Hii ni very late post, lakini mtaniwiya radhi kwani I only blog at my spare time! Wenzetu wanasema “better late than never”! Nitukio ambalo lilikuwa limeandaliwa na organization ya Vital Voices wakishirikiana na Dare To Dream foundation! Kiongozi wa shughuli yote alikuwa ni Emelda Mwamanga (Mrs) ? ambaye ndie Mkurugenzi Mkuu wa Dare To Dream foundation, Bang Magazine, na pia ni “mshika bendera” a.k.a Ambassador wa Vital Voices Tanzania! Mgeni rasmi alikuwa ni Mh. Devota Likolola (Mbunge viti maalum)
Tukio zima lilifanyika siku ya Jumamosi, tarehe 08, March, 2017 katika ukumbi wa Danken Hall pale Mikocheni. Ambapo yalianza kwa kutembea kidogo huku wanawake wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali kuwakilisha sauti ya vilio vya wanawake wote inchini Tanzania na dunia kote!
Dhumuni haswa la hii shughuli ilikuwa kuwakutanisha wanawake wote ili kuadhimisha siku ya Wanawake duniani na pia kujifunza mambo mbali mbali toka kwa wanawake ambao wamethubutu kufata ndoto zao na kufanikiwa japo kwa changamoto mbalimbali ambazo zingewafanya wakate tamaa! Pia kulikuwa na mambo mengine ya kujifunza kutoka kwa wanawake wengine katika makundi yao kama VIKOBA! Katika shughuli hiyo kulikuwa na baadhi ya Motivational speakers ambao waliongea mambo mbali mbali yanayo husu nafasi ya mwanamke katika kuendeleza uchumi wa familia na jamii kwa ujumla. Waongeaji hao alikuwepo Mh. Devota Likolola, Dr. Blandina, Chris Mauki, Mkandarasi bora wa kike-2017 Ms Waziri (Nimesahau jina la kwanza) na wengine wengi!
Waongeaji wote waliongea vizuri sana na ifuatavyo ni sehemu ndogo ya maongezi ya Dr. Blandina ambapo aliwasihii sana wanawake kuwa na tabia ya kujifanyia tathimini wao wenyewe badala ya kufanya vitu kwa kufata mkumbo wa marafiki / mashoga! Pia aliwataka wawe na tabia ya kujiwekea malengo na strategy plan ya maisha yao kama kweli wanataka kuingia kwenye dunia ya kujenga viwanda kama wanaume! Na zaidi aliwasihii kutokuogopa kutumia neno HAPANA pale panapo bidi kutumia neno hilo! Tafadhali msikilize mwenyewe. ….?
Shughuli hii kwakweli ilikuwa nzuri sana! Binafsi nilijifunza mengi, tulifurahi na kuburudika. Ngoja nikuonjeshe kidogo ?
Asante sana Emelda Mwamanga na timu yako yote! Salome thank you much! Be blessed!