TAFAKURI YA LEO JUU YA CCM MPYA -Peter Sarungi

Peter Sarungi (The next Speaker)

Nimepata taarifa juu ya kuzaliwa CCM mpya iliyo badilika katika muundo wa chama na uendeshaji lakini ikiendelea kubaki na itikadi yake ya zamani. CCM Mpya iliyosemwa na mwenyekiti wake kwamba itakuwa chama kwa wanachama yaani chama kitakacho milikiwa na wanachama wenyewe tofauti na mwanzo. Inasemekana kabla ya upya huu, chama kilikuwa kina endeshwa na wanachama wenye nguvu za fedha, vyeo na hata umaarufu. Sasa kwa upya huu, chama kitaendeshwa hata na mlalahoi bila kujali umaarufu wake, cheo chake ama fedha zake… (SAFIII SANAAA..) 

LAKINI..????? Tafakuri yangu ni jinsi gani chama hiki kitaendeshwa na kumilikiwa na wanachama kama inavyoitwa CCM Mpya… ………Ikiwa kiwango cha uwakilishi wa wanachama hawa kwa idadi katika vikao muhimu na vinavyo toa maamuzi muhimu ya chama umepunguzwa kwa zaidi ya nusu??? Yaani kutoka mia tatu na kitu hadi mia moja na kitu..!!!Ikiwa idadi ya vikao vilivyokuwa viki tathmini utendaji wa chama na serikali vimepunguzwa???Chama chenye wanachama na wapenzi wapatao milion 8, kutoka mikoa 35, ikiwa na jumuiya mbalimbali karibia tano na matawi lukuki, chama kinacho ongoza nchi kuongozwa na wajumbe 165 badala ya 385 alafu tuna sema CCM mpya ya kumilikiwa na wanachama??

Hili panga ni kali na sijui kama hawa vijana wenzangu Benard R. Shigela ?na Yesaya Shamsele ?walio anza vizuri kujifunza siasa na uongozi kama watapata nafasi na fursa ya kuwepo kwenye vikao vya CCM mpyaJJk alidokeza sababu ya mabadiliko haya kuwa ni UKATA…. Tunasoma Namba.. Hii sababu ya kuifanya CCM kumilikiwa na wanachama bado kwangu haija ingia akilini labda wadau watufafanulie..

Leave a Reply