Wapendwa wasomaji wangu, maisha ni mafupi sana, mshukuru Mungu kwa pumzi ya uhai anayokupa kila siku! Na sio hivyo tu, Shukuru hata kwa vile unavyoviona ni vidogo kwani hivyo ndivyo vitakavyo kukamilisha wewe! Kama huwezi kushukuru hata kwa hivi vidogo Mungu anavyokujalia basi amini usiamini hautoweza barikiwa zaidi ya hapo!Kwamfano, mimi nilipokuwa under age ?, nilikuwa naomba Mungu anijalie niwe na uwezo wa kuwa nakuja Marekani mara kwa mara! Lakini tazama Mungu alivyo mwema, mimi sio tu ninauwezo wa kuja Marekani kama nitakavyo bali naishi Marekani! Kana kwamba hiyo haitoshi Mungu amenibariki zaidi ya mimi nilivyokuwa nikiomba, mtoto wangu amekulia hapa, amesoma hapa, na anaishi hapa! Kila ninapokuwa barabarani huku mwanangu ndiye anayeniendesha huwa na-smile in my heart nakusema ASANTE MUNGU! Najua siendeshi gari la kifahari sana kama wengine lakini namshukuru Mungu kwa kunitimizia ndoto zangu above and beyond my imagination!
Kuna watu wapo hapa hawajaona wazazi wao miaka chungu mzima! Wengine mpaka wazazi wao wanafariki lakini hawawezi hata kutoka kwenda kuwazika wazazi wao au ndugu zao! Sasa kwanini mimi nisimshukuru Mungu na kufurahia maisha wakati ninakila sababu!! Vile vile namshukuru hata kwa zile ndoto ambazo ameona zisitimie kwa wakati huu kwani yeye ndio mpangaji wa vyote najua atanitimizia tu! Natamani kuwa bilionea, najua hii ndoto itatimia tu kwa uwezo wake??? Nakama haitotimia bado maisha yatasonga na nitamshukuru kwa yote! Furahia maisha katika hali uliuonayo sasa kwani maisha ni mafupi sana usipo furahia sasa utafurahia lini?! …….Nawatakieni weekend njema kwenu wote! Hapa U.S.A hii weekend ni ndefu kidogo sababu Monday ni public holiday, nawatakieni happy memorial! Ngoja nifurahie maisha by sorrounding myself with LOVE! Eeh, niwape umbea? Muhaya kakasirika, mmh! Wivu ukizidi nao ni shidaaaa ???? but still nashukuru kwa yote ?? Mbarikiwe wote!