Naomba nianze kwa kusema hivi, msinichoke kumuweka au kumuongelea huyu dada yangu kipenzi cha roho yangu ndani ya hii blog! Naomba muelewa nampenda sana kwani ni wapekee mno! Usije ukafikiri ni kwasababu ni “super star” ndo maana na muweka humu hapana ni roho yake ya ukarimu, utu, na uungwana wake ndio maana na muweka humu and freely with all my heart I will always support what she’s doing. Watu kama dada ShyRose Bhanji ni wachache sana katika dunia hii ya leo iliyo jaa social networks ambazo too much fake people pretending kuwa wema wakati all the need is publicity na kutengeneza hela kwa kupitia migongo ya wenye maisha duni na wenye upeo mdogo wa kupembua mambo. Ni ngumu kujua nani nikweli anania thabiti ya kusaidia au kuguswa na jambo la mtu na kufanya kile awezacho kusaidia hiyo hali bila kutegemea faida yoyote ile. Na hiyo ndiyo sababu mimi nampenda sana huyu dada yangu kwani siyo FAKE! Ni mtu wa kujishusha, anaongea na kupenda watu wote bila kujali “status” zao. Halafu sasa ana ile “free spirit” just like me ?? you know what I am talking about right?! Yani Kama unataka ku have fun why kujibana bana? Go and have fun but accordingly to age appropriate! Siyo unakuta mama kalibia anaozesha bado anaangaika na show za kina “Yamoto bend” sasa teenagers nao wafanye nini? Jamani naomba muelewe kwanini nawaongelea sana watu waaina hii ya Shy-Rose Bhanji zaidi. Unajua tuna wadogo zetu / wenetu ambao wanatuangalia na kujifunza toka kwetu. Ambao wao napo itakapo fika muda wa kufunza kizazi kijacho watawafunza kile walicho jifunza toka kwetu? Sasa nini tunawafunza? Au ni nini unataka wajifunze toka kwako?! Basi nafikiri sasa mtaniruhusu niendelee kupost habari au picha za dada yangu kipenzi bila shida. Kwani ameonyesha mfano mzuri katika jamii yetu na anastahili kuigwa na kupongezwa na watu wote! “Today, my Nieces and I spent our time with such wonderful kids (orphans) while donating food and other necessities to Mwandaliwa orphanage in Mbweni. I thank Allah for enabling me to be able to donate, spend time, give love and affection to the ones who are less fortunate. We complain about such little things everyday and aren’t grateful or appreciative of the little things we do have. It really breaks my heart because there are so many people out there who aren’t even able to eat today. We have to learn to appreciate the little things in life and give back every once in a while. I was very inspired with the kids and their caretaker… It’s a true blessing to be able to give back….Thank you Lord!” Hayo ni maneno ya wadada wa taifa letu ambayo yaliambatana na hizi picha hapo jana alipotembelea kituo cha watoto yatima huko Mbweni ambapo ndipo naye anaishi katika mji huo.
Najua hii haikuwa mara yake ya kwanza kufanya hivi. Ameshafanya hivi mara nyingi tuu. Ila kinacho mtofautisha yeye na wengine wengi ni kuwa huwa atafuti “wapambe” wakuongozana nao. Yani yeye hufanya kimya kimya tunakuja kuona picha tuu. Wengine ni lazima watangaze weee na kutafuta wapambe ndio waende. Yani hao wa hivyo ni kutafuta umaharufu zaidi kuliko nia dhabiti ya kusaidia. Na ndio maana kuficha tabia zao inakuwa ni ngumu kwani wakitoa huko bado wanarudi kutukana na kudharau hao hao maskini ambao walijifanya kuwapelekea misaada. Au utakuta ni ngumu sana kwao kujichanganya na masikini japo wana pretend to care about them. Ni waongo sana! Hivyo kwa hili la dada yetu siwezi sema hongera dada ShyRose Bhanji kwani hakufanya hivi ili kupongezwa na mtu bali for her own goodness! Sina sababu ya kumpongeza bali namuomba Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa rehema na upendo azidi kumbariki huyu dada yetu kipenzi. Siwezi sema aendelee kwani hivyo ndiyo alivyo, bali azidi kumpa afya njema na uwezo wa kufanya haya mema ambayo anayafanya katika jamii yetu. Najua kuna baadhi ya watu watasema wapo wengi wanatoa misaada lakini hawajitangazi, we’ll nakubaliana na hilo! Naomba tuu ukumbuke ShyRose Bhanji hajajitangaza! Yeye alichofanya ni ku share picha kama anavyo share picha zingine za kumbukumbu ya vitu anavyo fanya hapa dunia as a good citizen of this world! Yani hii yeye ni tabia yake na si tukio la kutafuta umaharufu! Na naomba ujuwe kuwa hao wengine ambao wako kwenye level ya maisha au status ya dada yetu ShyRose Bhanji ambao hufanya vitu kama hivi bila kujitangaza au kuonyesha picha mitandao wengi wao huwa wana NGO zao na wanatumia hizo picha kupata hela kutoka kwa wafadhili nje ya inchi na ndio maana hawataki kuwa wazi kwani wanajua nia yao si ya kusaidia bali ni njia ya wao kupata kipato. Na ili watu wasijuie kile wanafanya basi wanaamua kufanya mamno kimya kimya! Jamani kwa mfano huu uliyo hai kabisaaaa hivi kunatatizo gani tukimfanya ShyRose Bhanji kuwa dada wa Taifa letu la Tanzania?! Kwani nani kanuna?! Mimi ndo nishasema hivyo ? Kuanzia leo hii ShyRose Bhanji ndiyo Dada Mkubwa wa taifa la Tanzania. Asanteni.