Leo nimepewa somo na Sir O.O Igogo kuwa uwaminifu na huruma ni nguzo kuu ya maisha, hivyo nizingatie! Aliyasema hayo baada ya kunitumia picha ya aliyekuwa mke wa mmoja wa fundi wetu marehemu Tyson.
Mke wa Tyson alitokwa na machozi baada ya kukabidhiwa fedha ambazo ziligundulika kuwa zilikuwa hazijamaliziwa kulipwa katika kazi ya ujenzi wa ukuta wa nyumbani kwetu ambayo marehemu mumewe aliifanya mwaka 2014. Jamani msiwe wadhurumaji kwani hauto kaa ubarikiwe kamwe! Wengi wanashindwa kuelewa kwanini mafanikio yao huwa yanakuwa ya muda mfupi wakati wengine maisha yanawanyookea mika nenda miaka rudi! Acha dhuruma Mungu hapendi!! Machozi ya watu yanalaana sana! Btw, wangapi huwa mnaweka rekodi ya kila risiti na gharama za ujenzi wa nyumba zenu? Hii huwa naona sana kwetu kila jengo huwa nakitabu chake kila kitu kinarekodiwa na risiti zote zinatunzwa. Ujenzi ukikamilika basi kitabu kinakaguliwa na kufungwa na kuwekwa kwenye kumbu kumbu za kudumu. Sasa kama kuna mtu hakulipwa pesa zake kama marehemu Tyson au kuna kitu kilisahaulika kufatiliwaa basi kitafanyiwa kazi wakati huo. ………Anyway, poleni sana wafiwa. R.I.P Tyson!