SABABU ZA UGIZA WA AFRIKA- Peter Sarungi

Ptr 1. DINI/IMANI YA WAAFRIKA NI IPI..?

Sababu ya kujiuliza maswali hayo ya juu ni kutokana na udhaifu, udumazi na ufinyu wa fikra zetu sisi watu weusi katika kuendeleza jamii zetu na bara letu. Kuna msemo inasema kuwa “Ukubwa wa matatizo ndio kipimo cha akili” na katika kutafakari kwangu nikakutana na falsafa ya mwimbaji hodari wa Tanzania Marehemu Remy Ongala (R.I.P) Alipoimba kilio cha samaki (Live perfomance). Wimbo wake umeniachia maswali mengi ya kutafuta majibu na kumepanua uwezo wa kufikiri zaidi tena tofauti ili tu nipate majibu.

Swali la kwanza: ni ipi Imani/ Dini ya watu weusi? Kabla ya kupata jibu hilo ni lazima tujue kuwa Imani ni hali ya kuwa na uhakika na vitu/ jambo lisilokuwa bayana yaani kuwa na uhakika na jambo usilolijua uwepo wake. Imani huponya, uhadhibu, huelekeza na hutatua matatizo katika jamii. Jamii ni lazima iwe na imani katika kujibu swali kuu la maisha baada ya kifo au kujibu matatizo yaliyoshindwa kuelezeka ama kutibika. Hivyo jamii nyingi zinataka kufanana katika imani ndani ya bara moja, mfano wazungu wanaamini katika kristo, wachina wana imani yao, wahindi wana imani yao, waarabu wana imani yao, wajamaica wana imani yao, wakorea wana imani yao na hata warusi wana imani yao. Na hizo ni imani zao ambazo hawaku iga kutoka katika jamii zingine bali zilibuniwa na wazee wa kale wa mwanzoni ili kujenga fikra za jamii zao kstika imani waliyoona inawafaa.

Je waafrika tulikuwa na imani ipi? maana imani ya ukristo na uislamu ni imani zilizoletwa kipindi cha ukoloni, ni imani tulizolazimishwa kupokea chini ya ukatili na utumwa wa kikoloni. kila mtu anajua athari za ukoloni, ukoloni ulisababisha tukawa wanyonge katika dunia, tukawa watumwa na wajenzi wa uchumi za wengine katika duni, tukalaani na kuacha mila&desturi na tamaduni zetu, tukapoteza imani zetu, tukadharau sayansi na teknologia zetu, tuacha mafundisho yetu, tukatupa fikra zetu na kununua elimu ya wakoloni, tukaacha majina yetu na kukumbatia majine ya wenzetu na tukaacha mitindo ya maisha yetu tukaegemea mitindi ya wakoloni. Ukoloni ulipoteza dira ya waafrika, ukapandikiza mbegu ya imani ngeni, mbegu ya elimu yao, mbegu ya kuiga kila kitu chao na kukiona ni kizuri, Mbegu ya kujidharau, kujinyenyekeza, kujipendekeza na kujishusha, Mbegu ya kushindwa kufikiri tofauti na mkoloni yaani waafrika tuna amini mkoloni ndio kila kitu hata maandiko ya imani zao zinatuaminisha kuwa wao ni wateule na lugha zao ndizo teule.

Waafrika tuliweza kumfukuza mkoloni na kupata uhuru kutokana na wazee wetu walio pambana kwa njia zote hadi za imani zetu kipindi hicho mfano vita ya majimaji. Pamoja na kumwondoa mkoloni lakini mkoloni aliweza kuacha mbegu zake za Imani, mafundisho na elimu katika lugha yao. Hizi mbegu ndizo ambazo zinasumbua sana kwa mtu mweusi kuwa huru katika kufikiri. Fikra zetu zimewekewa ukomo wa kufikiri katika kutatua matatizo ya jamii zetu. 

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

#MyTake

Waafrika hatupendani kwa sababu ya mbegu ya mkoloni, IQ za kufikiri ni ndogo kwa sababu ya mbegu ya mkoloni, tumekuwa wanafiki na waongo kwa wana nchi kwa sababu ya mbegu ya mkoloni, tumekuwa wabinafsi na wasaliti katika siasa zetu kwa sababu ya mbegu ya mkoloni, tumekosa dira na hata malengo thabiti ya miaka 30 ijayo kwa sababu ya mbegu ya mkoloni.

Tafakari na uchukue hatua

Leave a Reply