Ni miaka 59 ya kujuana kwao na September 12, 2020 walitakiwa kufikisha miaka 56 tangu wale kiapo kitakatifu cha ndoa yakwamba “MPAKA KIFO KIWATENGANISHE”! Kiapo chao kitakatifu aliapa katika kanisa la Roman Catholic lillopo katika kijiji cha Kowak, wilaya ya Rorya mkoa wa Mara. Siku ya leo tarehe 06 / 05 / 2020 Mungu aliamua kuitimiliza ahadi walio iweka mbele zake. Mnamo majira ya saa kumi na moja alfajiri saa za Africa Mashariki baba yetu kipenzi mzee Joseph Musira alilala usingizi wa mauti katika hospital kuu Musoma alipokuwa akipatiwa matibabu!
Tunahuzunika kwasababu sisi ni wanadamu tulioumbwa kwa hisia. Tulikua bado tunampenda sana. Rafiki yake (Mke wake) bado alikua anamuhitaji sana. Lakini mapenzi ya Mungu yametimia nasi tunasema Amen!
Pumzika kwa amani ya Bwana baba yetu, ulitupenda nasi tunafarijika kujua yakwamba umelala ukitambua upendo wetu kwako. Maisha uliyo ishi ni mfano wa kuigwa kwa watu wengi sana. Umeishika imani na kuiishi kwa vitendo mpaka mwisho wa safari yako. Ulikuwa Mwalimu ulielimisha jamii nyingi sasa. Mchango wa elimu kama Mkurungenzi wa elimu wa mkoa katika Diocese ya Mkoa wa Mara kwa zaidi ya miaka 25+ kamwe hauta sahaulika. Hata baada ya kustahafu walikuhitaji wakati wote nawe hukusita kwenda kusaidia. Kazi zako za kujitolea katika mambo mbali mbali ya jamii zimeacha alama kubwa kwa vizazi vya sasa na hata vijavyo.
Asante kwa kuwa baba mlezi wa mama yangu wakati akisoma Secondary. Kazi ambayo hukusita kuifanya tena kwangu mimi nilipokuwa mwanafunzi pale Kowak Girls Secondary school. Umeishi maisha vyema nasi tutayasherekea kwani unastahili! Pumzika kwa amani, tukutane asubuhi njema. ????
“Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.” ** 2Timothy 4: 6-8
- “Leo ngoja niandike kidogo. Mwl. Joseph Musira alikuwa baba kwangu, alikuwa Mwl. wangu wa hesabu na Jografia nikiwa nikiishi nao ni mshauri. Alinilea kwa upendo usio mfano akiniita “rafiki yangu” Halafu ananitania “Susilia” kisha anacheka wote familia ni kicheko. Jamani na umri niliyo nao nikimsalimia Mwl. kwenye simu napiga magoti hadi chini, watu hunicheka kwa kupiga magoti kwa mtu nisiyemuona lakini upendo wake ulinikaa katika akili mimi nashtukia nimeshapiga magoti nikisikia sauti yake. Mzee Musira, ameniinua kutoka msingi, amenifanya nimefikia hapa kwa kunisaidia na kunitia moyo nikiwa darasa la saba hadi nikafanya vizuri na kujiunga na Rugambwa Sekondari School enzi hizo. Mara ya mwisho nilikwenda kuwasalimia akiwa ameanza kuumwa nikampelekea Rozari nzuri kutoka Jerusalem akafurahi sana kwa maana Wimbo wake ulikuwa sala. Lakini safari imefika hatungeweza kuongeza dakika wala nukta. Amepiga vita vilivyo vizuri vya upendo akiwa ni mkwe wa kwanza kwa Baba yangu na mama yangu Marehemu Mzee Cornel Awiti Oyata na mama Valeria (Mareh.) Maishao yao ni hubiri tosha kiasi kwamba mabinti na wajukuu wa Mzee Awiti wangeiga mfano wao hakika kifo ndicho kingetutenganisha na wenzi wetu. Baba wa mfano na kila mara mimi na mzee wangu O.O Igogo tunawataja kwa maisha matulivu, furaha na amani waliyonayo. Familia hii ninawaombea faraja peke yake Bwana awatie nguvu ni maumivu makali lakini ni lazima tushukuru kwa kila japo. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake litukuzwe.” *** Shemeji wa marehemu Mama Igogo pichani juu ????
Till we meet again baba yangu, tutakukumbuka daima!
One thought on “Tanzia: Pumzika kwa amani baba yetu mzee Joseph Musira”