TUAMINI LIPI KATI YA HAYA?
1. Report za BOT zinaonesha kuna mdororo mkubwa wa uchumi wa nchi. hali inayopelekea vichochezi vingi vya uchumi wa nchi kuanguka kama vile utalii, taasisi za fedha, sector ya usafirishaji na uchukuzi, sector ya viwanda na kilimo.
2. Wanasiasa na viongozi wetu wanapinga kudorora kwa uchumi wa nchi wakituaminisha kuwa fedha zipo ila ni lazima ufanye KAZI. Wanasema eti wale wanao lia njaa ni wapiga dili waliokosa dili za pesa chafu.
3. Mtaani haijulikani nani ni msafi au mchafu, nani ana fanya kazi au mfanya biashara, nani ni mtumishi wa umaa au wa sector binafsi ila wengi wao kama sio wote wanalia njaa ya kuadimika kwa fedha mtaani.
Sasa sisi ambao tupo tupo tu tuamini lipi?