Regrann from @open_kitchen2014 – Siku zote katika maisha yangu nilipenda sana kuitwa mama lakini kwa sababu ya uzito wangu ambao ulikuwa unanipa complications katika uzazi ilinichukua muda mrefu sana kufanikiwa mwaka 2010 nilibahatika kwa mara 2 kupata ujauzito baada ya hormone treatment za kufa mtu nilipigana na kubeba mimba mpaka almost 7 months lakini kwa bahati mbaya my pressure haikuwa controlled vizuri mtoto akafia tumboni nilikaa labour masaa 12 sitokaaa kuyasahau mpaka nikafanikiwa kujifungua and she was a girl almost 1.5kg tukamzika next to my mum . Baada ya mwezi nikapata bahati ya kwenda shanghai china kulikuwa a world expo kupitia Tan trade nikafunga mzigo wangu wa vinyago maana ilibidi nifanye mchaka mchaka nikapakia mzigo kwenye container pamoja na wenzangu na hapo sijapona vizuri ila Mungu ni mwema alinipa nguvu za ziada mwezi unaofuata nikapanga safari na kuondoka hakuna siku niliwahi kumwona mume wangu analia kama hiyo siku ananipeleka airport alilia sana kwa uchungu na kunionenea huruma kwamba sijapona vizuri then naenda kuhangaika nguvu zenyewe bado hazijarudi vizuri alinibembeleza sana nikamwambia bora niende nikapigane nifanye kazi kuliko kukaa kitandani na mawazo mimi naamini kila jambo Mungu anapanga kwa muda wake i am strong mentally na nitaweza tu wewe kuwa na amani.
Tulikuwa wafanya biashara wengi kidogo kama 10 hivi tulifika na kupokelewa vizuri na watu wa ubalozi wetu so ikabidi tu share apartment mimi akaniomba dada mmoja ni share nae alikuwa na mtoto wa kiume alikuwa kama na miaka 10 plus or 8 yrs hiyo apartment ilikuwa single room so mimi nikachukua bed wao wakasema watachukua sitting room because kuna more space na kuna sofa bed kubwa basi next day tukaanza kukimbizana kupanga mizigo kwenye banda letu kwakweli ilikuwaa kazi ngumu sana kwasababu mzigo ulikuwa umeshushwa almost 2km away ndio store ilipo vinyago ni vizito sana so inabidi uvitoe store uje kuvipanga kwenye banda na ukifika lazima uvipige kiwi yaani tulikuwa hoi na huwezi kuleta vyote maana nafasi ndogo so inabidi ulete kidogo kidogo na hapo sina nguvu za kutosha but najipa moyo i can do this ukizingatia hakuna kukaaa ukimaliza kupiga kiwi kupanga unasimama uuze bidhaa zako yaani ikifika jioni miguu yote imevimba unchoka hata kuongea huwezi.
Yule dada aliyeomba kukaa na mimi akawa so rude kwangu ghafla mara kanuna mara hataki mtoto wake akuongeleshe watu tunakaa same room tunfanya biashara same banda dah nikasema huu ni mtihani but mtoto was so kind akawa tukikutana nje ananiambia Aunty its ok my mum is like that msamehe tu he was a good boy mimi nikaamua kumpotezea na kuishi kivyangu nikiingia room kwangu kimya naoga nalala .
Nikiamka naenda store najazia mzigo kwenye stand yangu napiga kazi na hapo mchina hajui kiswahili wala kingereza biashara tunafanya kwa calculator yaani we acha tu unaongea mpaka unapasuka untoa mifano yote maana wote tunauza same product sasa wewe hapo inabidi uwe mjanja mteja akipenda kinyago chako usimwachie ukimwachia tu imekula kwako Aiseee nilipigana for 4 weeks none stop 7 days a week 12 hrs kila siku on my feet Mungu ni mwema niliuza mzigo wangu wote sikubakiza hata kitu kimoja nilimshukuru sana Mungu maana kuna wamasai wakubwa wananishinda urefu nilisema hawa kweli nitawauza but i had faith mteja alikuja akanipa bingo ndefu dah i was so happy nilipomaliza tu mzigo nikafunga sanduku langu huyooo nikarudi zangu dar mifuko imejaaaa nilikuwa nimechoka sana but i did it niliinvest kama dola 10,000 usd kila kitu mzigo plus all expenses nikapata kama 35,000 usd in 30 days i was so happy nilijiona mimi ni mshindi mkubwa sana i did not give up kabisa mazingira ya kazi na kuishi yalikuwa magumu but i stayed focus .
Miezi miwili baada ya kurudi nikajikuta nina mimba tena nikaanza hormone treatment pressure ikawa controlled then Mungu akanipa zawadi ya Baby Iman so leo nataka wewe usikate tamaaa no matter what NEVER GIVE UP BELEIVE IN YOURSELF AND BELEIVE IN GODS TIMING .
kila kitu Mungu anapanga kwa muda wake mitihani inakuja kila siku we need to stay focused
Watu tumetoka mbali sana kwenye haya maisha ya kupambana but Mimi sijawahi kukata tamaa? – #regrann