Jana ilikuwa siku ya wazazi shuleni kwao na Blessing. Hivyo baba alikwenda kutimiza wajibu wake ? watoto wakisikiliza kwa makini Wazazi wanachangia sana maendeleo ya watoto kwa kuonyesha kuwajali kwa kuchukua muda kukaa nao hata kama wako busy kiasi gani. Sio lazima ukae au ushinde na mtoto wako muda wote, bali ni nini unafanya naye wakati ukiwa free ndiyo inajalisha. The quality time you spend with your children is what matters not the time span. Kuna wazazi wako nyumbani 24 / 7 na bado watoto wao wako ‘homeless’!! Yani watoto hawapati quality time na wazazi wao. Watoto hawapewi wala hawa fundishwa upendo na wazazi wao. Watoto wana lelewa na video games au wana lelewa na mahouse girl wakati wazazi wanaishi hapo hapo nyumbani. Mzazi hata hajali wakina nani wanao mzunguka mwanaye hata mtoto anafanyiwa unyanyasaji hajui. Mtoto si mdoli (toy)! Mtoto ni mama / baba, mke / mume na kiongozi wa taifa la kesho. Je wewe kama mzazi umemuandaa vipi kushika nyathiwa hizo?! Tafakari na uchukue hatua.