Andiko langu lililopita nilijaribu kuwatahadharisha Upinzani juu ya kupooza kwao katika siasa za sasa. Niliwakumbusha na kuwa sihii wabadili mbinu na mikakati yao juu ya kuendesha siasa zao na hata kuleta maendeleo kwa wananchi walio wachagua.
Leo nimeona video inayomuonesha G.Lema (MB) mbunge wa Arusha akitoa msimamo juu ya kadhia aliyoipata kutoka kwa Mkuu wake wa mkoa RC M.Gambo akisema:
“kuanzia leo ikitokea kiongozi wa upinzani amedhalilishwa na ikiwa protocal na itifaki za serikali haikufuatwa kwao hata ikiwa ni mbele ya Raisi basi watafanya TIT FOR TAT hapo hapo.”
Kwa maana yangu binafsi nilivyo ielewa kauli hii ni kwamba Mbunge wa Arusha anakuja na mkakati mpya wa kujibu mapigo ya papo kwa papo hata kama itakuwa ni mbele ya Raisi as long itifaki na protocal za serikali hazikufuatwa kwa viongozi wa upinzani kama alikuwa anastahili.
Hasara za mkakati huu..
1. Ikiwa itafanyika hivi mbele ya wageni kama ilivyofanyika Arusha basi huu utakuwa ni Uhuni wa kulaani.
2. Mkakati huu bado hauoneshi nidhamu ya viongozi wetu na inaweza kuwachukiza wananchi ambao ni wastaarabu.
3. Yaweza kusababisha serikali kukwepa kushirikisha viongozi wa upinzani katika hafla mbalimbali kwa hofu ya kutokea vurugu na aibu kwa jamii.
Faida za Mkakati huu.
1. Ikiwa itafanywa kwa ustadi mkubwa na matokeo yakawa ni makubwa kwa jamii basi yaweza kuwa ni moja ya mkakati mzuri wa kuondoa kadhia hii ya kutengwa na kubezwa kwa upinzani. Maana serikali zetu mara nyingi hutatua tatizo baada ya kuona matokeo ya tatizo.
2. Ikiwa itafanywa vizuri basi yaweza kuwa ni “KIK” ya kisiasa na inaweza kuteka vyombo vingi vya habari. ukweli ni kwamba chakula cha mwanasiasa yoyote ni kutoka kwa habari zake nzuri na za harakati kuonesha ana tetea wananchi wake kama serikali ya sasa inavyofanya.
#Mytake.
Ni vizuri kubadilika kila mara ili adui yako asikufahamu vizuri lakini tumia mbinu zenye matokeo makubwa kwa wakati mmoja ili kulinda nyakati zingine. Mbinu hii ni ndogo sana ukilinganisha na tatizo la demokrasia na siasa zilizopo sasa, kuna haja ya kuja na mbinu nyingi zaidi mipya itakayo shitua ulevi wa madaraka mnao ulalamikia. Endeleeni kufikirisha vichwa vyenu maana kuchagua kuwa Mpinzani katika nchi yetu sio raha hata kidogo, Ni Mzigo mkubwa wenye kuhitaji mapambano ya ziada ili kufikia malengo.
asanteni.