Posho haikustahili kulipwa kwa Wabunge wanaolipwa mshara kila mwezi- Stephen Mndalila

Screenshot_2016-06-09-18-11-32-12015-04-22 21.13.43Kama wote tulivyo sikia kuwa Naibu Spika amesitisha posho kwa wabunge wote ambao wata sign kuwa wapo bungeni halafu baadaye kususia bunge kwa kutoka nje. Sina huwakika hii formula kama ina apply kwa wale wabunge watoro………basi RC Paul Makonda ali post hili swala kwa Facebook yake na kuomba maoni ya watu! Wengi wamefurajiya na kuunga mkono hoja hiyo. Na mmoja ya watu waliotowa maoni yao kuiunga mkono joja hiyo ni Stephen Mndalila. Naye maoni yake yalikuwa kama yafuatavyo:-

FB_IMG_1465514043663-1I think we need yo think about commonsense solutions! Wanyimwe posho na mshahara kwani kuna wabunge waliokataa kupokea posho na haiathiri maisha yao wala kutekeleza majukumu yao! Kwanza posho haikustahili kulipwa kwa wabunge ambao wanalipwa mshahara kila mwezi! Posho ni kuwaibia watanzania jasho lao! Eti unalipwa posho ya kukaa kwenye kikao wakati unalipwa mshahara na marupurupu? Posho iondolewe kwa kila mbunge na fedha zipangiwe shughuli zingine za maendeleo ya wananchi wengi walio masikini! Tuna jumla ya wabunge 396 na kila mmoja akilipwa posho ya laki 2 kwa siku na kujikimu ni laki moja na 20 kahiyo kwa wabunge wote kwa siku wanalipwa posho ya kukao jumla ya 79,200,000/- milioni 79 kwa kila siku wanapokuwa kwenye kikao! Na posho ya kujikimu ni jumla ya 47,52000/- milioni 47 laki 5 na 20! Mshahara kwa mwezi milioni 8! Awe amechangia hajachangia lolote bungeni analipwa! Kwanini hizi pesa za posho zisiondolewe na zikapelekwa kwenye kujenga hospitali na kununua dawa au kununua madawati au kujenga nyumba za walimu? Ifike kipindi kuwa mbunge ni kujitolea na isiwe sehemu ya kutajirika kupitia kodi ya wananchi labda wabunge watafanya kazi kwa bidii kwa sasa everything look luxury wakati watanzania wengi wanasota na umaskini!

Leave a Reply