Ni bahati mbaya sana kwamba shuleni tunafundishwa jinsi ya kuwa mwanasheria, wahandisi au daktari hatufundishwi jinsi ya kuwa ‘mwanamume’. Matokeo yake unakuta mwanamume anashindana au anapigana na ‘mwanamke’ au wanajibizana maneno kwenye simu au Instagram au Facebook au what’s up. Toka wakiwa watoto vijana wa kiume lazima wafundishwe kuwalinda na kuwahifadhi dada zao. Ili wakiwa wakubwa wawalinde na kuwatetea wake zao. Kukosa kufanya hivyo ndio unakuta mwanamume mtu mzima anapigana na binti baa au club, au anashindana na binti kupanda daladala, au anampita mama mjamzito kwenye foleni, halafu anajiona mjanja wa mjini, siwalaumu kwa sababu elimu hii imepuuzwa.
Kaka yangu, umesema kweli kabisa kuwa elimu hii imepuuzwa. Asante kwa kuliona hilo. Lakini hukusema nani aliye ipuuza?! Maadili huwanzia nyumbani. Watoto hujifunza kwa kuangalia wazazi wao wanafanya nini na si kusikia wazazi wanasema nini! Wazazi wanaweza ongea sana lakini kama wao wenyewe hawaishi kulingana na kile wanacho kisema basi ni bure! Hili limekuwa ni tatizo kubwa sana na imesababisha wazazi wengi wa wakizazi hichi cha karne hii kupungukiwa na maadili na hekima! Utakuta wengi wanajua kuongea lakini angalia matendo yao je yanaendana nayale wayasemayo?! Sasa hicho ndicho nawao walicho jifunza kutoka kwa wazazi wao ‘kuongea bila matendo’! Baba anasema heshimu wakubwa wakati huo huo baba huyo huyo anamtukana na kumdhalilisha mama / mkewe mbele ya watoto! Unafikiri watoto watajifunza nini? Don’t get me wrong siungi mkono udhalalishaji wa aina yoyote ule. Haijalishi unafanyika mbele za watu au in privite! Nalaani vikali mno!……Pia tatizo lingine wakina baba (haswa wa Kiafrika) walio wengi wako very selfish! It’s all about how they feel bila kujali watu wengine haswa watoto zao wanajisikiaje. Mawazo ya watoto hayathaminiwi kabisa katika ngazi ya familia! Basi na hii imechangia sana watu kuwa selfish kwasababu kila mtu anafikiria nafsi yake yeye mwenyewe hata kama wengine wanaangamia ilimradi yeye anafurahia moyoni mwake basi hiyo ni sawa!
Tunatakiwa tubadilike, na mabadiliko yanaanza na wewe mwenyewe. Its about time to start a real talk about ‘familyhood’ in African families particularly Tanzanian community! When you know better you do better!