Kila mtu hapa dunia amejifunza kitu fulani kwa maana ya kuwa hakuna aliyezaliwa akijua kituchochote bali ni kwakujifunza. Mfumo ya kujifunza ipo ya aina mbili formal (mfumo rasmi) na informal (mfumo usio rasmi). Haijalishi ni mfumo gani umetumia kujifunza kwani yote lengo lake ni kutoa elimu. Na wale watu wanao tumika kutoa elimu wanaitwa walimu kwasababu wanakuelimisha.
Labda nifafanue kidogo kwa wale ambao watajiuliza tofauti ya mfumo rasmi na mfumo usio rasmi. Mfumo rasmi wa kujifunza ni kujifunza kitu au kupata elimu ya kitu fulani kupitia mlolongo wa ngazi na njia tofauti ambazo zimeainishwa kulingana na mfumo wa elimu husika kutoka katika mamlaka ya elimu husika. Na elimu ya mfumo usio rasmi ni kujifunza vitu au kupata elimu kwa njia ambayo aitambuliwi kulingana na mamlaka husika. Kwa mfano mtu anaweza kua mpishi mzuri kwa utundu wake au kufundishwa na bibi yake, mtu wa hivi atakuwa ameelimika katika mapishi lakini sikuwa amekwenda shule ya mapishi. Mtu kama huyu anaweza akafundisha watu mapishi yake lakini hawezi kufundisha watu juu ya chakula bora kwani kuna elimu furani kuhusu vyakula ambayo hana japo anajua kupika.
Turudi kwenye mada yetu. Jamii haswa za Kiafrika zimekuwa na tabia ya kutokuheshimu walimu bila kujua kuwa walimu ni moja ya nguzo muhimu sana katika jamii. Binafsi nafikiri walimu ni nguzo ya pili ukitoa familia (wazazi) ambayo nafikiri ni nguzo ya kwanza muhimu katika jamii yoyote ile. Walimu wanachukua nafasi ya wazazi wetu pale tunapokuwa mashuleni kwani hawa hutufunza maadili na maarifa muhimu ya jinsi ya kukabiliana na maisha. Walimu si tuu wanatufunza kuandika bali tabia zao na mienendo yao inachangia sana katika ukuwaji wa tabia zetu na maendeleo ya nchi.
Yatupasa kuwapenda na kuwaheshimu sana walimu wetu. Tuwaonyeshe umuhimu wao na thamani yao kwa faida ya maendeleo ya taifa letu.
Tupatapo nafasi si vibaya kuwajulia hali zao na kuwashukuru kwa mchango katika maisha yetu binafsi.
Kufundisha ni karama si kila mtu amezaliwa nayo. Japo siku hizi techology inafanya kila mtu aweze kufundisha kwa njia moja ama nyingine. Kwani unaweza jifunza kwa kusoma status ya mtu au kwa kuangalia maisha ya watu fulani au familia kwa kutumia television au social media. Napenda kumpongeza sana schoolmate wangu toka Kowak Girls kwa kuamua kutoa mchango wake katika maendeleo ya taifa letu kwa njia ya elimu. Wanasema uwalimu ni wito, kwani ni kazi ngumu sana kumuelimisha mtu haswa watoto. Uvumilivu na busara ya hali ya juu inahitajika sana. Ubarikiwe sana Furaha.