Imeandikwa….
1. Baba bora ni yule anayelinda na kutetea familia yake, anaye tengeneza urithi mzuri kwa watoto, wajukuu hadi vitukuu na anaye hashimu familia yake.
2. Mke mwema ni yule anaye jenga familia yake bila kuharibu kwa mikono yake, anaye lea watoto katika maadili mema na anaye simama imara na mumewe katika hali ya hatari, dhiki, shida, raha, hofu, furaha, matatizo kama ya siasa, umasikini, chuki, wakati wa ujana na uzee, wakati wa afya na magonjwa.
3. Mtoto bora ni yule anaye heshimu wazazi wake na kujifunza maadili na maarifa kutoka kwa walio mtangulia. Ambaye anapenda kuwa kichwa na si mkia.
#MyTake.
Vijana ambao wamefika umri wa kujenga familia wachukue hatua kufanya hivyo, wasisubiri harusi na madoido ya kifahari maana kuna maisha ya ndoa baada ya kupata sifa za harusi.
??Fidel Pilato alikuwa akiangalia post zangu za nyuma huku akijaribu kuuliza maswali katika lugha nisiyo tambua.???…Hao ndio watu wazima wadogo, Taifa la kesho. NIWATAKIE MWANZO MZURI WA WIKI………MUNGU BARIKI KAZI YA MIKONO/AKILI ZENU.