Kusema kweli nimesikitishwa sana na kitendo cha baadhi ya Watanzania kumdhalilisha mototo wa Flora Mbasha. Naomba niseme mimi binafsi simjui Flora wala mumewe-Mr. Mbasha, na wala sijawahi kusilikiza nyimbo zake. Nilitokea kujua habari zake kipindi walipo kuwa na migogoro katika ndoa yao. Hapo ndipo nilianza kusoma habari zake na kuangalia mahojiano kadhaa ambayo alikuwa amefanya huko nyuma na baadhi ya TV shows. Hivyo ninayo andika hapa si kwamba namfahamu Flora au mumewe la hasha! Ni kwasababu ndivyo inavyo takiwa tufanye.
Kutokana na maneno ya watu kuwa huwenda huyu kichanga aliye zaliwa yawezekana asiwe mototo halali wa ndoa ya Flora na muwewe Mbasha kwa kuwa ndoa yao inamigogoro na kwa sasa wametengana. Basi wengi wamehoji nani ni baba halali wa mototo huyo. Cha kusikitisha zaidi wamenda mbali na kuweka picha yenye sura ya Flora, Mbasha (mume halali wa Flora), Gwajima (mtu anaye semekana ni Mchungaji na pia ana sadikika kuwa ndiyo baba wa mototo huyo), masikini piya sura ya kichanga hicho nayo imewekwa! Watu wote, wa mama kwa wababa, wakaka na kwa wasichana wote wanaandika comments za kudhihaki na kukebehi chini ya picha hiyo. Hizo comments nyingine zimewalenga wazazi, zingine zimewalenga washtumiwa, na zingine zinamlenga mototo huyo moja kwa moja! Mimi binafsi, nalaani vikali kitendo hicho cha kumdhalilisha mtoto wa Flora. Nakiita ni kitendo cha kinyama na ukatili wa hali ya juu. Children should be protected, and treated with the highest respected level of humanity regardless of how they entered this world!! Si Yesu ndio aliyesema “waacheni watoto wote waje kwangu maana ufalme wa Mbingu ni wao?!” Yesu hakubagua watoto, aliwaita wote kwake, sasa kwanini sisi tunabagua watoto? Matter-of-fact, children should never be the victim of their parents’ wrong deeds! Haijalishi mimba yake ilitungwa na wababa wawili, au ilitungwa mbele ya Madhabahu, au Msikitini, au ilitungwa kwenye majani porini, it doesn’t matter, and it should never matter; watoto wote wanatakiwa kulindwa na kuheshimiwa period!
Ni jukumu letu sote kama raiya wa hii dunia kulinda na kuheshimu watoto. Nandio maana nimeamua kuliongelea swala hili kwa uwazi katika blog hii. Hapa machozi yananitoka. Ndiyo, nalia! Kwasababu kwanza mimi ni mama, hivyo mototo huyu anaweza kuwa mwanangu wa kumzaa, au mjukuu wangu. Mimi ni dada, hivyo mototo huyu angeweza kuwa my niece or nephew! Jiweke kwenye miguu ya Flora, jaribu kuvaa viatu vyake kwa dakika moja, je ungekuwa wewe ungejisikiaje kuona mototo wako ambaye ndo kwanza amezaliwa katika hii dunia, hajui hata “social media” anadhihakiwa, na kudhalilishwa kwa namna hii?! Je, wewe ni mkamilifu? “Na asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe!” Mungu atusamehe kwakuwa hatujuli tulitendalo. Tulinde na Kuheshimu Watoto. Sing along with me…………….
Jesus loves the little children………..All the children of the world
Red and yellow, black and white………They’re precious in his sight
Jesus loves the little children of the world
Jesus cares for all the children……….All the children of the world
Black and yellow, red and white……..They’re all precious in His sight
Jesus cares for the children of the world
Jesus came to save the children………All the children of the world
Black and yellow, red and white………They’re all precious in His sight
Jesus came to save the children of the world
“The world will not be destroyed by those who do evil, but by those who watch them without doing anything.”-Albert Einstein