Hizi picha nimetumiwa sijapewa maelezo yoyote zaidi ya bibi harusi anaitwa Nuru. Lakini naona kama hili ni kanisa la Wasabato la Utegi,Rorya. Naomba tu niwape pongezi na kuziwakilisha picha kama zilivyo:- Hongera sana Nuru na mume mwema kwa kufunga pingu za maisha. Nawatakieni maisha marefu yaliyojaa upendo wa dhati na furaha ya kweli! Mkabarikiwe sana, mdumu katika Bwana! mlipendeza mno Nimekumbuka kitu! Nuru aliishi nyumbani kwetu KekoJuu wakati anasoma chuo lakini mimi sikubahatika kumuona! ……….. kwa mara nyingine, hongereni sana!
Blessing na nduguze
Blessing akifurahia weekend na nduguze huko KekoJuu ……hapa akiwa na cousin-sister wake Rhoda Igogo……… Btw, Blessing naye jina lake lingine ni Rhoda. Wamepewa jina la marehemu bibi mzaa baba ?pendeza sana mdogo wake mimi hapa. Ubarikiwe kwa kwenda kusalimia ndugu zako mmependeza sana. Ila sasa hapa sijui kama huyu ni Oliver au Mage ?? mmekuwa sana nashindwa watofautisha ? jamani Blessing si kwa jicho hilo ati ?? huyo aliyetizamwa lazima aweweseke si mchezo ?? halafu hiyo ‘cut walk’ ya nguvu sana ?? haya be blessed as your name ❤
A word of wisdom
So true! Katika hii dunia kama bado ungali unaishi usije hata siku moja ukamdharau binadamu mwenzio! Kama unataka mfanyie dharau na kejeli zote MAITI kwani haito badilisha kitu aliye kufa amekufa kazi yake na mambo yake yote yamemalizika! Lakini mwanadamu mwenye pumzi ya uhai si mwenzako kwani hakuna hajuae ya kesho! “Be nice to the nerd, you might end up working for them”!! Actually most nerds tend to be very creative!
Tamu Flavors
My wifi is cuter than yours ? my darling wifi looking good with her nephew. The Delaware people, love it!……….btw nawaombeni to LIKE her Facebook page ya Tamu flavors. Yeye anafanya biashara ya catering ya African food. Anapendelea kuviita “Authentic Kenyan Dishes”. Mlioko maeneo ya Delaware basi nakuomba majaribu kula vyakula vyake. Mtashuhudia wenyewe jinsi vilivyo vitamu. Asante sana
Things come with title “babu / baba”
yap! Ukitaka title kama baba / kaka/ babu / mama n.k lazima ukubali na mambo yote yanayo kuja nayo. Wahenga wanasema “ukipenda boga sharti upende na uwa lake”! …….. Nakumbuka Latoya Jackson (dada yake na marehemu Michael Jackson) alitaka ku adopt mtoto. Wakampa test ya ku babysit watoto wawili (2 babies) kwa masaa 12 ili kujua kama kweli yupo teyari kuwa mama. Ndani ya masaa mawili akasema she is surely not ready ??? akasema its too much work she can’t do it ?? (tazama video ?)…………….. (Pichani ni babu na wajukuu zake pamoja na mwanae wote wanataka kukaa na babu )
??? hapa kavalishwa kofia na Blessing lol! Umeneja mwisho getini nyumbani ni baba / babu tuu ??? hapa na mjukuu wajina wake, ni mtoto wa mdogo wangu. Mdogo wangu alikuwa ananyonya kidole sana. Amenyonya mpaka anamiaka karibia 8 ndo akaacha. Naona mtoto wake naye anatabia hiyo ?? I hope itakwisha soon
Ujumbe: respect wazazi wetu haswa single parents. Wahenga walisema “kulea mimba si kazi kazi kulea mwana”! I did it one time, I’m done with it! Its time to do me ??
R.I.P Mr Violence!
Kwakweli wanawake wenzangu acheni kuishi maisha ya kunyayasika si vizuri kiafya, kiakili, kimwili, wala kiroho!………… Yani mimi naona nimekuwa muoga hata wa kuongea na mtu mwenye dalili za unyanyasaji, roho mbaya ya kikatili, au mnafaiki! Siwataki hao watu anywhere close to me!! It’s 21st century say #R.I.PMr.Violence….!
#TBT
It’s #TBT na leo I’m throwing back my darling daughter akiwa na miaka sita (6 yrs old) mwaka #2000 kwenye harusi ya kaka yangu. Yeye alikuwa mmoja wa flower girls. Harusi ilifungwa #TemekeSDAChurch na marehemu Pastor Joshua Onyango. Sherehe ilifanyika #PTAHallSabaSaba. Hiyo nyingine ni mwaka huu siku birthday yake 04/02/2016 kama ulipitwa na post hiyo bonyeza hapa mwanangu (kulia) na mdogo wake bibi harusi (kushoto). ?
LB: Designer of the year 2016 acceptance speech!
LB inaendelea kunguruma kwa nguvu sana ndani ya jiji la Atlanta, Georgia! Wiki iliyopita alitunikiwa kuwa Mwanamitindo wa Mwaka 2016 kutoka kwa Black Women In Jazz & The Arts Awards Association yenye makao makuu yake ndani ya Georgia State. Ms. LB aliongea kwa kuelezea kuwa mapenzi yake na mambo ya fashion yametoka kwa marehemu mama yake mzazi. Pia kipaji chake cha ubunifu wa nguo kilionekana na mumewe Mr. Mali Kimesera! Atoa asante nyingi sana kwa mumewe. Wakati huo huo alitoa shukran zake za dhati kwa muanzilishi wa Black Women In Jazz pamoja na msemaji wa shirika hilo kwa kutambua na kuthamimi kazi yake mpaka kuona kuwa anafaa kupokea tunzo hiyo. Ukumbuke kuwa tunzo hiyo wanapokea watu maarufu sana hivyo kwa LB kutunukiwa tunzo hiyo si tuu fahari kwake bali kwetu sisi wote Watanzania kwani hii inazidi kuikuza jina la Tanzania nje ya inchi! (Tafadhali tazama video).
Mimi binafsi kama Mtanzania mwana diaspora na rafiki wa Linda, nampongeza sana tena sana! Namuombea mafanikio makubwa zaidi ya haya. Hivi nitaanzaje kuacha kumshukuru mume mwema! Mungu akubariki sana shemeji yetu wa ukweli. Uzidi kupenda dada yetu naye aka kutangaze dunia nzima ikujue wewe mume mwema! ……. Kama ulipitwa na hii post kuhusu Hottest And Best Couple Of The Year 2016 bonyeza hapa Kwa mara nyingine tena hongera sana LB! Well deserved!
Bonus video of LB
Hot shot of the day
I love this pic! Love the dress, the shoes, em legs Omg! Too cute! Pendeza sana ❤❤❤
The Amish
Hapa Marekani kuna watu wajulikanao kama Waamish. Hawa watu hawatumii umeme, hawa endeshi magari (wanatumia puna na farasi kama usafiri), hawaendi shule hizi za Kawaida kwani wana shule zao wenyewe ndani ya vijiji vyao. Wala hawatumii technology yoyote ile ya kisasa, na vyakula vyao ni organic tuu ambavyo wanalima wao wenyewe. Nguo wanazo vaa hushona wao wenyewe ambazo ni style zile za kizamani sana na huwa hazibani yani ni kubwa kubwa.
Wanatabia ya kuishi nje ya mji kwa mfumo wa vijiji. Familia zao huwa hazitengani kwani nyumba zao huwa ndefu kama treni! Kila mtoto wa kiume akiowa anaongeza chumba chake kwenye mstari. Nilipo kuwa naishi Wichita nilibaatika kuwatembelea kwenye makazi yao. Kwakweli unaweza usiamini kuwa ni Marekani. Chakushangaza ni kuona Wamarekani wakiwashangaa Waafrika ambao bado wanaishi katika mazingira kama haya wakati hapa kwao pia wapo!!
Anyway, hizi picha ni za rafiki yangu Janet Kisyombe. Yeye na ndugu zake walibahatika kuwatembelea hao Waamish siku chache zilizopita. Ni watu ambao ukikaa nao utabaki unashangaa sana. Kama mtu anatumia moto wa kuni kufanya nyumba iwe na joto wakati wa baridi ambapo angeweza kuweka umeme na kurahisisha kila kitu! Asante sana Janet kwa picha. Ubarikiwe
Father and daughter moment
Nimependa sana hizi picha za ‘Fathers and daughters moments’ kushoto ni Mr. Obama na binti yake Malia na kulia ni Mr. Kimesera na binti yake Brenda. Wamependeza sana Wow! too cute! I support Linda’s msg ☝ Yes, It does! wabarikiwe wababa wote!
Hongera sana LB
Many congratulations to Missy LB for being honored the 2016 Fashion Design Award by the Black Women In Jazz & The Arts Awards 2016. Personally I am truly proud of you keep representing our country so wel!
Tukio hili la kufurahisha lili tokea mnamo tarehe April 10, 2016, katika hotel ya Marriott mjini Atlanta, Georgia
Baadhi ya watu maarufu ambao walitunukiwa tunzo hiyo siku hiyo ni Legend Ms. Cicely Tyson na Melba Joyce na wengine wengi!
Missy LB akiwa anaingia ukumbini huku akiwa amevalia vazi aliyo buni na kushona yeye mwenyewe Pendeza sana LB alifurahiya tuzo na binti yake Brenda, wote wakiwa wamevalia mavazi ya LBmlipendeza mno! Kwa mara nyingine tena hongera sana Linda Bezuidenhout. Nakutakia mafanikio makubwa zaidi ya haya ?
“changamoto nyingi hapa duniani ukigeuza upande wa pili utagundua ni fursa” -Dina Marios
Baba mmoja alikuwa amekaa kwenye kiti chake chini ya mti anasoma gazeti. Pembeni yake alikuwepo mtoto wa miaka 6 ambaye alikuwa akimsonga kwa maana nae alikuwa anataka kuangalia kilichomo ndani ya gazeti.
Baba huyu ili kuondoa usumbufu akaona ni vema achane ukurasa mmoja ili ampatie mwanae. Ukurasa huu ulikuwa na ramani ya dunia, akamuonesha “unaiona hii ramani eh? baba yake akaichana ile ramani vipande vidogo vidogo kama kumi na tano. Akamwambia mwanangu nenda ukavipange hivi vikaratasi mpaka iwe ramani kama ilivyokuwa, ntakupa booonge la zawadi. Hii yote ikiwa ni katika kuondoa usumbufu.
Mtoto akaenda kujifungia baada ya dakika chache akarudi akiwa amevipanga kwa usahihi kabisa. Kwamshangao haaaaaa!! Umewezaje kufanya haraka hivyo? mtoto akajibu nyuma ya vikaratsi hivi ilikuwepo picha ya sura ya mtu hivyo nilivipanga kwa kukufuta sura hiyo.
Oooh! Unajua maishani suala si kukutana na changamoto bali ni jinsi gani unazichukulia changamoto hizo. Ukikutana na changamoto yoyote tuliza akili na utapata mlango wa kutokea changamoto nyingi hapa duniani ukigeuza upande wa pili utagundua ni FURSA. Fanya hivyo utashanga mambo yanavyokuwa rahisi kwako. Ila ukiwa kipofu wa kuitazama ile changamoto kwa hisia za itakuwaje utabaki hapo hapo.
Good Morning!
Father and son moment
Ain’t they cute! Wamependeza sana, great picture and happy belated birthday Dr. Martin Sarungi. Live long!
Hot shot of the day
I loved this! Cute! Cute! Mr and Mrs Dangote na Queen Latifah………… Pendeza sana. beautiful!
“Sijawahi kuishi kwa kumtegemea mtu ila ninaishi kwa kumtegemea Mungu”Le mutuz
Motherhood
I love this pic. Zari na wanae wamependeza sana. Kuwa mama ni kazi ya kishujaa sana, nikazi ambayo unatakiwa ujitolee kwa asilimia zote si tu kifedha bali pia kwa matendo yako, na kwa mawazo yako! Wabarikiwe wamama wote!
Our humble beggings!
Sikutegemea kuweka hapa hii picha siku ya leo. Lakini nimeona moyo wangu umenisukuma kuweka basi ngoja nifanye kile kitu roho napenda! Hii picha tulipigia tukiwa kijijini Utegi, Rorya, Mara mwaka 1987. Tulienda kusherekea siku kuu ya Christmas. Katika hii picha kuna watu wawili ambao hawapo nasi tena.
(1) aliyevaa sandals nyeupe. Yeye alikuwa mama yangu mkubwa mke wa marehemu baba yangu mkubwa mzee alijulikana kama Mama January
(2) Shangazi yangu kipenzi cha roho yangu. Theresia Obuoro Igogo. Ambaye amekaa karibu na mimi. Alikuwa msichana mmoja tu kwenye tumbo la bibi yangu mzaa baba. Yeye ndo mwanangu amepewa jina lake (Theresia a.k.a Teddy) in honoring of her. Ipo siku nitamuongelea kwa kirefu zaidi kwani yeye ndio chanzo cha mibaraka yote ambayo watu wanaiyona katika familia yetu!!
Wengine ni:- mama yangu mzazi?
dada yangu ambaye ninamfuata ? mdogo wangu anaye nifuata kwa mara ya pili na mimi mwenyewe ? ??? what a massive #ThrowBackSunday..! Hilo “banda” la udongo kwa upande wa kushoto lilikuwa ndiyo jiko la marehemu bibi yetu nyakati hizo (baadaye alijengewa lingine). Na kwa upande wa kulia ilikuwa ni sehemu wanalala mbuzi.
Everyone starts from somewhere! Hakuna kitu kinacho onekana hapa duniani ambacho hakina mwanzo wake au chanzo chake! #TheRoots Na huwa nikikumbuka tulipo toka then unakuta mtu anataka kuingilia mambo ya familia usizozijua chanzo chake!! I swear, naweza toa mtu ng’eo ya macho! Kama wewe hukuwepo nasi nyakati hizi then keep your nose where it belongs!!
Nilimtumia mdogo wangu na baba yangu hii picha. Wakashangaa sana. Mdogo wangu alikuwa hajawahi kuona hii picha vile vile maisha yao walivyo kuwa ni tofauti na sisi tulivyo kuwa wadogo. Hivyo hana kumbukumbu ya maisha haya ya hali ya chini. Hapo kwenye picha alikuwa na miaka mitatu (3yrs). Basi hivi ndivyo alivyo sema ?
Na baba yangu yeye nilimtumia muda kidogo na hivi ndivyo alivyo sema ? (Samahani kwa some typos) Anyway! That’s our humble beggings. I’m glad nime share nanyi kidogo ?
A word of Wisdom
Yes! Only God sits that High! Kuna “watu” wanajiona wao ni Mungu! Yani bila uwepo wao kwenye maisha yako au kwenye jambo lolote unalotaka kufanya kuwa huta weza songa mbele bila wao! Yani watafanya kila njia kukufanya uwamini kweli bila wao wewe huwezi songa mbele. Bila wao wewe hauna dhamani yoyote ile mbele za watu! SMH! Kuna mtu ambaye alishawahi kunuambia hivi karibuni “kama umeshindwa kupatana na basi hutoweza patana na mtu yoyote yule.” In my mind I was like ‘really’!! Who made you God!! Yani from their heshima yangu kwake imeshuka mno! I mean imeshuka sana! Kwani hawa ndio wale “watu” niliokuwa nawaongelea kwenye post iliyopita!
Watu wanafiki, wanacheka na wewe usoni kumbe nyuma yako wao ndio wanao suka na kusambaza majungu! Too bad, at this age and stage in my life I HAVE ZERO TOLERANCE NA WANAFIKI!……. anyway, mpendwa msomaji wangu nakusihi sana usimdharau binadamu mwenzio haswa usiye mjua. Huwezi jua huyo unayemdharau na kumdhihaki ndiye atakaye kuwa mkombozi wako! Only God sits that High! !
“Suala la mshahara si issue sana”- Mh. ShyRose Bhanji
Wakati niko Dawasco mwaka 2005 kuna makampuni makubwa kama 6 walinipa job offers ikiwemo NMB. Hata hivo NMB ndio walikuwa na mshahara mdogo kuliko wote…… nikaona si issue so nikachagua NMB kwa vile ilikuwa haijulikani kabisa na haikuwa kwenye soko. Nikajipangia malengo kwamba (yaliyoambatana na malengo ya NMB) ndani ya miaka 5 benki hiyo lazima ikue, iskike na iwe benki kubwa hapa nchini. Bahati nzuri benki tayari ilikuwa na mtaji mkubwa wa mtandao wa matawi almost nchi nzima…… kwa ushirikiano na wafanyakazi wenzangu tukaipaisha……. mshahara nilionza nao uliendelea kupanda kadri siku zilivokuwa zikienda……. lengo la post hii ni kuwashauri wale wote wanaotafuta kazi: suala la mshahara si issue sana ila pata kazi then onyesha maujuzi then kiwango chako kikionekana mshahara utapanda tu…