TATIZO MMEKUBALI KUCHEZA NGOMA ZINAZO PIGWA NA UPINZANI.- Peter Sarungi

 Kwenye ngoma zetu kuna wanao piga ngoma na kuna kundi la wanao cheza ngoma inayopigwa. Siku zote mpiga ngoma ndiye mwamuzi wa aina gani ya mdundo upigwe ili mcheza ngoma acheze, mpiga ngoma akizima ngoma basi na mchezaji naye anasitisha kucheza, mpiga ngoma ndiye ana amua speed ya ngoma ama ngoma ipigwe kwa muda gani.

Siasa za sasa za nchi ziko kisayansi sana kiasi kwamba upinzani wametawala njia nyingi za upashaji habari. Siasa hii naifananisha na ngoma zetu za jadi, yaani ni kama vile upinzani wanapiga ngoma ili watawala wacheze.

Hii ngoma ya wapinzani imeanzwa kuchezwa tangu mwaka jana baada ya utawala mpya kuanza kazi, upinzani umeshapiga ngoma kwa midundo mingi sana tofauti iliyomfanya mtawala kucheza bila kuchoka.

Hizi ni baadhi ya ngoma zilizopigwa na upinzani na watawala wakacheza kwa maana ya kujibu mapigo.

1. Ukuta

2. Uchwara

3. Phd

4. Michango ya Tetemeko

5. Njaaa

6. Bring back ben alive

7. Free Lema

8. Free Max wa JF

9. Swala la uteuzi wa wabunge

10. Bashite

Haya ni machache yaliyo vuma na kuchukua headlines za magazeti na mitandao ya jamii. Na hizi zote zimekuwa zikianzishwa kwa malengo ya kuonesha na kuaminisha mapungufu ya serikali kwa wananchi.

Siwalaumu upinzani maana hiyo ndiyo sayansi ya siasa na ndiyo kazi yao, ila nawalaumu sana chama tawala na watawala wenyewe kwa kushindwa kupiga ngoma zao ili upinzani nao wacheze. Ninavyojua mimi, JPM amefanya mambo makubwa ambayo yanatosha kuwekwa kwenye haedline kwa muda mrefu, lakini wasaidizi wa watawala na wapenzi wa chama tawala wamekaa kimya na kujikuta wakijibu mashambulizi ya upinzani katika hoja zao bila kujua kwamba wanacheza ngoma. Hizi kick ndizo zinazo pamba upinzani usisahaulike hadi 2020 hata kama mkikataza siasa za majukwaa.

Au labda watawala wamejitoa kwenye ulingo wa siasa? Au wapenzi wa chama tawala wameshindwa kuusoma mchezo wa siasa? Huu mchezo hautaki hasira wa mabavu ya dola ila unataka mkakati wa kujivunia mazuri yanayo fanywa na Utawala Chama tawala kukaa kimya na kucheza ngoma za upinzani ni sawa na huyu ☝ aliye kabidhiwa brifkes ya ofisini akaringa bila kujua kuwa imetoboka. Amkeni mpige ngoma wapinzani wacheze, fanyeni kama Magoiga SN.

Asanteni

Leave a Reply