Katika pita pita yangu huko Facebook nikakutana na huo ?ujumbe/ angalizo!……… Nimuhimu sana watu kujifunza kuwa kila kiumbe chenye uhai kina hisia na kinafaa kuheshimiwa!! Katika jamii yoyote ile iliyo staarabika, wenye watu wenye kujitambua na yenye busara huwezi kuta hata siku moja wakiita binadamu kulinganga na ulemavu wao, rangi zao, au mapungufu yoyote yale walionayo! Hata Adam na Hawa baada ya kukaidi amri ya Mwemyezi Mungu hakuwaita majina tofauti na yale walio nayo! Sasa sisi kwanini tunapenda ku label watu? Tena watu wengi sana in Bongoland wanfikiria its OK to label people as the society has “legalized” it!!! ……………….. Hili angalizo linanikumbusha my childhood life!……… Nilipokuwa mdogo nilipata matatizo ya meno ikabidi nitolewe meno yote ya juu na baadhi ya chini. Kwabahati mbaya meno yangu yalichelewa kuota mpaka nakaribia darasa la pili (Std 2). Sasa basi yani harassment that I used to get at home was huge compared to what other students teased me at school!! Yani nilikuwa hata nashindwa kuongea na ndugu zangu saa zote nikitaka kufungua mdomo niseme kitu utasikia mtu ananicheka na kuniita “mapengo”!! Yani hata saa nyingine mtu badala ya kukuita jina lako utasikia anakuita “wee mapengo”!! Halafu kana kwamba hiyo ilikuwa haitoshi nikawa nafananishwa na bibi yetu fulani (sasa hivi ni marehemu) huko kijijini Utegi ambaye alikuwa na matatizo ya meno hivyo meno yake yote yaling’oka (hakuwa na meno). Napia alisadikika kuwa na sura mbaya!!! Hivyo badala ya kuniita jina langu wakawa wananiita jina la huyo bibi pale walipo ona nimekosea kitu au wakitaka kuniudhi or just to make funny of me kwani walikuwa wakisema I look exactly like her!!! Trust me, hivi vitu vinauma sana tena sana especially when you are just trying to enjoy your childhood like other children and all you can think is someone watching my mouth? So am I really ugly as they say it?!!………Honestly these type of abuses need to end!! It’s not cool, not funny, it is wrong in all levels!! It kills people’s self esteem!! ……….. kitu ambacho sijakielewa kwanini TAS waone nisawa kuitwa “albino” ? Lakini si “zeruzeru”? Kwani kiswahili cha “albino” ni nini au mie ndo sielewi?!……………. Anyway, regardless, we have to respect and honor their wishes!! The name is offensive to them then people need to stop using it whether unaelewa kwa nini au la! Jukumu lako nikuacha kulitumia na si kujua kwanini!! Na ujifunze kuwa na UTU wa kuwaita watu kwa majina yao halisi na sio kutokana na ulemavu wao!!