Dikteta ( Kwa lugha nyepesi ) Ni mtu ambaye anaongoza Nchi Kwa faida yake yeye na kundi lake la utawala. Tanzania haijawahi kuwa naye mtu wa namna hii. Mfano wa Huyu Ni Mobutu, Bokasa, Idi Amin nk.
Dikteta Uchwara ( Kwa tafsiri yangu ) Ni mtawala ambaye anaelekea kuwa Dikteta Kwa tafsiri hiyo hapo juu. Tanzania haina kabisa Huyu maana hawezi kutokana na misingi ya Nchi kuwa imara.
Dikteta Mamboleo Ni mtawala ambaye analeta Maendeleo bila kutaka kuhojiwa. Maji mtapata. Barabara mtapata na Hata ndege mtapata lakini msihoji amepataje. Mifano ya madikteta mamboleo Ni Mingi sana duniani na ndio madikteta wa kisasa hao. Mfano maarufu Ni Vladimir Putin.Haya ni baadhi ya maoni ya watu ?