UKIMWINDA SANA MJUSI ANAGEUKA NYOKA.
Huu ni msemo wa wahenga ambao uhalisia wake unaonekana mara chache porini lakini hutokea sana kwa maisha ya binadamu. Naamini kuna watu walisha wahi kumwinda mjusi kipindi walipokuwa watoto na katika kumwinda mjusi gafla walipo toa jiwe wakakutana na nyoka, inapofika hapo lazima hali ya hatari itatokea.
Naiona nchi yangu kwa mbali inakaribisha hali ya hatari. Mkuu wa kaya alianza kuongoza nchi yake kwa misingi ya sheria huku akijitambulisha kuwa yeyeni mkali kwa maneno na matendo yake. Baada ya kuwa mkali sana watoto wakaanza kulalamika huku wakionesha kuto ridhika na maamuzi ya baba. Watoto wakaanza kumwinda baba kwa vifungu vya sheria huku wakimtangaza baba kuwa ni dikteta. Na kwa jinsi baba alivyo na msimamo, hakuwahi kurekebisha makosa yake hasa yale yaliyovunja sheria na hata kuonesha upendeleo wa wazi wazi huku akiwagawa watoto wake kwa kauli na matendo.
Kwa sasa hali imekuwa mbaya maana watoto wameanza kumkana baba yao kwa kutumia mama yao Katiba. Wana mshawishi mama yao (Katiba) awaoneshe baba mwingine kwa kutamka kuwa huyu sio baba mzazi na wamtafute baba mwingine.
Kwa hatua ya mawindo yalipo fikia, nawaona watoto wanahisi wanaye mwinda ana fanana na Mjusi hivyo wanaongeza jitiada za makusudi wakiamini nguvu za mjisi zipo mkiani na wala sio nguvu za kuogopesha kiasi cha kutaka kumtoa kwenye pango lake.
Lakini nahofia sana hasira za baba, baba akikasirika na kuamua kutumia nguvu zake basi anaweza akawalazimisha watoto kuendelea kuitwa baba kwa kumtishia mama na hata kuwa adhibu vikali watoto wanao kwenda naye kinyume, na akiona bado anapingwa basi anaweza kumbadili mama mwingine na kufunga ndoa ya kudumu. Kwa hatua hii, baba hatakuwa tena mjusi bali atakuwa ni nyoka.
Kwa sasa watoto wajiandae kukutana na nyoka katika mawindo yao, wasidhani wataendelea kukutana na mjusi walie mzoea kumwinda. Wajiandae na plan B,C na hata C ya kukutana na Nyoka.
By the way baba amesha geuza kichwa bado mkia wa nyoka tu aanze mashambulizi kwa watoto wanao winda.
“Be careful and watch it” Mkuu wa kaya 24/3/2017