Wakati na join Efm @efm_93.7 nilipata support ya watu wengi na pia nakumbuka watu wengi zaidi walinicheka na kunong’onezana amepotea, amefulia ni ndio basi tena. Ametoka radio inasikika mikoa mingi Tanzania kaenda karedio kidogo kanasikika Dar tu na Pwani. Na inawezekana hadi leo bado wanacheka na kuponda.
Kwenye list zilikuwepo radio kubwa tu zilizopenda kufanya kazi na mimi. Kwa hali niliyokuwa nayo nilikaa kwa Kina na kufanya maamuzi. Nilishaanza kuboreka na redio lakini Nilifanya research zangu kitaa na uongozi wa Efm93.7 @efm_93.7 nilishakutana nao mara kadhaa kisha nikafanya maamuzi.
Nikasema Yes naanza upya tena kwenye radio ndogo na mpya na nina ona bright future ahead. Sio vibaya kuanza upya kwenye maisha na sio lazima kukariri formula ile ile au wasemavyo watu angeenda BBC sijui safari ya maisha yako ipo mikononi mwako.
Kuna ndege anaitwa Tai ndege huyu huruka juu sana, ana nguvu sana na akiwa juu anaweza kuona hadi chini. Ndege huyo kuna wakati manyoya yake na mabawa huzeeka anakuwa hawezi kuruka tena vizuri yaani anakuwa fala tu. Anachofanya anajificha kwenye mapango anajipiga piga mpaka manyoya yote yanatoka mwilini kisha yanaanza kuota upya. Yakisha jaa anatoka mapangoni akiwa kazaliwa upya na anaruka tena juu zaidi mabawa yakiwa na nguvu zaidi.
Kuna wakati kwenye maisha inabidi uwe kama Tai. Anza upya, tafuta nguvu mpya, unakubali umepigika then unaanza upya. Efm nimekutana na vijana bado wana nguvu, ari na kiu ya kufanikisha nimejifunza kutoka kwao na wanajifunza kutoka kwangu. Ni miezi 7 sasa toka nimeanza hapo I feel new, spirit yangu imeamka upya kama wakati ule naanza 2005_2006
Leo Efm 93.7 @efm_93.7 imetimiza miaka 2 na bado mambo mazuri na makubwa yanakuja my big boss @majizzo na vijana wake hawataki utani TUNALISONGESHA
#tunalisongesha HAPPY BIRTHDAY EFM