Hii issue ya Joyce inasikitisha sana japo siyo jambo lakunishangaza kusikia unyanyasaji kama huo!..... Ma'am, nashindwa hata niandikaje kwani swala la domestic abuse kwa wanawake na watoto ni swala ambalo liko very near and dear to my heart but at the same time very sensitive to me! Niswala ambalo sipendi kuliongelea sana kwani bado linanikumbisha machungu mengi sana haswa kuhusiana na my dearest aunt ambaye ametangulia mbele ya haki!! Bado sijioni kama nina nguvu ya kuliongelea mbele za watu! Siku mwanaume akanyanyua mkono wake kunipiga aisee nitahakikisha hadi mama yake mzazi anapata "ngeo" ya kudumu!! Wala simpigi mimi namkodishia wahuni tu!! Stupid kabisa!! Hii karne ya 21 nani bado anapiga mwanamke?!! Tena hadharani kwenye gari?!! Halafu eti wapuuzi wanasema umekosea kusema hadharani, gosh! Anipige mimi aone mpaka CNN watamjua!.... Siku zote ukiona mwanamke amefikia hatua ya kuongea mambo yake ya ndani hadharani basi jua yamemfika!! Hana pakukimbilia asipo yasema ataishia kujiua!! Siyo kwamba hampendi mumewe hapana anampenda enough kutaka msaada wa nje waweze kumsaidia. You do what is best for you Joyce as long will save your life!! Wewe unafikiri kwanini mimi pia niliamua kuanzisha hii blog yangu?!! Niliona uonevu ninaofanyiwa nawapika majungu na kwakuwa Wabongo wengi ni wepesi wa kuamini uongo kuliko ukweli hivyo nikasema I need my own platform ambayo nitakuwa huru kueleze mambo yangu na kuweka ukweli hadharani ili kila mtu ajue! Niliona jinsi marafiki na ndugu walivyotumiwa kuwa maadui wangu number moja nikasema I am taking it to the public ili waone! Nakama mjuavyo njia ya muongo ni fupi, sasa hivi wenyewe wamefyata mkia! ......Hivyo Joyce usione haya wewe sema tu wenye akili zetu tulinakuelewa sana! Hapo utakuta umeangaika kwa ndugu na hakuna msaada wowote zaidi ya vikao visivyo na mbele wala nyuma! Halafu siku hizi unakuta kila kitu wanaingiza siasa hata maswala ya familia yani kweli siku za mwisho Biblia inasema shetani ataharibu familia na ndoa, na ndio haya tunashuhudia!! Kwanza huyo mumeo nikiongozi sasa kiongozi gani ambaye familia yake tu yawatu ambao naamini hawazidi 10 imemshinda kuongoza mpaka anampiga mkewe sasa ataongozaje jamii yenye maelfu ya watu?!!
Hii issue yako umenikumbusha kifo cha mtoto wa kaka yangu alikuwa anaitwa Joyce Kibindi. Mtoto wa watu aliangaika na mumewe eti ngoja yeye awe mjasiliamali uku amsapoti mumewe kwenda chuo kwani aliamini mumewe akimaliza degree vizuri basi atapata kazi nzuri na hali ya maisha yao itakuwa nzuri kidogo!! Ma'am, how wrong was she!!
Mume kamaliza chuo kapata kazi yenye mshahara nzuri kwani alikumbuka fadhila za mkewe!! Pombe na wanawake ndio walikuwa "mashosti" zake! Mke na watoto hana habari nao kabisa! Mtoto kaangaika kulalamika na kuitisha vikao kwa ndugu, wapi!! Wakina mama nao wimbo ni ule ule vumilia tu yanapita!! Mtoto wa watu alivumilia uvumilivu ukamshinda hakawa haoni pakukimbilia tena ISIPOKUWA KABURI!! At age of 28 with so much to live for Joyce committed suicide!!
Kifo cha Joyce kinaniuma sana mpaka wa leo hii, yani hata hapa naandika machozi yananitoka kwani nakumbuka jinsi alivyokuwa mzuri, smart, charming, very kind lakini maisha yake yalifupishwa because of the failed society!! Yes, hii jamii inayolea wanaume kuwa "cold hearted killers" kwa kuweka mazingira ya malezi ya kunyanyasa watoto wakike ndio inayoleta matatizo haya yote!! Nawakina mama ambao wanashindwa kusimama kidete na binti zao kwa kukemea hizi tabia hadharani ndio wanao ongeza matatizo haya! Embu fikira kama mume wa Joyce angekuwa muungwana angesema kuwa mkewe ndio asome kwanza si Joyce leo angekuwa bado yupo hai na familia ikawa salama! Yani kuna baadhi ya wanaume wa Tanzania wana roho za paka!! Niwakatili sijaona mfano hata hawa walioko huku nje ya nchi wana roho zakishetani!!
Halafu watajifanya kusingizia "siasa"!! Wengine wanataka uongozi wa communities ili tu kuficha maovu yao!! Kwakweli hii inafanya unaogopa hata kumsapoti mtu kwani hizi betrays ni nyingi mno!! ........Sasa baadhi ya wanawake wanaojifanya wasomi ndio wapumbavu hakuna mfano!! Sitaki hata kuwasikia!! Anyway, pole sana Joyce, nakama unajisikia kusema wewe sema tuu usije kufa bure kwa kujifanya shujaa ushwara!! Wewe kuongea haya yote yanakufanya uwe shujaa kwa wanawake wengi tu including me!! Hata Mungu anasema jisaidie kabla sijakusaidia!!
Related