“Ukiomba mvua lazima ukubali kukutana na tope pia, hiyo ni sehemu ya mvua. Jana imepita hakuna ajuaye kesho, kitu pekee ulichonacho ni SASA ishi kutumia sasa kwasababu huna uhakika na kesho. Stay present.”
Nimeupenda sana huo ujumbe toka kwa mjasilia mali na Mwalimu Vumilia Sassi. Ujumbe unamaneno mepesi sana lakini maana yake ni nzito! Wengi tunaomba Mungu atuletee mvua kwenye maisha yetu / mashamba yetu ili mbegu tulizopanda au tunazotaka kupanda ziote! Lakini wakati huo huo hatutaki kuona wala kujanyaga matope!
Hivi tutaombaje mvua halafu hatutaki kuona udongo umeloa? Sasa hizo mbegu zetu zitaingiaje chini ya aridhi na kuweka mizizi yake kwa chini kama udogo ni mgumu haulimiki! Ninachotaka kusema ni kwamba ukitamani na kulilia mafanikio yako binafsi basi lazima uwe teyari kukutana na changamoto mbali mbali. Jinsi utakavyo weza kudili na hizo changamoto ndio itakupa picha halisi ya mavuno yako (will determine your success). Kama hutaki kudili na matope basi usiombe mvua kwani hauko teyari kulima! Oprah Winfrey aliwahi kusema kuwa kama hauko teyati kuongelewa basi hauko teyari kwa maendeleo!
#Ukiomba Mvua Lazima Ukubali Kukutana na Tope