Fathers: Son’s first hero and daughter’s first love! – part 1

Tunapoelekea kusherekea siku ya wakinababa dunia (June 19th) je, umeshawahi kujiuliza wewe ni baba wa ina gani? Au unataka kuwa baba wa aina gani? Au unamuandaaje kijana wako / mtoto wako wakiume kushika title hii “baba”? Au wewe ni yule mzazi unaye subiria mtoto ajifunze kutoka mtaani halafu siku aikifanya kinyume na matarajio yako unaanza kumgombeza utafikiri ulishawahi kumfundisha njia iliyo sahii!

Unaweza dhania kuwa mtoto wako ni mtoto bora kwakuwa anapata “As” darasani au anapata Academic Awards nyingi lakini kupata A au academy awards hakumfanyi mtu kuwa good citizen wa hii dunia, wala hakumfanyi kuwa a good man / woman, wala hakumfanyi kuwa a good husband / wife, au a good father / mother. It takes more than getting “As”  in class or academic achievements to make your child a greater human being! Don’t get me wrong, Im all for academic excellence achievements thingy, I adore smart and genius people in all type of academic field, but let me quote Aristotle “educating the mind without educating the heart is no education at all”! Mtoto anatakiwa kupata malezi bora! Yes, wapewe elimu ya dunia lakini nilazima mtoto apewe elimu ya kimbingu / kiroho pia ili kumsaidia kuwa kiumbe bora!

Ulisha sikia kwenye news wanasema “she / he was an A student au alikuwa na excellence academic records”  halafu wanashindwa kuelewa ni kwanini ame made a very poor choice ambayo ina m-cost probably for life! Narudia, “educating the mind without educating the heart is no education at all”!!……… Halafu mimi nimeshaona mara nyingi hawa watu amnao wao wana ji-consider ” educated” wengi wao wako so “ignorant” with a chip on their shoulders like they know more than others or they are the best in making good decision(s)! Wakati ukweli ni kwamba hawa watu often their intelligence level is low! Huwa mara nyingi wana make decisions zao based on their friends that they consider to be in the same “level” which; often ina wa cost sana na hata ku destroy their academic achievements that they worked so hard for! Plus most of them wapo insecure na wanakuwa intermediated with people who got talent!

Watu maharufu walio wengi (sisemi wote) ukisikiliza story zao utasikia wakiongelea juu ya mama zao sana au bibi zao upande wa mama kuliko baba zao. Na hii nikutokana na mateso ambayo wamepitia au shida walizo pata kutokana na tabia au life choices ambazo baba zao walichagua! Tyler Perry ni mmoja ya watu ambao baba yake alimtesa sana yeye pamoja na mama yake pamoja na ndugu zake wengine. Kama mnavyo msikia kwenye hizi interviews

Manyanyaso katika familia yapo ya aina nyingi na katika ngazi tofauti haswa kama baba ndiye mwenye kipato kikubwa kuliko mama. Kuna wababa ambao wanatumia pesa zao kunyanyasa familia zao. Yani mambo yake yeye ndio yafatwe hata kama yanaangamiza familia! Au unakuta baba ana hela lakini hataki somesha watoto au kusaidia kitu chochote kile chamaendeleo ya watoto. Kazi yake ni ku-destroy watoto wake financially and emotionally! Wababa wa aina hii mara nyingi wanakuwa very addicted na hii tabia kiasi yakwamba hataki kuona watoto wake wanafanikiwa na kitu chochote especially kuwa na financial freedom ili tu aendelee kuwanyanya! Ushaona wababa ambao behind the science wao ndio wana destroy watoto zao?! Na huwa ni ngumu sana watu kuamini haswa kama wamefanikiwa kutengeneza mazingira fulani yakuaminika katika jamii! Inahitaji watu makini sana kuelewa watoto ambao wako kwenye mikono ya wababa wa namna hii!

Basi unapoangalia hizi videos za interviews zake,  kama wewe ni baba tafakari je ni baba wa namna gani na unampango gani kubadilisha mwenendo wako kama mwenendo wako unafana na wababa yake na Tyler Perry. Nakama ni baba mtarajiwa je unajiandaaje kuwa baba mwema? Na kama ni mama au baba mwenye mtoto wa kiume je unamuandaaje kijana wako kuwa mwanaume na baba bora katika jamii!……. Kuna wa baba walio wema wazuri kuliko hata mama hao tutaongelea siku nyingine!

Mimi ni Kipepeo-Nuya Helen Dausen

FB_IMG_1465433625996Nuya Hellen Dausen ( @nuyahellen ) mmoja kati ya Watanzania wawili waliotajwa na jarida la #FORBES kuwa mjasiriamali mwenye umri chini ya miaka 30 (Forbes 30 Under 30) leo amezungumza katika #Clouds360 ya #CloudsTv. Akizungumzia hatua alizopitia Nuya amesema ailianza biashara baada ya Kutoka Marekani kupata mafunzo ya Uigizaji na kujikuta hana kazi kwa miezi 8 na ndipo akaanza Biashara ya vipodozi vya asili.

Nuya ambaye amesoma Masuala ya Filamu na International Trade anasema “Nilianza ‘kugoogle’ na kuangalia video YouTube ili nijifunze kutengeneza vipodozi. Nilianza kutengeneza lakini nikawa nakosea. Baadae nilipata Mwalimu huko Malaysia. NIlikwenda Malaysia ambapo nilikuwa sijui mtu huko lakini nilikutana na mwalimu wangu ambae alinifundisha vizuri nikarudi nyumbani kuendelea na biashara yangu”.

Nuya anasisitiza kuwa “Mimi nilianza kuangalia biashara hii kwa nchi za wenzetu, wao wameanza Biashara hii miaka mingi na “they are making a lot of money” Mimi niliona #Fursa huko nikaishika. Kwa Forbes kunichagua kwenye list yao, wamenihakikishia kwamba kweli ninaweza kufanikiwa”.

#Forbes wamemtabiria Nuya Hellen Dausen kwamba ndani ya Miaka 20 ataweza kutengeneza takribani Dola Milioni 200. Yeye mwenyewe anasema ataweza kupata pesa hiyo kabla ya miaka hiyo.(Sababu yeye ni #Kipepeo Anajitambua, Hana wasiwasi na Safari yake pia Anajisimamia)

Source and Credits to Clouds Media Screenshot_2016-06-09-09-52-06-1

Nuya Hellen Dausen ni msichana wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 29 ambaye ametajwa kuwa miongoni mwa vijana 30 wa Afrika ambao ni mabilionea wa siku chache zijazo.

Jarida la Forbes ambalo ni maarufu kwa kutoa takwimu na ripoti mbalimbali za watu na pesa zao, watu na harakati zao lilimtaja Hellen na Mtanzania mwingine mmoja aitwae Edwin kuwa ndio watanzania pekee kwenye list hiyo ya Mabilionea 30 ambao watakua mabilionea baadae na kuajiri maelfu ya watu.
Mbali na Watanzania hawa mabilionea, pia kutana na mastaa wengine kutoka Tanzania kwenye Inside Bongowood, Jumanne saa 15:30 kwenye Maisha Magic Bongo
Hellen ni bilionea wa siku chache zijazo lakini pia ni mtu anaependa burudani japokuwa ana zaidi ya mwaka mmoja hajawahi kwenda night club.
1. Anasema toka ameanza kuwa mjasiriamali amekua na mawazo ya tofauti na hata msukumo wa kustarehe sana kama kutoka kwenda night club umepungua kwa kiasi kikubwa, kila siku anawaza anapigaje hatua za keshokutwa.
2. Miongoni mwa wasanii ambao anasikiliza sana nyimbo zao ni pamoja na Vanessa Mdee kama Nobody But Me, Niroge na Nitajuta ya Yamoto Band.
3. Starehe yake kubwa ni kwenda ufukweni ambapo anasema, “Napenda sana kwenda kulala beach, nitalala hata masaa matatu na inanisaidia kupata mawazo mapya au kuyajenga niliyonayo.”
4. Series ambayo amewahi kuitazama na hatoisahau niPrison Break, ni series ambayo hata akiambiwa arudie kuitazama hatokataa japo ametazama series nyingi, hiyo ni namba moja kwake.
5. Channel ambazo huwa anazitazama sana kwenye King’amuzi cha DStv ni pamoja na E! na MTV Base.
source: Dstv.com

My attitude today: Exist on your own terms!

2016-06-08 21.22.46

Hot shot of the day

FB_IMG_1465435868405watoto wote ni wazuri, I mean hakuna binadamu mbaya. Lakini lazima tukubaliane kuwa kuna wengine Mungu aliwaumba kwa upendeleo zaidi!! What a cute baby boy! Look at those eyes, lips, eyebrow, I mean this baby is Dope!…. Hivi huyu akiwa mwanao hata Daycare utakubali kumuacha kweli ?? Yani roho yako itakuwa juu juu kama marehemu mtarajiwa ??? Halafu mtoto kama huyu ananoga zaidi kama mambo ya dolla nayo yametulia ati!

Nimeona kuna mtu kauliza watu Facebook kuwa je huyu angekuwa mtoto wako ungempa jina gani? Mimi kama angekuwa wangu ningemwita Micah (which means, “who is like God?” In Hebrews) au ningempa Gabriel  (which means “God is my strength”)

Mungu amlinde huyu mtoto na mapepo yooote ya hii dunia ??

“Mwanaume bora havai mlegezo (sag trousers)”

Kama wewe ni mwanamke na haujaolewa na upo kwenye mauhusiano na mwanaume ambaye haujafunga naye ndoa basi zingatia hili, linaweza kukusaidia na kukupa nuru nzuri ya ndoa bora yenye tija katika maisha yako ya mauhisiano.

Chagua mwanaume bora kwa kutizama utashi wake na mawazo yake chanya, mwanaume bora ni yule aliyekuzidi utashi, tabia nzuri pamoja hekima na busara na mwenye mapenzi ya dhati kwako.

Mwanaume anayekufaa ni yule anayekujali na kukuheshimu, mwanaume bora ni yule anayekupa mawazo ya kesho akiwa leo,mwanaume anayekufaa ni yule anayekufuta machozi na asiyekuliza kila siku.

Dada yangu tafuta mwanaume ambaye ni kichwa ili wewe uwe shingo sababu hakuna kichwa pasipo shingo.

Tengeneza mwanaume wako bora, anza naye kwenye maisha ya chini mkipeana faraja na matumaini ya kutengeneza ndoa bora na yenye mafanikio ya kipesa, na mauhisiano yenye afya yaliyo na mapenzi matamu na bora, usipende wanaume wa wanawake wenzio mtengeneze handsome wako.

Dada yangu achana na mabrothermen wanaopaka poda ,wanawanaotembea na selfiestick hawana tija, mwanaume bora havai mlegezo (sag trousers).

Mwanaume bora hata kama hana pesa daima huwa na hazina ya mawazo na ndoto zenye matumaini ya kuwa na future nzuri baadaye.

Achana na wanaume maarufu wengi wao hawana mapenzi ya dhati wanapenda kuwatumia wanawake kwa tamaa zao za mwili.

Dada yangu mimi nakupenda na natamani uwe na ndoa bora na uchague mpenzi bora, mpende mpenzi wako kwa moyo wote achana na zile kauli za wanaume wote wanafana.

Muombe Mungu akupe mume bora na wewe uwe mke bora sababu mke mwenye mapenzi ya dhati huwa anabeba baraka za mafanikio ya mume wake …Tafakari mauhusiano yako yapoje ….Jarida la Bahari lina wazo bora juu yako kaa mkao wa kura ili ulisome kwa kufurahia hazina ya maarifa na Burudani.

Wakati ni sasa sio kesho acha kuwa na idadi kubwa ya wanaume, chagua mwanaume wako mmoja bora, pia achana na utamaduni wa kuchat na ma ex.wako .

Tengeneza mume wako bora achana na wanaume wadhaifu na wasio na tija kwako chagua wanaume bora kwa sifa za ndani na sio kwa ubora wa nje.

“If a girl ever steals your man, there’s no better revenge than letting her keep him. Real men…can’t be stolen.” FB_IMG_1465443306537

Credits: Benjamin James #Bahari

A word of wisdom: WHEN TO BE SILENT . . . The Bible

1. Be silent In the heat of
anger – (Prov 14:17)

2. Be silent When you don’t
have all the facts – (Prov
18:13)

3. Be silent When you
haven’t verified the story –
(Deut 17:6)

4. Be silent If your words
will offend a weaker
person – (1 Cor 8:11)

5. Be silent When it is time
to listen – (Prov 13:1)

6. Be silent When you are
tempted to make light of
holy things – (Eccl 5:2)

7. Be silent When you are
tempted to joke about
sin – (Prov 14:9)

8. Be silent If you would be
ashamed of your words
later – (Prov 8:8)

9. Be silent If your words
would convey the wrong
impression – (Prov 17:27)

10. Be silent If the issue is
none of your business –
(Prov 14:10)

11. Be silent When you are
tempted to tell an
outright lie – (Prov 4:24)

12. Be silent If your words
will damage someone
else’s reputation – (Pro
16:27)

13. Be silent If your words
will damage a friendship
– (Prov 16:28)

14. Be silent When you are
feeling critical – (James
3:9)

15. Be silent If you can’t say
it without screaming it –
(Prov 25:28)

16. Be silent If your words
will be a poor reflection
of the Lord or your
friends and family – (1 Pt
2:21-23)

17. Be silent If you may
have to eat your words
later – (Prov 18:21)

18. Be silent If you have
already said it more
than one time – (Prov
19:13)

19. Be silent When you are
tempted to flatter a
wicked person – (Prov
24:24)

20. Be silent When you are
supposed to be working
instead – (Prov 14:23)

“WHOEVER GUARDS HIS MOUTH AND TONGUE KEEPS HIS SOUL FROM TROUBLES” – (Prov 21:23).

“BE STILL, AND KNOW THAT I AM GOD” (Ps 46:10).

Source: one of my friends on Facebook

Service to others is the rent you pay for your room here on earth ~~~~~~ Muhammad Ali

Screenshot_2016-06-07-17-13-11-1

The strength of woman……

Screenshot_2016-06-06-20-49-36-1-1

Hot shot of the day

FB_IMG_1465304630400ShyRose Bhanji, looking calm and collected in her Arabic / Muslim attire….. kapendeza sanaaaaaa………… Ramadhan Kareem Muheshimiwa

Do not mix work with family!

FB_IMG_1465267345526

Source: Dr Ben Carson 

is always the woman’s fault when the man cheats!

We need to stop this nonsense that, it is always a woman’s fault that their husbands/bf cheat because of them.

A friend of mine posted a blog saying, after a woman gets married, she stops caring about herself, gains 100lbs, bluh bluh…. That’s why the husband will go look for side dishes who are slimmer etc.

What about men who look like they swallowed the biggest Abs ball when they get married?? So we are allowed to go look for 6 packed men? Let’s stop this BS that it is always the woman’s fault when the man cheats.

You can marry Miss. Universe and still cheat. Once a cheater always a cheater. Stop this nonsense of hormones. So the ones that don’t cheat are women in men’s clothing ??????   #WomenPower

Faith Mbori
Faith Mbori

My attitude today: keep your nose where it belongs!

2016-06-04 15.08.37

Matukio katika picha

FB_IMG_1465300493686Hawa Gwao (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye meza kuu kama mmoja wa majaji katika show ijulikanayo kama The West Midlands Talent show iliyopo United Kingdom FB_IMG_1465300454708Hawa pamoja na mmoja wa majaji  FB_IMG_1465300465341Hongera sana Hawa

#Hoja: ACHA KUFANYA MAMBO HAYA NA UTAFANIKIWA 100%

1. ACHA KUWA NA MARAFIKI WANOKUPOTEZEA MUDA:

Watu wengi tumekuwa na marafiki wengi sana na marafiki ni mhimu sana katika maisha yetu haya wapo wanaotufaa na wasiotufaa kuwa na marafiki wanao weza kukusaidia na kukupa hamasa ya kimaendeleo ,malengo yako na kuwa na maisha Fulani. Hivyo achana na marafiki wasio kuwa na msaada kwako.

2. ACHA KUKIMBIA MATATIZO YAKO

Waswahili wanasema kuwa “kukimbia tatizo si kutatua tatizo” Hivyo basi kama tatizo umekutananalo basi tafuta njia ya kulitatua tatizo hilo kwani matatizo hayaji kuisha katika dunia hii kama unakimbia utakimbia mangapi ? unatatizo la pesa kwanini usitafute pesa ila kama hufanyi kazi unategemea kupata pesa huwezi. Matatizo hayaepukiki komaa na ulitatue utajikuta kama uko peke yako katika hii dunia lakini kuna watu wana matatizo zaidi yako na wanahangaika kuyatatua.

3. ACHA KUJIDANGANYA MWENYEWE

Katika maisha ya sasahivi unaweza kumdanya mtu yoyote yule lakini ogopa sana kujidanganya. Vijana wengi tumekuwa tukijivuna mbele za watu kuwa tuna hili mara lile ili mradi tu tuonekane ni watu wazuri kwa watu wanao tusikiliza.

4. ACHA KUIGA MAISHA YA WATU WENGINE

Vijana wengi hili kwetu limekuwa janga kubwa sana maisha yetu yamekuwa yakuigiza sana (copy and paste) hasa hasa tunapenda kuonekana ni watu Fulani wenye maisha mazuri, hatuzijui shida ni watu wakula bata wakati si kweli. Maisha yetu yamekuwa magumu na yatakuwa magumu kwasababu ya kuiga maisha ya watu wengine ishi maisha harisi uliyonayo watu wakujua asili yako siyo kuigiza unaweza kosa kusaidiwa na watu.

5. ACHA KUKUMBUKA YALIYOPITA

Hapa kuna mambo mengi tunajifunza wengi hukumbuka yaliyopita hasa waliyo shindwa kuyafanya au yaliyowaumiza kwa kukumbuka yaliyopita haiwezi kukusaidia kwani kila tuamkapo asubuhi ni kama tumezaliwa upya na siku ni nyingine,tarehe na mambo utakayoyafanya ni mengine si sawa na jana. Waswahili wanasema “Tusahau yaliyopita tugange yajayo” hii ina maana kuwa wewe si wa kipindi kile bali ni mwingine na akili ni mpya.

6. ACHA KUOGOPA KUFANYA MAKOSA

Makosa ndiyo walimu wetu mkubwa sana katika maisha yetu na kila binadamu si mkamilifu toka uzaliwe mpaka sasa kuna makosa mengi uliyoyafanya na kupitia makosa hayo umejifunza kutorudia makosa tena na makosa hutujenga zaidi na kuwa makini zaidi kama ukifanya kosa huna haja ya kujilaum chukua muda kujilekebisha na kusonga mbele kosa lisiwe tatizo la kukukatisha tamaa.

7. ACHA KUNUNUA FURAHA

Vitu vingi tunavyo vihitaji vinagharama kubwa sana na vitu hivyo si kwamba tuna vipenda bali ni tamaa tu tuliyonayo na hiyo yote ni kuamini kuwa furaha ya maisha tutaipata huko si kweli. Mungu alitupatia furaha, na upendo bure ni vitu unavyozaliwa navyo fikiria kama vingekuwa vinauzwa wangapi? Wangapi tungekuwa hatuna furaha. Hivyo basi anza kuyafurahia maisha yako hivyo vingine vitakufuata.

8. ACHA KUSHINDANA NA MTU KIMAISHA

Acha kushindana na mtu kimaisha haitakusaidia huwezi jua yeye anafanya nini kuzipata pesa zake au mali zake na wewe unazipataje ushindani mzuri katika maisha ni ule wa kwako na mafanikio yako jiangalie kile unachokifanya na matokeo yake unapata nini? huo ndio ushindani mzuri kuliko wote sio kushindana na mtu kimaisha acha.

9. ACHA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO YASIYO SAHIHI

Katika mahusiano si kitu cha kujiingiza tu au kama unaoa si kuoa tu kwasabu Fulani kaoa basi na mimi nioe, si kudai kuwa nimechoka kufua ngoja nioe sasa ndiyo maana karne hii inaongoza kwa wanandoa kuachana na ndoa za utotoni kwasababu watu hawajipangi ni kuiga tu. Mahusiano au ndoa ni kitu kikubwa sana na kama umempenda mtu onyesha kuwa unampenda kweli mtangulize mbele yako kuwa ndiyo kila kitu kwako/ kila kitu kinaenda kwa ajiri yake. Kama unaingia katika mahusiano mheshimu mwenzako na kumpenda mpe nafasi kubwa katika maisha yako.

10. ACHA KUJILAUMU

Kuacha kujilaumu ni njia mojawapo ya kufanikiwa katiaka maisha yako unapo kosea amini kuwa wewe si mkamilifu na hakuna binadamu aliyekamilika jipange songa mbele. Wagunduzi wa vifaa mbalimbali vinavyotumika kama vya umeme na vinginevyo si kwamba hawa kufanya makosa walikosea sana mpaka kutoa kitu sahihi .

11. ACHA KUONGELEA YAWATU FULANI

Kuzungumzia maisha ya mtu Fulani haikusaidii ni kupoteza muda tu kwanini usiwaze maisha yako unatakiwa kufika wapi na ufanye nini kuishi maisha mazuri unakaa na kuanza kuzungumzia mtu Fulani yupo hivi mara hivi wakati huo huyo mtu unaemsema yeye yupo kazini we upo kijiweni mtalingana kweli? Acha kuzungumzia maisha ya watu fanya yako ufurahie maisha.

By Mike Mwakatundu MP2020

Source: Change Tanzania

You can’t stop water from flowing!

2016-06-07 07.03.33

A word of wisdom

Hold on to your faith even when things look hopeless. Faith is the substance of the things we hope for, and when you have God in your life, you have hope no matter what the circumstances look like.~~~~~~~ Victoria Osteen

Ramadhan Mubarak

IMG-20160605-WA0002jamani si ndo ule umeandama eeh! Haya nawatakieni Ramadhan njema wapendwa wasomaji wangu, ndugu, jamaa, na marafiki. Mtukumbuke katika dua zenu FB_IMG_1465210863756Happy holy month to all Muslims around the world ?

Wapo watu wenye tabia za Chatu huyu

Ilikuwa kawaida yake kulala na nyoka wake, na haya ndiyo yaliyomkuta. FB_IMG_1465163970073Hii ni hadithi ya kweli kuhusu mwanamke aliyekuwa na nyoka wake aina ya chatu aliyempenda sana. Nyoka alikuwa na urefu wa mita 4, aliishi naye kwa muda mrefu na siku zote nyoka yule alionekana mwenye afya. Hata hivyo, nyoka alianza kukosa hamu ya kula kwa wiki kadhaa jambo lililomnyima raha mama yule kwani alihisi nyoka wake ni mgonjwa. Mama alijaribu kumpa kila kitu alichoweza ambacho nyoka wangependa kula lakini haikusaidia kitu, mama yule alikata tamaa na aliumia zaidi kwakuwa alimpenda sana nyoka wake. Hatimaye mama yule aliamua kumpeleka nyoka wake kwa daktari wa mifugo. Daktari alimsikiliza yule mama kwa makini kisha akamuuliza , ” Je, unalala na nyoka wako wakati wa usiku? anapenda kulala karibu zaidi na wewe na kujipimisha urefu wake na wako? “

Mama kwa matumaini makubwa alisema, “Ndiyo! Ndiyo! anafanya hivyo kila siku na inanipa huzuni kwa sababu nahisi kuna kitu anatamani kuniambia lakini hawezi na Mimi pia nashindwa kumuelewa hivyo nakosa namna ya kumsaidia ili ajisikie vizuri kama siku zote “

Daktari akampa jibu la kushtusha moyo ” Mama, chatu wako si mgonjwa ; … “Ndiyo, chatu hakuwa mgonjwa, amekuwa katika maandalizi ya kumla mama yule. Daktari akaendelea, “Kila wakati anataka kukaa karibu na wewe, kujikunjakunja mwilini mwako na kukutambaa kila muda, lengo lake ni kupima ukubwa wako na kuangalia namna gani utakuwa mzuri mlo wake. anajilinganisha kujua jinsi gani utawa mlo mkubwa kwake hivyo anajipanga kwa mashambulizi. Na ndio maana hataki kula sasa ili kulipa tumbo lake nafasi ya kutosha kwaajili yako pindi atakapokugeuza kitoweo chake “.

FUNDISHOWatu wako wa karibu zaidi unaowaamini, wapole na wanaoonyesha kukupenda wanaweza kuwa wabaya zaidi kwako. Upendo wa dhati na dhamira nzuri haitokani na namna watu wanavyo Kukumbatia na kukuchekea. Unafiki huambatana na Upendo wa kujilazimisha. Usiogope mashambulizi yanayopangwa na maadui zako juu yako Bali ogopa rafiki mnafiki anayekukumbatia na kukuchekea huku anakumwagia sumu kali. Adui wa MTU ni wa nyumbani mwake.

Mbarikiwe.

Source: Unknown 

My attitude today: all women be like

2016-06-05 20.16.46

Asie na kasoro ni Mungu pekee -Dina Marios

Alikuwepo mfalme mmoja ambaye yeye alikuwa na tatizo katika jicho lake moja la kushoto na mguu mmoja alikuwa hawezi kusimama akiwa ameunyoosha. Jicho la kushoto limefumba halioni. Siku moja akahitaji wataalamu wa kuchora wa mchore kwa umahiri mkubwa picha yake ipendeze iwe na mvuto wa ajabu pamoja na madhaifu yake.

Wachoraji mbali mbali walijitahidi kufanya walichoweza kuhakikisha hili linawezekana maana waliahidiwa dau kubwa kutoka kwa mfalme. Walichora lakini bado ule udhaifu ulionekana wazi na hazikuwa na mvuto kama yeye alivyotaka.

Basi alitokea kijana mmoja ambaye yeye alimchora mfalme kama “muwindaji flani ambaye amefumba jicho moja na amekunja mguu mmoja akilenga shabaha kukipata kile anachokiwinda. Mfalme alifurahishwa sana na picha ile na kijana akashinda.

Katika maisha ni vema tujitahidi kuficha madhaifu ya wenzetu na kuchochea yale wanayoyaweza katika maisha ili kila mtu awe na furaha siku zote bila kujali muonekano na mapungufu yake.

Muda mwingi tunanyoosha vidole kudhihaki na kutangaza mapungufu ya wenzetu, maumbile n.k Tunajifunza kuwapenda watu ndugu zetu, jamaa, wapenzi, marafiki kwa kuyapa kipaumbele yale mazuri waliyonayo ukizitafuta kasoro za mwanadamu hutazikosa ni nyingi kweli na asie na kasoro ni Mungu pekee. FB_IMG_1465217175783Dina Marios!

Blog