Tanzia: pumzika kwa amani ya Bwana baba mkubwa mzee John Obure!

Marehemu mzee John Obure enzi za uhai wake

Kwaniaba ya familia ya Mr and Mrs O.O Igogo naomba kuchukua nafasi hii kutoa salamu zetu za pole kwa familia ya marehemu mzee John Obure na Mwalimu Anna Cornel Awiti a.k.a Mrs John Obure, kilichotokea alfajiri ya leo huko Mwanza, Tanzania. Tunawaombea utulivu na amani wakati wote wa maombolezo wa msiba huu wa baba na Mungu akaendelee kuwa nguzo imara na kimbilio lenu wakati wote. Mwenyezi Mungu akawe mfariji wenu siku zote. Sisi sote tu mavumbi na mavumbini tutarudi!

Kwa faida ya wasomaji wangu, marehemu mzee John Obure ni baba yangu mkubwa. Yeye alimuoa mama yangu mkubwa ajulikanaye kama Mwalimu Anna Cornel Awiti. Wao maisha yao yote yalikuwa Musoma, na miaka ya hivi karibuni walihamia kijiji cha Shirati kilichopo wilaya ya Rorya mkoa wa Mara. Mzee John Obure yeye ni mzaliwa wa Shirati, na alioa mrembo toka kijiji cha Kowak wote ni wana Rorya kwa asilimia 100%!

Mr and Mrs John Obure wakiteta!

Kama wanavyo onekana pichani ni marehemu akiwa na mkewe wakiteta jambo fulani wakati wa msiba wa baba yangu mkubwa mzee Joseph Musira (soma ?) Tanzia: Pumzika kwa amani baba yetu mzee Joseph Musira ….. Marehemu Mzee Joseph Musira alioa first born (mtoto wa kwanza) na Marehemu mzee John Obure alioa second born (mtoto wa pili).

Mama zangu wakubwa mtoto wa kwanza na wapili katika pozi nyumbani kwa Mr and Mrs Musira. Wote ni wakazi wa kudumu hapo Musoma, hivyo ni majirani.

Mama zangu, mabinti wa mzee Cornel Awiti na Valeria Awiti

Pichani ni mama zangu wote 6 kwa ujumla wao. Mwenye nguo ya Orange (rangi ya chungwa) ndio mke wa marehemu mzee John Obure. Bibi yangu mzaa mama alizaa watoto 12 ambao walikuwa mpaka utuuzima! Sita (6 ) wakiume na sita (6) wakike. Wakike wote wapo hai, twamshukuru Mungu kwa hilo. Lakini wakiume wamebaki watatu (3) na watatu wengine wamesha lala usingizi wa mauti. Lakini kiuhalisia bibi yangu alizaa watoto 14! Uzao mmoja ulikuwa pacha (twins) wao walikufa siku waliozaliwa. Twamshukuru Mungu kwa yote.

Pichani juu nikiwa na mama yangu mzazi pamoja na mmoja wa watoto wa marehemu ajulikanaye kama Dr. Joseph John Obure. Hapo ilikuwa ni 2018 Washington DC. Kaka yangu huyu yeye anaishi North Carolina na familia yake.

R.I.E.P baba mkubwa!

Kwa mara nyingine tunatoa pole zetu za dhati kabisa kwa familia ya marehemu mzee John Obure.

“Kwa jasho lako utajipatia chakula mpaka utakaporudi udongoni ulimotwaliwa; maana wewe ni mavumbi, na mavumbini utarudi.” *** Mwanzo 3.19

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote. ????

Siku ya mazishi

Mke wa marehemu

Dada wa marehemu!
Dada mkubwa wa marehemu

Wajukuu!

mtoto wa marehemu (watatu kuzaliwa) Dr Joseph Obure
Mtoto wa marehemu (wapili kuzaliwa) Deus Obure

Leave a Reply