Kuhojiwa kwa vingozi wa jamii zinazo tuzunguka siyo jambo la kushangaza au la ajabu kwani halikuanza leo wala jana. Ukichukua mamlaka ya kuongoza watu basi lazima uwe teyari kuhojiwa kwani wana haki ya kufanya hivyo. Japo saa nyingine wanaokuuliza wanaweza wakakukwaza na maswali yao lakini kama kiongozi unakuwa hauna haki ya kuwakataza au kuwazuia kukuhoji pale wanapojisikia kufanya hivyo.
Kunawengine wanaweza kuhoji siyo kwamba hawajui ukweli, la hasha! Ni watu wenye ajenda zao mbovu, hivyo watakupa maswali ambayo wanajua majibu yake lakini wewe kama kiongozi inabidi utumie hekima yako kuwajibu na kutoa ushahidi ikabidi.
Kwa mfano, tunaona jinsi Yesu alipokuwa jangwani akifunga na kuomba, shetani alimuhoji “....kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate.” Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu.’” Yesu alimjua huyu ni Shetani lakini kwakua alikuja kuwakomboa watu wote hivyo alitumia hekima yake ya juu kumjibu, bika kumzuia kumuhoji.
Shetani aliendela kumuhoji Yesu kwa siku arobaini ambazo Yesu alikuwa Jangwani. Embu tafakari, pamoja na Yesu kushinda na njaa kila siku lakini bado Shetani alikuwa mbele ya uso wake akimpa maswali kila siku na Yesu akamuacha amuhoji. Siyo kwamba alishindwa kumnyamazisha Shetani au kumfukuza, hapana! Alimuacha Shetani atumie uhuru wake! Nayeye kama Mfalme atatumia hekima na mamlaka yake kumjibu.
Watu wenye tabia kama hizi za Shetani wapo miongoni mwetu na katika kila jamii. Niwajibu wa viongozi wetu kujua kua wapo kutumikia watu wa aina zote waliopo ndani ya jamii husika, hivyo hata wakija na maswali ya kukebehi au kukera ni wajibu wao kuwajibu kwa kutumia hekima na mamlaka waliyo nayo. Si busara kutishia watu wanapohoji viongozi, hekima itawale siku zote.
Mungu atusaidie.
Related