Tusibeze uthubutu wa mtu tena kijana wa kawaida ambaye bado hajawa nguli katika siasa wala uongozi. Tumpe muda maana hiyo vita aliyoichagua ni vita ngumu inayo hatarisha maisha yake. Huyu ndiye kiongozi pekee wa kumuombea tofauti na wengine. Huyu yupo kwenye vita ambavyo kama wewe ungepewa fursa ya kuwa mkuu wa mkoa huu basi inawezekana ungeshindwa kudeal hata na dagaa kama Makonda alivyoanza. Tumpe moyo mkuu na kumwombea kwa Mungu apigane vita vizuri, naamini hata kama hatashindwa kufikia mafanikio tunayoyataka lakini atakuwa amefanya sehemu flani ya kutatua uovu huu ambapo mwingine atakaye jitokeza katika vita hiyo ataanza alipo ishia Makonda. Hatuwezi kunyamaza kimya kwa tatizo kubwa kama hili na asitokee hata mtu mmoja wa kusema hata kidogo alafu tukajiona tupo samala, Laa hasha kukaa kimya ni kuhalalisha uwepo wa tatizo. Vijana wengi wana angamia na kupoteza nguvu kazi na vipaji kwa sababu ya kukaa kimya na hata kubeza jitiada hizi ndogo zinazo chukuliwa na Makonda. Tuungane na Makonda kutenda na kufikiri tofauti kwa kuchukua hatua za kutenda badala ya malalamiko na matamko yasiyo isha wala kusaidia jamii. Tuweke siasa pembeni kwenye majanga makubwa kama haya ili kuunga kila hatua zitakazo chukuliwa na yeyote katikakupambana na Tatizo hili.
Asanteni..
Sabato Njema wana wa Mungu.