Tumerudi hewani!

Wapendwa wasomaji wangu, naomba mnisamehe sana tena sana kwa usumbufu uliotokea. Ilikuwa nje ya uwezo wangu, kwani damage iliyofanywa ilikuwa ni kubwa sana. Hackers wali hack my database na kuishambulia kisawa sawa! Hivyo shughuli yake ilikuwa ni pevu kwani sikutaka kupoteza hata kumbu kumbu moja! Nashukuru Mungu kwani kila kitu kimerudi kama kilivyokuwa hapo mwanzo. Nawashukuru sana Godaddy.com pamoja na WordPress kwa kazi nzuri waliofanya kwa muda wa zaidi ya wiki mbili. They’re my heroes! FB_IMG_1469659269564Haya mambo mswano, na sasa tuna logo yetu no more picture of mine hapo juu LOL!………….Asanteni kwa uvumilivu wenu!

Eid Mubarak to you all!

IMG-20160705-WA0010Eid Mubarak to all my Muslim readers, family, and friends!…. .Enjoy the blessings!

“Watanzania, mimi sikubali kuwa jiwe”-Mwl. J.K Nyerere

Kisa hichi kinanikumbusha story ya mke wa Lutu kwenye Biblia japo hakifanani sana lakini the moral of the story still the same. Ukitaka kusonga mbele na kuwa na mafanikio makubwa inabidi kuwa jasiri sana wakutosikiliza ya watu! Watu ambao wanajua kuwa “wamechemsha” kwa kutofata mashariti ya kufika to their “promise land” or destiny wengine huwa wanakua na busara na kutumia experience yao kwa kuwafundisha au kuwaambia wengine wasifanye makosa walio fanya. Lakini kuna ambao wanakuwa na hasira sana na wengine na kuanza kupiga makelele kwa wale ambao wanaonyesha muelekeo wa kufika kwenye nchi ya asali…….. Watu hao ndo wazushi, waongo, wachonganishi, wapika majungu n.k hayo yote wanafanya kuwakatisha tamaa wale ambao wanaonyesha dalili ya kufanikiwa. DON’T  NEITHER LISTEN NOR  JOIN THE NOISE MAKERS! They are nothing but biggest losers! USIKUBALI KUWA JIWE!!

My attitude today: Let no body treat you like an emergency survival kit!

2016-07-01 14.44.41

Tanzia: R.I.P Hon. Beatrice Shelukindo

Taarifa ya Msiba Screenshot_2016-07-05-08-36-28-1Familia ya Bwana William H. Shelukindo, Inasikitika kutangaza kifo cha Bibi Beatrice Matumbo Shelukindo kilichotokea siku ya Jumamosi 2/7/2016 huko Arusha.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu 8 Galu Street,Ada Estate, Dar es salaam na huko Arusha.

Mazishi yatafanyika siku ya Jumatano Tarehe 6/07/2016 alasiri Mjini Arusha.

Bwana ametoa Bwana, ametoa Jina la Bwana lihimidiwe. Screenshot_2016-07-05-08-09-22-1Poleni sana wana familia, ndugu, jamaa, na marafiki kwa msiba huu. Bwana alito, na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote! R.I.P Beatrice Shelukindo!

Words of wisdom

*WISE WORDS FROM A GREAT THINKER AND OBSERVER!!*

*Buffalos kill 7 people every year.*

*Lions kill 500 people every year.*

*Hippos kill 800 people every year.*

*Spiders kill 5000 people every year.*

*Scorpions kill 7000 people every year.*

*Snakes kill 10000 people every year.*

*And then, surprisingly,*

*Mosquitoes kill 2.7 million people every year. Yes, the smallest are the deadliest!*

*Small ‘sins’, hardly noticed by many, are the most deadly to your spiritual life.*

*Avoid excuses for not praying and allotting few moments of your day to your Creator.*

*Sins of omission are just as deadly as sins of commission.*

*Gossiping and small lies, are committed more frequently and are deadly.*

*Mind those little compromises that you do daily. They are the ones that will bring your downfall.*

*Successful people have two things on their lips, “Smile and silence”.*

*Smile can solve problems, while*

*Silence can avoid problems.*

*Sugar and salt may be mixed together*

*but ants reject the salt and carry away only the sugar.*

*Select the right people in life and make your life better and sweeter.*

*If you failed to achieve your dreams, change your ways not your Creator.*

*Remember, trees change their leaves, not their roots.*

*You will never reach your destination if you stop and throw stones at every dog that barks.*

*Haters will see you walking on water and say it’s because you can’t swim.*

*Even if you dance on water, Your enemies will accuse you of raising dust.*

*Make it your ambition to lead a quiet life, to mind your own business and to work with your own hands.*

*Remember Don’t ever wrestle with a pig. You’ll both get dirty, but the pig will enjoy it.*

*BE WISE!*

Source: One of THC members

Tangazo: Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka ya Mawasiliano

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO  MAELEZO YA KAIMU MKURUGENZI MKUU, MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA, ENG. JAMES KILABA KUHUSU UAMUZI KUHUSU UKIUKWAJI WA MASHARTI YA USAJILI WA NAMBA/LAINI ZA SIMU ZA MKONONI

Ndugu Waandishi wa Habari,

Tumewaita hapa leo ili kutoa uamuzi kuhusu mashauri ya ukiukwaji wa masharti ya usajili wa namba/laini za simu za mkononi uliofanywa na makampuni ya simu za mkononi.

Makampuni hayo ni:

1. Airtel Tanzania Limited,

2. Benson Informatics Limited ambayo inatumia jina la biashara la SMART,

3. MIC Tanzania Limited ambayo inatumia jina la biashara la TIGO,

4. Viettel Tanzania Limited ambayo inatumia jina la biashara la Halotel,

5. Vodacom Tanzania Limited,

6. Zanzibar Telecom Limited ambayo inatumia jina la biashara la Zantel.

Makampuni hayo yamekiuka masharti ya usajili wa laini na matumizi ya laini kama yalivyoaninishwa kwenye Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya 2010 na Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Leseni za 2011.

Kabla ya kuelezea uamuzi huo, naomba kwanza nitoe maelezo ya awali kuhusiana na suala zima la usajili wa laini/namba za simu za mkononi.

Itakumbukwa kwamba usajili wa namba simu umekuwa ni wa lazima baada ya sheria ya EPOCA ya 2010 kuanza kutumika. Kifungu cha 102(1) cha EPOCA kinafafanua kwamba mtu yeyote ambaye anamiliki simu ya mkononi ana jukumu la kutoa taarifa kwa mtoa huduma ikiwa kutakuwepo na mabadiliko ya umiliki wa simu hiyo au namba iliyosajiliwa kwa jina lake. Kifungu 102 (2) kinamtaka yeyote ambaye atataka kutumia simu au namba ambayo ilikuwa inatumiwa na mtu mwingine kusajili simu na namba hiyo. Aidha Kanuni za Watumiaji (The Electronic and Postal Communications (Consumer Protection) Regulations 2011) na Kanuni za leseni (Licensing Regulations 2011) zina vipengele kuhusu usajili wa namba za simu.

Kanuni ya 10(2) ya Kanuni za watumiaji kinasema mtu yeyote ambaye anamiliki au ana nia ya kutumia laini ya simu au kifaa chenye laini ya simu ndani anatakiwa kujisajili kwa mtoa huduma au wakala aliyeidhinishwa.

Kanuni ya 33(1) ya Kanuni za leseni kinaeleza kwamba mtu yeyote ambaye anauza au kwa namna yeyote ile anatoa laini ya simu au kifaa chenye laini ya simu ndani anatakiwa kuandikisha wateja kwa kutumia fomu maalum ambayo inamtaka mtumiaji atoe kitambulisho chenye picha yake halisi.

Sababu za kuanzisha utaratibu wa kusajili namba za simu ni pamoja na:-

(i) Kuwalinda watumiaji na jamii kutokana na matumizi mabaya ya huduma za mawasiliano.

(ii) Kuwezesha kuwatambua watumiaji wa huduma za ziada za simu, kama huduma za kibenki, kutuma na kupokea fedha, kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia simu kwa mfano kulipia huduma za maji, umeme, vipindi vya televisheni vya kulipia n.k.

(iii) Kuimarisha usalama wa taifa.

(iiii) Kuwawezesha watoa huduma za mawasiliano kuwafahamu vizuri wateja wao na kuwahudumia ipasavyo kadri ya mahitaji yao.

(v) Kuwa na taarifa za matumizi ya simu za mkononi kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya sekta.

Mnamo Aprili 2013 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na makampuni yanayotoa huduma za simu za mkononi walikubaliana juu ya hatua za kumaliza kasoro zilizokuwa zimejitokeza katika usajili wa namba za simu. Aidha walikubaliana kutokuwezesha laini/namba za simu kutumika kabla ya usajili kukamilika na taarifa za mteja kuhakikiwa.

Makubaliano mengine yalikuwa kwamba mitandao ya simu isifanye kile kinachoitwa ‘ usajili wa awali’.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inafanya ukaguzi wa mara kwa mara wa usajili wa namba za simu.

Hivi karibuni, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imekagua mifumo ya usajili wa laini za simu na kugundua ukiukwaji katika maeneo manne:

1. Namba kutolewa bila mteja kutakiwa kusajiliwa.

2. Namba kusajiliwa kwa majina, vitambulisho na nyaraka za watu wengine.

3. Namba kutokufungwa hadi usajili ukamilike

4. Namba kusajiliwa usajili wa awali.

Makampuni sita ambayo yaligunduliwa kutenda makosa hayo yote au baadhi yaliitwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania tarehe 2 na 3 Juni 2016 na kutakiwa kutoa utetezi wao kuhusu ukikwaji wa masharti ya Usajili wa namba za simu za mkononi.

Kufuatia kusikilizwa kwa mashauri hayo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilifikia uamuzi ufuatao kwa kila kampuni ya simu za mkononi husika:

UAMUZI:

Baada ya kusikiliza utetezi wa Mtoa Huduma kwa maelezo ya mdomo na maandishi, na baada ya kuzingatia utetezi huo, ni wazi kwamba Mtoa Huduma amekiuka kanuni ya 33 ya Kanuni za Leseni za mwaka 2011 zilizotolewa chini ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) na pia amekiuka vifungu 93,130 na 131 vya Sheria hiyo.

Kwa kuzingatia kwamba ni wajibu wa Mtoa Huduma kuhakikisha kwamba uuzwaji na utoaji wa laimi za simu unafanyika kwa mujibu wa kifungu 93 (2,3 na 4) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010, na Kanuni ya 33 ya Kanuni za Leseni za 2011 na kwamba Mtoa Huduma amekiuka matakwa ya Sheria; na

KWA KUTAMBUA KWAMBA matumizi mabaya ya laini/ namba za simu za mkononi kunahatarisha usalama wa Taifa na kunachochea tabia hatarishi katika jamii na kunaendeleza tabia za kiuhalifu nchini;

KWA HIYO BASI, Mamlaka inatoa AMRI kama ifuatavyo:

1. AIRTEL TANZANIA LIMITED ilipe kwa Mamlaka,ifikapo 30 Julai 2016 faini kama ilivyoainishwa hapa:

(a) SHILINGI 74,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Sabini na Nne) kwa kuruhusu kuuzwa kwa laini 148 bila kutumia kitambulisho halisi cha mnunuzi.

(b) SHILINGI 33,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni thelathini na tatu na laki tano) kwa kuruhusu laini 67 ziuzwe bila kujaza fomu ya usajili.

(c) SHILINGI 32,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni thelathini na mbili na laki tano) kwa kuruhusu laini 65 ziwashwe kabla ya kuuzwa; na

(d) SHILINGI 42,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni arobaini na mbili na laki tano) kwa kuruhusu laini 85 zifanyiwe usajili wa awali na kutumika kwenye mtandao wake.

2. BENSON INFORMATICS LIMITED ilipe kwa Mamlaka,ifikapo 30 Julai 2016 faini kama ilivyoainishwa hapa:

(a) SHILINGI 7,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Saba) kwa kuruhusu kuuzwa kwa laini 14 bila kutumia kitambulisho halisi cha mnunuzi.

(b) SHILINGI 7,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Saba) kwa kuruhusu laini 14 ziuzwe bila kujaza fomu ya usajili; na

(c) SHILINGI 3,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Tatu) kwa kuruhusu laini 6 ziwashwe kabla ya kuuzwa.

3. MIC TANZANIA LIMITED ilipe kwa Mamlaka,ifikapo 30 Julai 2016 faini kama ilivyoainishwa hapa:

(a) SHILINGI 93,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Tisini na Tatu na Laki Tano) kwa kuruhusu kuuzwa kwa laini 187 bila kutumia kitambulisho halisi cha mnunuzi;

(b) SHILINGI 43,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Arobainii na tatu na laki tano) kwa kuruhusu laini 87 ziuzwe bila kujaza fomu ya usajili;

(c) SHILINGI 41,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Arobaini na Moja) kwa kuruhusu laini 82 ziwashwe kabla ya kuuzwa; na

(d) SHILINGI 11,000,000 (shilingi za Milioni Kumi na Moja) kwa kuruhusu laini 22 zifanyiwe usajili wa awali na kutumika kwenye mtandao wake.

4. VIETTEL TANZANIA LIMITED ilipe kwa Mamlaka,ifikapo 30 Julai 2016 faini kama ilivyoainishwa hapa:

(a) SHILINGI 36,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Thelathini na sita Laki Tano) kwa kuruhusu kuuzwa kwa laini 73 bila kutumia kitambulisho halisi cha mnunuzi.

(b) SHILINGI 36,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Thelathini ba Sita) kwa kuruhusu laini 72 ziuzwe bila kujaza fomu ya usajili; na

(c) SHILINGI 34,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Thelathini na Nne Laki Tano) kwa kuruhusu laini 69 ziwashwe kabla ya kuuzwa.

5. VODACOM TANZANIA LIMITED ilipe kwa Mamlaka,ifikapo 30 Julai 2016 faini kama ilivyoainishwa hapa:

(a) SHILINGI 49,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Arobaini na Tisa) kwa kuruhusu kuuzwa kwa laini 98 bila kutumia kitambulisho halisi cha mnunuzi;

(b) SHILINGI 24,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Ishirini na Nne) kwa kuruhusu laini 48 ziuzwe bila kujaza fomu ya usajili;

(c) SHILINGI 19,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Kumi na Tisa) kwa kuruhusu laini 38 ziwashwe kabla ya kuuzwa; na

(d) SHILINGI 4,500,000 (shilingi za Milioni Nne na Laki Tano) kwa kuruhusu laini 9 zifanyiwe usajili wa awali na kutumika kwenye mtandao wake.

6. ZANZIBAR TELECOM LIMITED ilipe kwa Mamlaka,ifikapo 30 Julai 2016 faini kama ilivyoainishwa hapa:

(a) SHILINGI 36,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Thelathini na sita na Laki Tano) kwa kuruhusu kuuzwa kwa laini 73 bila kutumia kitambulisho halisi cha mnunuzi;

(b) SHILINGI 11,500,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Kumi na Moja na Laki Tano) kwa kuruhusu laini 23 ziuzwe bila kujaza fomu ya usajili;

(c) SHILINGI 7,000,000 (shilingi za Kitanzania Milioni Saba) kwa kuruhusu laini 14 ziwashwe kabla ya kuuzwa; na

(d) SHILINGI 2,000,000 (shilingi za Milioni Mbili) kwa kuruhusu laini 4 zifanyiwe usajili wa awali na kutumika kwenye mtandao wake.

Pamoja na faini hizi, Watoa huduma hawa wametakiwa kuchukua hatua zifuatazo:

a) Kuwasilisha Mamlaka a Mawasiliano Tanzania ifikapo 15 Julai 2016 orodha iliyohakikiwa ya wakala wa kusambaza na kuuza laini za simu nchi nzima kama inavyotakiwa na kifungu 92(2) cha EPOCA;

b) Kuacha mara moja kuwatumia wakala au wasambazaji wasioruhusiwa kuuza au kusambaza laini za simu nchini;

c) Kuhakikisha kwamba laini za simu zinauzwa na Wakala anayetambuliwa na Mtoa Huduma na ambaye ana anwani ya makazi inayofikika na pia mwenye Namba Tambulishi ya Mlipa Kodi (Tax Payer Identification Number); na

d) Kuzima laini zote zilizo sokoni ambazo zimewashwa na kuwasilisha taarifa ya utelekezaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ndani ya siku saba kutoka tarehe walizopokea Uamuzi huu.

Mtoa Huduma yoyote atakayekaidi utekelezaji wa AMRI atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kushtakiwa kwa makosa ya jinai.

Mwisho, napenda kumalizia uwasilishaji wa uamuzi huu kwa kusisitiza yafuatayo:

Utaratibu wa kusajili laini za simu za mkononi unawahusu watoa huduma na watumiaji pia. Watumiaji, watoa huduma, wakala wa makampuni ya simu za mkononi na wananchi kwa ujumla wanakumbushwa kwamba ni kosa kisheria kutumia au kuwezesha kutumiwa kwa namba ya simu ambayo haikusajiliwa.

Ni kosa la jinai kutumia namba ya simu isiyosajiliwa. Adhabu ni faini ya shilingi laki Tano au kifungo cha miezi mitatu. Kusajili nenda kwa mtoa huduma wako au wakala wake ukiwa na kitambulisho chenye picha yako. Toa taarifa sahihi.

Aidha ni kosa kusajili laini kwa kutumia majina yasiyo sahihi.

Watumiaji wote ambao hawasajili namba zao za simu wafanye hivyo mara moja. Kuthibitisha usajili wako piga *106#.

Asanteni kwa kunisikiliza.

IMETOLEWA NA:

KAIMU MKURUGENZI MKUU,

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

4 JULAI, 2016 TCRA_clipMaoni ya mtumiajiScreenshot_2016-07-05-08-08-08-1Updates

Screenshot_2016-07-05-11-07-54-1Screenshot_2016-07-05-11-07-06-1Screenshot_2016-07-05-22-43-54-1

In loving memory of Advocate Joseph Stanley Mbuna

Wapendwa wasomaji wangu, hapa tupo kwa ajili ya kufunzana, kufurahi, na kucheka. Na pale inapokuwa ngumu kufanya hivyo kwasababu ya mitihani ya dunia hii basi tutafarijiana na kupeana moyo…….Basi miaka 7 ilivyo pita, siku ya tarehe 2 mwezi wa 7, mmoja ya wadau wangu (nimemuita “mdau” kwasababu huwa natumiaga picha zake na za familia yake hapa kwa hii blog bila tatizo lolote) alipatwa na msiba wa baba yake mzazi. Hivyo imekuwa ni taratibu ya familia yao kufanya ibada ya kukumbuka mpendwa wao kulingana na imani ya dini yao na mila zao. Kwa kawaida huwa wanaenda kwenye kaburi la baba yao na kusafisha kama picha zinavyo onekana hapo chini! ?…….. Kwakweli siwezi wadanganya mimi binafsi ndio kwa mara ya kwanza kuona ibada hii inavyo fanywa (japo nikwenye picha). Huwa nasikia watu wakisema walienda kusafisha kaburi lakini sikuwahi shuhudia wala kuona kwa picha. Hivyo nimejifunza kitu hapa!….. Naomba usinicheke au kunishangaa ila elewa yakwamba mimi ni Msabato na kwenye ukoo wetu wengi ni Wasabato hivyo ibada kama hizi huwa hatuzifanyi kwani Wasabato hatuamini katika ibada baada ya kifo!…… Naona hata aibu kusema, lakini hali halisi ya yale makaburi ya kwetu Utegi ni pori hata nyoka nadhani wanaishi humo ??? upande wa mama yangu wao ni Roman Catholic hivyo mama zangu wakubwa na wajomba zangu ndo huwa nasikia wakienda safisha makaburi. Mama yangu alibadili dhehebu yeye ni Msabato hivyo huwa ashiriki ibada hizo ?? …… anyway nimejifunza kitu kuwa siyo lazima kufanya ibada kama wengine bali unaweza kupatengeneza pawe pasafi just for the dignity. Enyi Wasabato wa Bongoland msije nitoa roho ??? Wasabato wenzetu wa huku makaburi yao masafi kuna watu wanasafisha kila siku. Sasa nyie vipi bwana ?? acheni hizo ??

Ok hivi ndivyo Foster alianza siku yake. Kwa kuweka status hii kwenye Facebook account yak. Very touchy!……Screenshot_2016-07-04-19-22-03-1Screenshot_2016-07-04-19-21-46-1FB_IMG_1467678090743FB_IMG_1467665450271Kaburi la marehemu mzee Joseph Stanley Mbuna kama linavyo onekana  FB_IMG_1467665535996-1Mama, mke wa marehemu ambaye pia ni mama mzazi wa Foster na bibi yake the Upcoming stylish Nathaniel  (mchungulie hapa)
FB_IMG_1467665494271-1Foster akiwa na mama yake Mrs. MbunaFB_IMG_1467665469712-1Kazi ya kusafisha ikiendelea…..ukimtegemea Mungu hata kwenye huzuni na maumivu makali utapata nguvu!FB_IMG_1467665432075FB_IMG_1467665514314Foster na mdogo wakeFB_IMG_1467665442402Foster na wadogo wakeFB_IMG_1467665421023Foster na mdogo wake pamoja na wanawe FB_IMG_1467665475278Foster akipozi kwenye kaburi la babaFB_IMG_1467665463030FB_IMG_1467665456999Mama Foster na wanawe FB_IMG_1467665426716Uncle and nephewsFB_IMG_1467665409576Wapendwa, poleni sana kwa msiba wa baba. Mungu wa Mbinguni azidi wapa faraja kwa kutegemea yeye pekee kuwa yeye tu atosha! Upendo, amani, na mshikamano vikadumu siku zote katika familia yenu!……… Bwana alito, na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote……. Azidi kupumzika katika amani ya Bwana marehemu mzee Joseph Stanley Mbuna !

NOTE: Picha zote kwahisani ya E.P.M photography. Kwa mahitaji yako ya picha tafadhali usisite kuwatafuta. Kazi yao ni nzuri na matokeo utayapenda!

Avery child deserves a champion!

Hello parents!…… How you talk to your children matters a lot! Because is what they hear in their heads and stays in their hearts! Be careful of how you motivate them instead of empower them. Sometime rise will pick up where you left off if you are intimidating them instead empowering them. You need to talk to your children according to their age appropriate in order to connect and get them to understand you. Children always make mistakes that’s why they are children! Don’t destroy your child self-esteem just because she/he has made some mistakes! All genius people learned through their mistakes! Let children be children!FB_IMG_1467655741747

Cheka uongeze siku za kuishi

FB_IMG_1467655826925-1??? no fooling around, praying like never before ???

Hello to all “The Alpha” females!

IMG_20160628_155205-1FB_IMG_1467607694813

Mother and daughter moment

FB_IMG_1467556839637Mwajuma and her Princess …..pendeza sana mbarikiwe

Teaching is a work of heart!

IMG-20160704-WA0000Being genius itself doesn’t make someone a great teacher. It takes more than a smart brain to be a teacher! It’s a calling!…….I’m very proud of my childhood friend, neighbor, Mgulani primary school mate, and Kowak Girls secondary school mate for doing this amazing calling of transforming people lives through teaching!…….May the good Lord keep using her and other good teachers to make this world a better pleasant place to live! IMG-20160704-WA0001Mungu abariki Walimu wote!……..Furaha you are the best ❤❤❤

Happy Independence Day to all Americans! & Happy 18th Birthday to Malia Obama

FB_IMG_1467641825863Wishing you all a very Happy Independence Day. Be blessed. ……… And Happy 18th birthday to Malia Obama and all July born babies ❤❤❤ FB_IMG_1467636627743Isn’t that cute and Poweful! Dad is holding her handbag! Setting the records straight of how the ‘next king’ should treat her daughter! Lovely! FB_IMG_1467641794568Beautiful!

Maneno ya hekima!

Screenshot_2016-07-04-07-49-23-1

Wana BCoy, Ruvu 91 wajumuika pamoja

IMG-20160702-WA0010Wana BCoy Ruvu 91 wakiwa kwenye kikao cha umoja wao kilicho fanyika Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Mmh! Nimesahau kuuliza majina yao ?? but kama wewe ni Alumni wa BCOY Ruvu 91 basi unaombwa kujumuika na wenzako waliopo kwenye picha IMG-20160702-WA0009Mwl. Nkuba next time please toa utambulisho basi ??……. anyway nice pictures

UPDATES:IMG-20160704-WA0003Mr Casmir Nkuba na Ms. Jacky baada ya kusalimiana IMG-20160704-WA0002Kushoto ni Mh. Erasto Tumbo, Mbunge mstaafu, baada ya kumpokea Mr Casmir alipofika kwenye kikao cha timu ndogo ya kuratibu reunion ya BCoy 91. Kikao kilifanyika Nguruko Annex , Dar, TzIMG-20160704-WA0004Wana BCoy, Ruvu 91 wakila, kunywa, na kufurahia pamoja……Kuna wengine toka Australia na U.S.A nao wapo njiani watajumuika nao katika kikao kijacho!

You are who are, and you’re enough!

No matter who you are, what you look like, or what you share with the world, there will always be someone who doesn’t approve. And that’s okay. You’re not going to like everyone and not everyone is going to like you. And that isn’t some fundamental failing on your part — that’s just life. It’s normal, and it’s nothing to beat yourself up over. There’s nothing wrong with wanting to be accepted, but you shouldn’t ever have to change who you are for the sake of winning someone else’s approval. You don’t live for other people. It isn’t your job to conform to their idea of what constitutes a “worthwhile” human being. You are who you are, and you’re enough. Instead of focusing on all the people who don’t accept or appreciate you, take some time today to remind yourself of all the people who do. It’s easy to forget about them, but they exist and they care. They’re the people who matter. To them, you matter. Let go of the rest.

2016-06-30 09.17.03Whoever wrote that ☝ (from one of THC members) may God bless your heart! You have touched my heart today in so many ways! Blessings be upon you ?

 

Tafadhali saidia kumtafuta mzee Munuo!

IMG-20160703-WA0007Anayeoneka kwenye picha hapo juu anaitwa Philemon Anamwikira Ikaa Munuo, miaka (61). Ametoweka kuuanzia siku ya juma tano tar.29.06.2016 nyumbani kwake Bunju B Dsm, Tafadhali yeyote atakaemuona apige simu Police au Kwenye number zifuatazao…… 0713449666 (Rich) 0754226760 (Tumsifu) 0713552828 (Rodrick) 0718555909 (lucas) 0713481648 (Tumaini)……Tafadhali sambaza ujumbe huu.

Tunakuwa wema kwa watu baki, lakini majumbani ni shida!

Tunakua wema kwa watu baki, lakini majumbani mwetu hasa kwa watoto zetu shida tupu

Nilikuwa nikiwahi kazini, nikiwa natembea haraka haraka nikaparamiana na mtu ambaye sikuwa nikimfahamu ” kwa kujishusha na kwa ukarimu nikamwambia samahani sana ndugu yangu, sikukuona ndio maana nikakuparamia, nisamehe sana.” FB_IMG_1467435053811Nilikuwa mpole mno wakati nikimwambia hayo. Na alinielewa na kunisamehe. Nikaendelea na safari yangu.

Lakini nyumbani ilikuwa ni hadithi nyingine. Jioni ya siku ile wakati napika jikoni, binti yangu alikuwa nyuma yangu akiwa amesimama. Nilipogeuka nilimparamia na kumuangusha.

Nilimkaripia nakumwambia pumbavu sana sasa unakaa nyuma ili iweje, haya inuka na uondoke hapa upesi sitaki nikuone!

Aliinuka na kuondoka pale kwa huzuni huku akilia. Sikutambua ni kwa jinsi gani nilikuwa mkali kwake.

Usiku wakati nimelala usingizi haukunijia na nikaanza kuwa katika fikra nzito nikafikiri nikiwa nimekwaruzana na watu nisiowafahamu barabarani nakuwa mpole kwao na kuomba radhi, ila kwa mwanangu nimpendae nimemuangusha hata samahani sijamuomba zaidi nimemkaripia!

Nikiwa naendelea kuwaza hilo akili yangu ikanisukuma niende nikaangalie angalie jikoni, kwenda kuangalia nikakuta maua yakiwa chini sakafuni ni maua ambayo binti yangu aliyachuma na alitaka kunipa kwa kuni suprise.

Niliyakusanya yale maua vizuri na nikayaweka ktk muonekano wake na nikaelekea chumbani kwa binti yangu. Niliinama na kumuamsha “amka mwanangu, amka!” haya maua ulichuma kwa ajiki yangu?

Alitabasamu a kuniambia “nimeyaona nyumba ya jirani nikaomba nikate machache kwa sababu ni mazuri kama wewe mama yangu” hapo hapo nikamwambia “binti yangu samahani sana kwa nilivyokua mkali kwako baada ya kukuangusha, sikutakiwa kukukalipia” binti akaniambia “usijali mama yangu, hata hivyo nakupenda” nikamwambia nami nampenda na nimeyapenda maua. Nikamfunika vizuri na kumtakia usiku mwema.

Usiku ule mwanangu alifariki kwa kubanwa na pumu, niligundua hilo baada ya asubuhi kwenda kumuamsha awahi shule. Nililia mno! Mpaka leo sijamsahau mwanangu machungu mengi mno moyoni mwangu.

Huwa najiuliza ingekuwaje kama angefariki na kinyongo cha mimi kumkaripia siku ile? Ila ninachoshukuru Mungu nilitengeneza amani nae kwanza. Ndipo mwenyezi Mungu akamchukua.

Muhimu: 

Hivi unajua kama ukifa leo kampuni yako unayofanyia kazi wanaweza wakamweka mtu mwingine kwa kipíndi kifupi tu kwenye nafasi uliyoiacha wazi?

Lakini kupoteza mwanafamilia ni hasara kubwa na pengo halizibiki kamwe! Umeshajitathimini na kujiona ni jinsi gani unaetendea familia yako? Mke wako, watoto wako au wazazi wako. Najua unaweza ukawa umejisahau.

Jifunze kuwatendea mema wapendwa wako, isije kuwa majuto ni mjukuu. Na kumbuka vitu hutumiwa na watu hupendwa.

Neno “Ningejua” huja mwisho wa safari

Mungu atusaidie.

Source: Tweve Hezron Facebook page 

Ramadhan Kareem!

FB_IMG_1467398207985Ramadhan kareem to all Muslims………..Happy Sabbath to my fellow believers…………Praise the Lord…….Sorround yourself with LOVE!

Blog