Hicho kichwa cha ujumbe / somo la leo nimetoa kwenye ule wimbo wa ‘Yamoto Band’ lakini sipo hapa leo kuzungumzia huo wimbo wala band. Nimeyachukua tu kwasababu yameendana na ujumbe wangu!
Unasema humpendi mtu fulani (labda tuchukulie Zari, the Bosslady) lakini anafungua FEKI AKAUNTI ya social media kila siku haipiti hata masaa sita bila wewe kuangalia ame post nini?! Wewe unakichaa na ninakuita mwendawazimu!! Haiwezekani mtu mwenye akili zake timamu anayejitambua akaishi maisha ya kujidanganya na kujiumiza hisia zake mwenyewe!! Wewe lazima utakuwa punguani!! I’m sorry, but no thanks!
Hivi unajua ni ngumu kiasi gani kuishi maisha ambayo yanaumiza hisia zako? Kuishi maisha yanayo kupa hasira na chuki na watu wengine tena ambao hata huwajui undani wao zaidi ya kile unachokiona kwenye social media! Sasa tabu yote hiyo yanini? Ni kitu gani kinakufanya unaishi maisha yanayo kutesa? Kumfatilia mtu kwa kila kitu afanyacho hiyo ni zaidi ya ajira? Na kwenye ajira kuna mapato mtu anatakiwa kupata baada ya kazi ngumu, sasa wewe ni mapato gani unapata baada ya kumfatilia? Maana sio tu unapoteza muda wako, bali pia umetumia fedha yako kulipia internet, umeacha kufanya jambo lingine ambalo kwa namna moja ama nyingine lingekusaidia kuona mbele zaidi, yote hayo hukujali ukaamua kumfuatilia mtu usiye mpenda?! Halafu bado utatoka hapo unapoteza muda kumsengenya na wendawazimu wenzako ?? Wonders shall never end!
Mimi binafsi sina muda wa kumfuatilia mtu ambaye ananikwaza, yani sikufungulii account fake hata mara moja nakupa block nasonga mbele! Embu nawe jaribu hii njia ninayo tumia mimi huwenda ikakusaidia. Hakuna haja ya kufungua account Feki kumfatilia mtu usiye mpenda! Maisha ni mafupi sana sasa usipotaka kuwa wewe katika hualisia wako ukaishi maisha yako sasa angali unapumua lini utaishi na watu wakakujua kua huyu ni fulani?!
Kamwe kataa kuishi chini ya kivuli cha mtu mwingine! Life is too short to blend in or to be someone else! Be real! Be you! We only live once!