“Put God first in everything you do! Don’t afraid to fail big! Don’t just aspire to make a living, aspire to make a difference!” ~~ Danzel Washington

https://youtu.be/-nF92WcPyUE

Sorry kwa msioelewa hii lugha, nakuomba utafute mtu anayeweza kukutafsiria……..Kiufupi katika maisha kufeli shule sio kufeli maisha! Shule ni muhimu sanaaaaaa lakini shule siyo kila kitu! Kumbuka kuwa hizo grade za kufaulu mtihani imewekwa na mwanadamu ambaye hajui Mungu ameumba ubongo wako katika ubora upi! Labda ungekuwa unafanya somo moja moja kila mwezi huwenda ungevuka viwango vyao. Hivyo mtu asikukatishe tamaa kwasababu sijui alipata A katika masomo yake, sijui ana degree ngapi! Mwambie mbona Danzel Washington kaweza, na alifeli college? Mwambie mbona Bill Gates ni tajiri mkubwa hapa duniani na hakumaliza college? Anasema mtangulize Mungu kwanza katika kila jambo, usiogope kushindwa hata kama utashiwa kwa kishindo kikuu, na usiridhishwe na kuishi maisha yako tu bali ridhishwa na kufanya utofauti katika jambo fulani au maisha ya mtu mwingine! ……..Angalia karama yako Mungu aliokujalia ndio uifanyie kazi! Hatuwezi wote tukapanda First class kwani vidole havilingani wala havifanani na hakuna enough space for all of us! Kuna wimbo fulani kwenye kitabu cha Nyimbo za Kikristo (tazama chini) unasema kama huwezi kesha mlangoni ukiwatolewa watu nafasi ya uzima basi kuwa kama Harun muaminifu ambaye alikuwa anasaidia kuinua mikono ya waliochoka, au hata sala na sadaka yako ni huduma / msaada tosha! Hivyo fanya kile roho yako inakugusa na kukupa amani!

107. Nipo Bwana, Nitume 
Hark! The Voice Of Jesus 

1. Sauti ni yake Bwana, “Kwenda, nani tayari” 
Mavuno yanakawia, Nani atayavuna? 
Kwa kudumu amaita, Zawadi atatoa; 
Nani atakayejibu “Nipo Bwana, nitume.” 

2. Kana huwezi safari Hata Nchi za mbali, 
Pana watu karibuni Wasio mjua Yesu; 
Kama huwezi kusema Jinsi ya malaika, 
Waweza kuutangaza Upendo wa mwokozi. 

3. Ingawa huwezi kuwa Mkesha mlangoni, 
Ukiwatolea watu Nafasi ya uzima; 
Kwa sala na kwa sadaka Watoa msaada, 
Kama Harun mwaminifu, Kuinua Mikono. 

4. Roho za watu zikifa, Bwana akikuita, 
Usiseme kwa uvivu, “Hakuna kazi kwangu.” 
Kwa furaha anza kazi Ile akiyokupa, 
Ukajibu mara moja “nipo Bwana, nitume.” 

Leave a Reply