Miaka mitatu nyuma watanzania wengi walijikuta wakiwa katika hali ya kukata tamaa baada ya mifumo mingi ya serikali na uendeshaji wake kutokidhi mahitaji ya watanzania ki uchumi, siasa na jamii.
Mimi nilikuwa mmoja wapo niliyekuwa naumia sana nilipokuwa nikipata taarifa za utendaji wa serikali na vitengo vyake kama polisi, mahakama, ardhi, afya, elimu, uchumi na mbaya zaidi ni taarifa za ufisadi wa nchi. Ilifika mahala ufisadi ukawa ni wimbo ulioimbwa na kila mwananchi kwa kusifia au kulalamikiwa.
kusifika kwa ufisadi na rushwa kulianza kuota mizizi kwa watanzania hasa vijana waliokuwa wakichipukia katika kazi na kupewa vitengo either kwa kushikwa mkono na mnene flani au kwa juhudi zake. Vijana tulikuwa msemo; Ukipata kitengo serikalini itumie vilivyo kutusua maana nchi haina mwenyewe. Vijana wengi walikosa uzalendo na uchungu wa nchi kutokana na tabia waliyoikuta kutoka kwa viongozi wao ambao walikuwa wakiitafuna nchi bila huruma. Vijana walifanya kufuru kwa kujenga majumba makubwa na magari ya kifahari ndani ya mda mfupi (Miezi 6) akiwa katika kitengo, Tabia hii ilisababishwa na wanasiasa waliotumia pesa nyingi kupata madaraka na uongozi na pindi walipopata uongozi waliwashawishi watendaji kufanya mambo yasiyokuwa ya kizalendo kwa nchi ili kurudisha garama na kupata faida zaidi na hata mtaji wa kuwekeza katika uchaguzi ujao.
Jamii zetu ziliathirika sana na tabia hii hasa vijana wetu wa kike maana ilifika mahala vijana wa kike wakaishi maisha ya kuigiza badala ya kuishi ualisia wao, wengi wao waliishi maisha ya kifahari pasipo kufanya kazi, mapenzi ya kweli yakawa ni historia, ndoa zikawa ni kwaajili ya kutoa nuksi kisha zinavunjika, kubeba mimba na kupata mtoto mmoja ikawa ni fashion na swaga za mabinti. Vijana wengi wa kiume mijini nao hawakupenda kufanya kazi za kuumiza akili, hawakupenda kufanya kazi kwa utaratibu na hawakuwa na uvumilivu katika maisha. Kila kijana alitamani akishapata kazi tu aweze kumikili gari, nyumba na mtoto mkali baada ya mda mfupi maana kwa kipindi hicho pesa iliweza kununua hadi mapenzi kutoka kwa baadhi ya mabinti waliojiona wazuri saana. Hivyo vijana wengi wakajiingiza katika ajira za kisanii na zingine zisizo halali kama utapeli, udalali waliolazimisha mifumuko ya bei, wauza poda, wafanyakazi hewa, mafisadi serikalini na wengine wakenda kwa wanganga na kutoa kafara za kutisha ili tu apate pesa ya kutamba na kufanya kufuru mitaani.
Siasa za nchi nazo zilibadilika sana kwa viongozi wetu ndani ya miaka 10 iliyopita. Viongozi walituaminisha kuwa kama huna cash basi siasa haikufai na hata wapiga kura tuliaminishwa kuwa mpigie kura anayekupa cash yaani kura zetu tuliziuza kwa pesa na zawadi mbalimbali. Siasa zikawa ni za maji taka kila mwanasiasa anatafuta pesa na umaarufu wa kuhonga ili aendelee kuchaguliwa. Wananchi hatukuona tena umuhimu wa siasa ikiwa viongozi tunao wachagua hawakidhi wala kutekeleza ahadi zao kwa jamii na wanasiasa safi walinyimwa kura kwa sababu ya kukosa cash na badala yake wafanya biashara na matajiri wa mitaa na majimbo ndio walioshindana kununua kura. Hali hii ilififisha dhana ya uchaguzi na demokrasia katika siasa.
Uchumi wa nchi ndani ya miaka 10 nao uli athirika kutokana na tabia ya ufisadi. Nchi ilisomeka kukua ki uchumi katika makaratasi lakini wananchi wengi walikuwa ni mafukara mifukoni waliokuwa wakiishi kwa mlo mmoja kwa siku. Vyanzo vikuu vya uchumi vili binafsishwa na kumilikiwa na wafanyabiashara na wanasiasa wachache(20%) waliomiliki sehemu kubwa ya utajiri wa nchi(80%) wakati wananchi wengi masikini (80%) walimiliki sehemu ndogo ya utajiri(20%). Maamuzi mengi ya uchumi wa nchi yaliumiza sana wananchi masikini mfano bei za bidhaa muhimu na garama za usafirishaji wake, viwango vikubwa vya kodi na kodi zisizokuwa na ulazima, maamuzi ya kuagiza bidhaa au kutengeneza bidhaa pamoja maamuzi ya kuacha sekta binafsi kutawala uchumi. Ndani ya miaka 10 tumeona hazina za nchi zikiachiwa huru kwa wageni kuvunwa kwa malipo madogo serikalini na viongozi wachache walioingia mikataba mibovu pasipo kuweka mbele uzalendo na maslahi ya nchi. Tulipofikia ilikuwa ni Hatariii kwa vizazi vijavyo..
Nakumbuka nimeanza kutambua haki yangu ya kupiga kura mwaka 2000 nilipokuwa kidato cha kwanza na nilishiriki nikiwa na uwezo wa kupambanua sera, ahadi na siasa za wagombea. Hivyo nilishiriki mwaka 2000, 2005, 2010 na 2015. Takribani awamu tatu za utawala nazishuhudia mpaka sasa.
Wanasiasa wengi waligeuza siasa kuwa ni uwanja wa kushawishi kwa kusema uongo wakati wakiomba kura, kuna wakati ilijengeka kuwa ili upate uongozi basi ni lazima uwe na pesa au uwe na uwezo wa kuunda uongo na kuupamba ukiwa unaomba kura.
Uchaguzi ulioisha 2015 umeshitua fikra zangu na kasumba niliyokuwa nayo ya muda mrefu ya kuamini kuwa siasa ni uhodari wa kusema uongo. Upepo ulikuwa ukibadilika kila wakati hadi ikafika sehemu wanasiasa wakakubali ukweli utawale katika hoja zao na ahadi zao.
Nimekuwa nikimsikiliza na kufuatilia kauli za Mh. JPM tangu alivyokuwa akijinadi na kuomba kura hadi alipoanza kazi ya uraisi na nimegundua kuwa Mwisho wa Uongozi na Utendaji wa Mazoea umefika. Nampongeza sana Mh. JPM kwa kuongoza kwa kufuata kauli zake toka alipokuwa akijinadi. Maana dhamira yake na kauli zake hazijabadilika tangu alivyoomba kura hadi sasa.
Hii inaashiria nini? Inashiria kuwa huko tuendako kuna majipu ya mazoea yatatumbuliwa sana. Ni vizuri watanzania tukaanza kuelewa maona ya Raisi hasa kwa kubadilika katika uongozi na utendaji unapokuwa unapewa dhamana au kazi katika idara za serikali. Kufanya kazi kwa mazoea pasipo kujali maslahi ya Taifa na wanyonge, kufanya kazi pasipo kufuata taratibu na sheria za nchi, kufanya kazi kwa kutumia cheo vibaya ni hatari kwa zama hizi za JPM.
Ni vizuri tukajitathmini je, mazoea tuliyonayo yanafaa kwa zama hizi za HAPA KAZI TU? Kama hazifai basi badili gear angani na ucheze ngoma iliyopo.
In the proposed state budget for 2016, the Norwegian government has suggested to phase out and eventually replace the Norwegian Quota Scheme. Therefore, we regret to announce that there will be no new admissions for the Quota Scheme for the 2016/17 academic year.
Brief description: The Norwegian Government offer scholarship funds for the Quota Scholarship scheme for Bachelor’s, Master’s and PhD Students from Developing Countries at universities and university colleges in Norway 2015/2016
Accepted Subject Areas: Students usually apply for degree programmes that serve as a continuation of their studies in their home country or for courses which can be a joint part of a degree programme in their home country (joint degree or sandwich programmes). Most of the programmes offered are at Master’s or PhD level, but the Quota Scheme also offers certain Bachelor’s study programmes.
About Scholarship: The main objective of the Quota Scheme is to contribute to capacity building through education that will benefit the home country of the students when they return. The Scheme is also intended to strengthen relations between Norway and the selected countries and thus contribute to internationalization at Norwegian institutions of higher education. Most universities and university colleges in Norway participate in the Quota scheme. The institutions involved are allocated a certain number of students under the programme each year. Most of the programmes offered are at Master’s or PhD level, but the Quota Scheme also offers certain Bachelor’s study programmes
Hongera sana Hellen Dausen tunajivunia kuwa na vijana kama wewe katika taifa letu! Tunakutakia mafanikio mema zaidi, na uzidi peperusha bendera yetu vyema!
Wishing you all a very Happy Memorial Day Wekend! Enjoy and be thankful ❤ …… ngoja niwaache leo na hii kinda old school toka kwa our Queen Lady JayDee just a #FBF
Jumaa Kareem to all my Muslim readers, friends, and family!….. Muwe na siku njema ya maandalizi ya Sabato kwa Wasabato wenzangu and Happy Sabbath to you all…….. Tumsifu Yesu Kristo ? ❤❕ ❤❕❤❕ sorround yourself with ❤
Wafanyabiashara ni wadau muhimu sana wa amani na ustawi wa nchi. Wao ndio chachu kuu ya ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja na mwananchi mmoja mmoja. Nchi yoyote dunia ingependa iwe na wafanyabiashara wazalendo au wafanyabiashara wenye kufuata taratibu na sheria za biashara zilizowekwa ili nchi hiyo iweze kufaidika na biashara husika.
Mfanyabiashara mzalendo sio lazima awe mzawa ila ni yeyote yule mwenye kujali mahala anapofanyia biashara yake kwa kufuata taratibu na sheria za nchi hasa ya kulipa KODI. KODI ndiyo inayo endesha shuguli zote za serikali ikiwa ni mapoja na kuimarisha huduma bora za kijamii na mazingira mazuri ya uchumi kama vile miundombinu, mawasiliano, ulinzi na usalama, huduma za kisheria, kusimamia ushindani wa kibiashara, utawala bora na mengine mengi yanayogusa maslahi ya wafanyabiashara.
Lengo kubwa la biashara ni kupata faida na kuendelea kupata faida miaka ijayo, biashara yoyote ile ni lazima ilipe (ilete faida) kama utaifanya wakati sahihi, mahala sahihi na kwa wateja sahihi na ndio maana imeitwa biashara. Lakini wafanya biashara wengi wamekuwa na tabia mbili mbaya sana kwa maendeleo ya Taifa letu. Kwanza wamekuwa na mazoea na tabia ya kukwepa kodi kwa kufanya kila linalowezekana ili wasilipe KODI kwa lengo la kupata faida maradufu. Hii tabia haikubaliki jamani maana wateja wenu ambao ni wananchi wamekuwa wakikubaliana na bei zenu wakiwa na imaninkuwa kuna sehemu fulani inakwenda katika serikali yao kama kodi kwaajili ya kuendeleza nchi lakini wafanyabiashara hawa wasiokuwa wazalendo wamekuwa wakichukua mapato yote hadi yale ya serikali (KODI). Hii tabia inaleta uchonganishi kati ya serikali na wananchi wake ambayo ni hatari sana na haikubali.
Pili, wafanyabiashara wamekuwa na tabia nyingine ya kulalamika kwa matatizo wanayoyapata katika biashara zao bila kuangalia chanzo. Lawama nyingi zimekuwa zikielekezwa kwa wasimamizi wa biashara na serikali inapotokea mazingira yao ya kufanyia biashara hayapo vizuri, lakini ukichunguza kwa undani utakuta matatizo haya yamesababishwa na baadhi ya wafanyabiashara wenyewe kwa kukwepa kulipa KODI ambayo ingeweza kuwaondolea matatizo yao. Nakubali sio matatizo yote yanasababishwa na wao lakini mengi wao ndio chanzo.
Nawasihii mbadilike na mjifunze kuwa wazalendo na wenye kufuata taratibu na sheria. BADILIKENI…
Niwakumbushe wafanya biashara kuwa Serikali ya sasa sio ile ya miaka iliyopita, Serikali ya sasa ni ya KAZI NA KODI TU. Mh. Raisi ana maono ya kuifanya Nchi kujitegemea yenyewe kwa kuendesha serikali na kuleta maendeleo kwa fedha zake bila kutegemea misaada, haya ni maono mazuri na ya kuunga mkono. Tufike mahala hata wewe mwenyenyumba ya kupangisha ulipe kodi kwa serikali baada ya kupokea kodi kutoka kwa wapangaji kama alivyoshauri mtaalam wa uchumu Valentine Vedasto alipokuwa anahojiwa na BBC.
Walioteuliwa kumsaidia Mh. Raisi (Dr. JPM) wafanye hiyo kazi kwa spirit kama ya Raisi, wasimuangushe maana tuna imani na maono yake.
Lovely Designer Mariam Beuzeidenhout Ishtiyaq of Fashionadoz, daughter of International designer Linda Beuzeidenhout (LB) of Atlanta, Georgia. Looking beautiful with her LB dress during her 8th grade (Elementary studies) graduation day! Mariam is already a well known fashion designer for baby dolls……..You can see some of her works and runways fashion show that she has participated through her Instagram page goes by Fashiondoz……..
Mariam has just finished her Elementary studies and now she is about to join high school this coming Fall semester! Its my honor to say congratulations Mariam! You did it! God bless you more and more!
Awwwwhhhh My third born FASHION DESIGNER @fashionadoz Is Graduating today from Elementary Studies. Ooo she just sent me this photo of her Making a grand entrance in her LB at her school. Awwwh photo taken by one of her teachers. Awww we are all getting ready to go see her walk awww I know I will cry today I know I will. Oooo jamani Maryam Leo anamaliza masomo ya msingi siamini machozi yashaanza kunitoka.
Hongera sana Linda na familia yako yote! Mungu azidi mlinda, amuongoze, na azidi kusimama katika nyia aliyopo sasa ??
Hatimaye a long awaited moment for many of us has come! Kwakweli swala hili lilipoanza nilihuzunishwa sana lakini sikushangazwa nalo kama wengine kwani nimeshaona matukio mengi ya hawa wanaume wanaotafuta power ya kuaminika katika jamii au katika familia wanafanya mambo ya ajabu including mauwaji na kama watu sio makini they may get away with it!. Bill Cosby hivi karibuni mambo yalikuwa magumu akawekwa underoath kwa kwenye case ya mwanamke mmoja (back in 2005) ambayo hakawa hana ujanja but to admit to drug women for sex! #SMH
https://youtu.be/lo0EBl9f9us
Kumbuka zaidi ya wanawake 50 walijitokeza mmoja baada ya mwingine na ku demand justice lakini statue of limitation ikawa inawabana! Sasa wengine wakajitokea ambao walikuwa ni underage teenagers some of them walikuwa waki act kwenye ile show ya The Bill Cosby show!……… Wazazi kueni karibu na watoto wenu ili waweze kukuelezeeni mambo yote bila uwoga wala aibu! Usiamini mtu yoyote!…….. Halafu haya maswala ya sexual or any kind of abuse mimi nafikiri yanachangiwa sana na wanawake wanaopenda “fake na cheap” life! Hawa watu ndo wana pretend everything is good nakuwapa hawa wanaume stupid force testimony about them ili tu wasaidiwe kitu fulani au ku maintain lifestyle fulani! Nimeshuhudia na wala sito ona aibu kusema! Hii tabia ndio inafanya hawa wanaume waendelee ku abuse wanawake na kuwafanya washindwe sema kwenye public kwasababu kuna stupid women somewhere wako radhi kutumika ili kuwafichia hawa wanaume mambo yao. Tena watatumia hela zao na power walio nayo kum victimize more the victim (s)! Nashukuru kuwa kuna wanaume kama President Obama ambao wako teyari kusimamia haki na ulinzi wa wanawake! Msikilize ?
Its so sad as the world was forced to believe this man is an icon when comes to “family hood” as he was a family man, husband and father figure. Kumbe yeye ndio abuser wakutupwa! Wanasema kama akiwa convicted ataenda jela kwa miaka zaidi ya 30! Sasa hivi anamiaka 78 inamaana atatoka akiwa na miaka 108! Judge aliyepangiwa hii case ni mwana mama can’t wait to see what will happen!……….? Sikiliza zaidi kuhusu hili sakata ?
Hongera sana Mtani wangu Muheshimiwa Zitto Kabwe! Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Haya wadada wa mujini heshima na itifaki lazima mzingatie ee!………. Halafu mmeona alivyo mzuri? Sasa wee mtani wangu, kwani hata zile tamthilia za “Bongo movies” huwa huwangaliagi?! Siunaonaga wenzako wanapiga magoti au hii ni kibongo bongo? Mwe! Wee Muha acha vituko ?? Hongereni sana. Tunawatakia maisha mema, ndoa njema, na mpendane milele zote.