Nilikutana na huu ? mjadala huko Facebook nikaona ni share nanyi……………Kitu ambacho huwa sielewagi ni kwanini baadhi ya Watanzania wanapenda kuilinganisha Tanzania na Marekani inapofika kwenye swala la maendeleo ya miundo mbinu na siasa? Hivi hamjui kuwa Marekani hawakutumia jasho lao kuijenga hii nch?! Marekani ilijengwa kwa nguvu ya watumwa! Watumwa walimwaga damu na jasho lao lilibubujika kuijenga hii Marekani ambayo mnataka kufananisha na Tanzania. Tanzania inajengwa kwa au itajengwa kwa jasho lako wewe na mimi!! Sasa sijui kwanini wewe unayelalamika usikubali kutoa jasho lako kwa maendeleo ya nchi yako? Kulalamika kwako hakuijengi Tanzania bali linajenga a “whining. Nation”!! Jiulize wewe kama Mtanzania mzalendo unachangia kitu gani katika maendeleo ya nchi yako? Au unaongezea watu stress zisizokuwa na ulazima!! Tafakari!