??? Nimecheka siyo kwamba ni mazuri bali nimejisikia “kafaraja kidogo” ndani ya moyo wangu kuwa kumbe siyo mimi tu peke yangu ndio nilisoma shule za #Kata au za watoto wa “walala hoi” wakati wa kutafuta elimu ya msingi. Kumbe hata Hoyce Temu naye alisoma kwenye shule za mazingira haya?! Wow! Kweli ulikotoka hakuna tija bali uendapo ndio mambo yote!?? Kumbe hata sisi tuliosoma shule za #kata huwa tuna ndoto ya kufanya mambo makubwa na kufanya dunia kuwa sehemu nzuri ya kuishi?! Kha! Kumbe inawezekana eeh!…….. Asante Hoyce kwa kutumege kidogo story yako! Naomba Mungu awajalie viongozi wote wa bara la Africa roho ya imani na utu ili waweze kutumikia watu wao kulingana na maadili ya uongozi na matakwa ya Mwenyezi Mungu. Africa bila vita inawezekana! Africa bila njaa inawezekana! Africa bila unyanyasaji kwa wanawake na watoto inawezekana! #UsikateTamaa #ItBeginsWithYou