezwa kwa moyo wa dhati kabisa (Hongereni sana). Lakini nasikitika kusema kuwa kazi yote hii ni kama 30% kati ya 100% ya wajibu wenu mlioamua kuutimiza juu ya siasa za nchi. Mimi ni mmoja kati ya watu wanaopenda vitu, matendo na fikra tofauti zenye kubadili mitizamo, imani na mienendo ya jamii maana naamini kuwa “FIKRA Tofauti Huzaa UBUNIFU na Ubunifu ndiyo chanzo na chachu ya MAENDELEO katika jamii”. Nchi yetu ipo katika nchi zinazofanya siasa za kuigiza, Siasa za majukwaa, siasa za propaganda, siasa za Ukweli kugeuka Uongo na Uongo kugeuka Ukweli, Siasa yenye kibwagizo cha Demokrasia, Siasa ya matabaka ya uelewa na vimelea vya Ubaguzi, Siasa ambayo mpinzani anatumia Chuki na vugurgu kutafuta madaraka na Mtawala akitumia vyombo vya Dola kulinda Madaraka yake, Siasa ambayo vyama vyake hutegemea Umasikini na Ujinga wa wananchi kama Mtaji wao, Siasa mabazo mifumo ya nchi huegemea upande mmoja, Siasa ambazo mwanasiasa anawekeza katika chama kuliko waliomchagua, Siasa zisizo na mabadiliko ya mbinu, Siasa za kungojea Marekani na Uingereza wamefanya nini ndipo nasi tuige, Siasa zisizo zungumzia ISSUES na badala yake zinazungumzia MATUKIO, Siasa zenye kulenga kizazi kilichopo tu badala ya kwenda zaidi kwa vizazi vijavyo, Siasa zenye kunukuu Fikra za Mwl Nyerere kama kikomo cha Fikra badala ya kuja na Fikra pevu zaidi, Siasa iliyoacha kutilia mkazo masomo ya siasa na uraia kwa vijana, Siasa ya UBEPARI katika nchi ya UJAMAA yenye mifumo ya utendaji ya URIBALELI…
Mtu huru anawezaje kufanya siasa katika nchi kama hii na ategemee kupata matunda huru? Nchi ambayo wananchi (wapiga kura wake) hawana uelewa juu ya HAKI na WAJIBU wao katika nchi, Hawajui kutofautisha ukweli na propaganda, Hawajui kutofautisha ushabiki wa vyama vya michezo na siasa, Hawajui mipaka yao wala ya watawala wao, Nchi ambayo mfumo wake kwa mwananchi tangu anazaliwa mpaka anazeeka ni Mtegemezi tu, Nchi ambayo walinzi wake ni wale ambao hawakufanya vizuri shuleni na wale ambao walikuwa ni wakorofi, majasiri na watukutu shuleni.
Kuna jambo Mtu huru amelisahau ambalo ni la muhimu sana kwa nchi kuwa huru. Apo ndipo WAKATI unapobadilika na kuwa UKUTA, Wakati wa siasa za chuki kwa vyombo vya Dola umepitwa, Wakati wa kuwaandamanisha wananchi wanyonge umeshapita, Wakati wa siasa za matukio umepita, Wakati wa siasa za migomo umepita. Kama Mbowe na timu nzima ya upinzani bado wana siasa za namna hii basi wajue kuwa wamefikia UKUTA na wana haja ya kubadilika.
Ningekuwa mimi ninkiongozi wa Upinzani kama alivyo Mtu Huru MBOWE basi ningefanya yafuatayo….
1. Ningewekeza na kuanzisha operation kwa wananchi za kutoa ukungu wa kuelewa haki na wajibu, siasa na uraia na kuwapa uelewa zaidi wa kijamii ili wawe huru na waweze kuja na fikra huru na mbadala katika nchi. Kwa sasa bado watanzania wengi hawajui mambo mengi ya siasa na hivyo maamuzi yao mengi yamekuwa ni ya kuiga na kufuata mkumbo.
2. Ningewekeza katika kurudisha mahusiano ya karibu sana na vyombo vya ulinzi na usalama. MBOWE, Huu sio Wakati wa kushindana na vyombo vya usalama ambavyo hata wao wengi hawana elimu ya uraia na ni vyombo vinavyoendeshwa kwa oder za wakubwa. Ni muhimu sana kwa chama mbadala kama Chadema Tanzania kuwa na watu kila idara kwa idadi kubwa katika vyombo vya usalama maana hivyo vyombo ndivyo vinavyotumika kulinda maslahi ya siasa za nchi.
#Mytake Tunahitaji Siasa Huru kutoka kwa wanasiasa Huru kwenda kwa Wananchi Huru wanaoweza kufanya maamuzi Huru katika nchi Huru ndio maana tunahitaji kutengeneza vyama Huru.
Asanteni sana