Hapa Marekani kuna watu wajulikanao kama Waamish. Hawa watu hawatumii umeme, hawa endeshi magari (wanatumia puna na farasi kama usafiri), hawaendi shule hizi za Kawaida kwani wana shule zao wenyewe ndani ya vijiji vyao. Wala hawatumii technology yoyote ile ya kisasa, na vyakula vyao ni organic tuu ambavyo wanalima wao wenyewe. Nguo wanazo vaa hushona wao wenyewe ambazo ni style zile za kizamani sana na huwa hazibani yani ni kubwa kubwa.
Wanatabia ya kuishi nje ya mji kwa mfumo wa vijiji. Familia zao huwa hazitengani kwani nyumba zao huwa ndefu kama treni! Kila mtoto wa kiume akiowa anaongeza chumba chake kwenye mstari. Nilipo kuwa naishi Wichita nilibaatika kuwatembelea kwenye makazi yao. Kwakweli unaweza usiamini kuwa ni Marekani. Chakushangaza ni kuona Wamarekani wakiwashangaa Waafrika ambao bado wanaishi katika mazingira kama haya wakati hapa kwao pia wapo!!
Anyway, hizi picha ni za rafiki yangu Janet Kisyombe. Yeye na ndugu zake walibahatika kuwatembelea hao Waamish siku chache zilizopita. Ni watu ambao ukikaa nao utabaki unashangaa sana. Kama mtu anatumia moto wa kuni kufanya nyumba iwe na joto wakati wa baridi ambapo angeweza kuweka umeme na kurahisisha kila kitu! Asante sana Janet kwa picha. Ubarikiwe