Leo siku ya kupiga vita dhidi ya unyanyasaji wa waina yoyote ile juu ya wanawake! …..Naamini watu wengi wanafikiria kupiga mwanamke ndio unyanyasaji pekee unao tambulika. Hapana! kupiga wanawake ni tatizo sugu sana Africa ndio maana unalisikia mara kwa mara. Na pia nitatizo ambalo watu wengi wako na hiyaria au comfortable kulizungumza hadharani! Lakini ukweli kuna unyanyasaji wa aina nyingi sana kwa wanawake! kama vile (1) unyanyasaji wa ngono / Sexual abuse (2) Unyanyasaji wa maneno / Viable abuse (3) Unyanyasaji wa hisia / emotional abuse (4) Unyanyasaji wa fikra / psychological abuse (5) Unyanyasaji wa kiuchumi au kifedha / financial abuse (6) unyanyasaji wa jinsia ya kike / female gender abuse, (7) unyanyasaji wa kiroho / spiritual abuse (8) unyanyasaji wa kutumia nafasi yake aliyo nayo / power abuse na mwisho ndo huo ambao ni common sana kwenye macho ya watu (9) unyanyasaji wa kimwili / physical abuseBinafsi hili swala la violence against women linanigusa sana na niko very sensitive nalo kwani nimeshuhudia sana kwa ndugu, jamaa, marafiki na hata mimi mwenyewe. Kwa mfano mwanaume anapo tumia positive image ya kuonyesha jamii kuwa anakupenda na watu wakaamini hivyo kutokana na “image” ambayo anaiweka mbele ya jamii kisha akafanikisha ku’-gain power na trust kwa jamii wakati ukweli huyo mwanaume hata salamu ndani ya nyumba hakupi! Huo ni unyanyasaji wa kifikra , kihisia, na power abuse. Unyanyasaji wa aina hii unatendeka sana hasa Africa lakini watu hawapo huru kuzungumzia kwasababu society in somehow wame u-legalized it!! Ni vigumu kwa mwanamke wa Africa ajitokeze mbele ya jamii na kusema huyu mume wangu ananinyanyasa wakati picha iliyopo machoni pa jamani ni happy family! Jamii ndio itakuwa ya kwanza kumuhukumu japo yeye ni victim!Nilishawahi wahi sema huko nyuma kuwa haya matatizo ya jamii yatatatuliwa au kukomeshwa na jamii husika. Jamii lazima iseme enough is enough!!……Na jamii ni nani?! Jamii ni wewe na mimi!! Usikubali kuwa sehemu ya hii laana ya unyanyasaji juu ya wanawake. Kemea hadharani na elimisha watu wote wake kwa waume kuwa hili halikubaliki! #ItBeginsWithYou