Sister Penny doing what she does best! Kufundisha watu nikipaji cha pekee sana haswa kufundisha watoto wadogo. Sio wote wanaoweza kusoma na kushika pen au chaki wanafaa kuwa walimu / wakufunzi! Ni talanta waliojaliwa nayo watu wachache sanaaaaaa kama huyu dada yangu. Hapa ni siku ya Sabato (Juma Mosi iliyopita) akiwafundisha watoto maneno ya Biblia kuhusu uumbaji wa Mungu. Penny yeye si mwalimu, ila anahicho kipaji cha kuelekeza / kufundisha watu kwani hata sehemu kubwa ya kazi yake ni kuelekeza watu……Kama nilivyo sema kipaji cha kufundisha watu ni kipaji cha pekee sana, kwakweli mimi sikujaliwa nacho ?? mimi na panick haraka sana na huwa nakuwa confused kama mtu anielewi! Hata mwanangu anajua hilo yupo radhi afundishwe na mtu mwingine lakini siyo mimi ??? nilimfundisha kuendesha gari mbona ilikuwa ni patashika?! Lakini hakuwa na ujanja alielewa tuu mpaka akapata driving license yake. Hakuna ubaya wowote kusema your weakness (es) ni njia moja wapo yakuonyesha kuwa umekomaa kifikra na unajitambua!Hivyo mimi huwa nipo muwazi sana sioni shida kusema my weakness as a normal human being! Naomba nimpongeze dada yangu Peninah Tenga kwa kipaji ambacho Mungu amemjalia nacho na anakitumia kama kinavyo stahili, zaidi kwa kumtukuza Mungu. Ubarikiwe sana dada yangu na Mungu awaongoze watoto wetu washikemafundisho yake, Amen!