Unapokutana na mtu mwenye mafanikio usimuombe pesa. Muulize amefanyaje kufikia hapo alipo!
“When you meet a person with means, a person that is well-off you think is successful that you always wanted to be; don’t go there asking for money” Hayo ni maneno yake Comedian na TV host Steve Harvey kwenye Oprah Master Class. Master Class ni show ambayo watu wengi waliofanikiwa katika nyanja mbali mbali za maisha wanaelezea mafanikio yao kwa undani zaidi toka walivyokuwa wadogo mpaka walipo fikia. Changamoto zipi walipata, vipi waliweza kuvumilia, kumudu hizo changamoto, na hata kufanikiwa bila ya kukata tamaa.
Unapopata nafasi ya kukutana na mtu au watu ambao unawaangalia kama “role mode / icon” katika maisha yako usiwaombe pesa waombe wakuelimishe nini walifanya kufikia hapo walipo. Watu wengi wapo wepesi wa kuomba pesa kwa mtu aliyejaliwa kuwa nazo kwa ajili ya kujikimu na hiyo shida aliyonayo. Nautakuta muda mwingi shida hiyo haiishi ni kaituliza tu kwa muda. Hii yote nikwasababu wengi tunapungukiwa hekima ya kujua kuwa ni kheri mtu akupe elimu ya maisha ya nini alikifanya mpaka kufika hapo ili uone kama na wewe unaweza tumia njia hiyo kufikia malengo yako au kujikwamua kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Au utakuta wengine tumepingukiwa hekima ya kuona mafanikio ya watu ni maovu mbele zetu nakuanza kutafuta njia ya kumuangusha bila kujua kuwa anguko lake ni maafa kwako pia. …….Hivyo tuwe waelevu kama nyoka na wenye hekima kama Solomon ili tuweze kujifunza kutoka kwa wengine haswa ambao tunaona wana tija katika maisha yetu.
Pale watu wanapokukatisha tamaa wewe piga moyo konde usiwasikilize. Kwanza mimi kwa experience yangu binasfi watu wengi wenyekukatisha watu tamaa ni watu ambao hawajiamini na pia hawapendi kuonekana kuwa wao wameshindwa katika kufikia kile wakitakacho hivyo hamna la zaidi zaidi ya kupiga makelele ili uwe muoga. Wakati ukweli wanatamani wangekuwa na ujasiri kama wako. Utaona wanakuja na maneno mengi ya kejeli ikishindikana wataingilia personal attack “hajaolewa”, “mnene”, “hana nywele”, “mbeba mabox” yani ukishaona mtu anaenda kwa personal attacks jua maumivu yamemuhelemea ??
.
.
Nasiku hizi social media, basi watatafuta kila event au tukio lenye viongozi waende kupiga picha ili warushe kwa Facebook / Instagram basi tu ufikirie kuwa there really happy and making it, wakati rohoni wanatamani wawe na kipaji au nafasi kama yako. ?? Wanasaikolojia wanasema mara nyingi watu wanao ongelea wengine vibaya muda wote huwa kuna mambo ambayo hayopo sawa kwa upande wao sasa kwasababu hawataki watu wajue huo upande wao hauwapendezi, basi dawa inakuwa ni kugeuza attention kwa wengine! Na huo ndio ukweli! Wewe usikate tamaa na mapicha yao! Nawala usiache mashauzi yao yasio na kichwa wala miguu yakuumize au yakutoe kwenye malengo yako.
Mimi nilivyoanza hii blog yangu nimetungiwa uzushi wa kila namna; ooh huyo muhuni anatafuta mwanaume, huyo FBI, huyo kada wa CCM (utafikiri walishaniona na kadi ya CCM au nimevaa gwanda la CCM ??), mara anatafuta umaaharufu, mara mkabila, mdini, yani maneno mengi mno wengine wakadiri hata kwenda kwetu kuchunguza maisha ya kwetu nakuja kuongea kwenye magroup yao. Mara kazi yake kudhalilisha watu. Eti huyo anagombania mali za wazazi wake ?? Wengine wakazunguka kuwaambia watu wasiweke picha zao kwa hii blog. Yani hayo yote walifikiri nitaacha kublog!! Lakini nipo hapa and I’m here to stay! Mimi najua ninachofanya na ninako kwenda hivyo sijali. Waliokua wanasema mimi kazi yangu ni ku copy and paste ndio hao hao wanakosa raha kwani wanatamani niwaweke humu kwa blog yangu nami hata habari nao sina ?? Ni maumuvi makali sana wanapata. Wewe songa tu, wakikwambia huwezi wambie wewe ni nani hata useme hivyo!
Kitu kingine usiamini kila rafiki. Yani ukiona mtu ambaye ni rafiki yako anachukia maendeleo au mafanikio ya mwingine achana na huyo rafiki mara moja. Kwani inamaana wewe ni rafiki yake Kwasababu haujamzidi kimaendeleo lakini siku ukitaka kunyanyuka atakuwa wakwanza kukuangamiza! Niamini nimeyaona!
Siku zote kuna mtu mmoja ambaye atakuelewa na ambaye atakuwa yupo teyari kukusaidia kufikia malengo yako. Mungu huwa hamtupi mja wake! Kama nipesa basi huyo mtu anaweza kusaidia, kama ni mawazo yanini ufanye ili ufanikiwe basi huyo mtu atakuwa yupo tayari kutoa ushauri. It means that person believes in you and truly cares about you! When it looks like nobody cares trust me someone is out there who really cares about you! Muda ukifika Mungu atamleta kwako. Usikate tamaa!
**Imeandikwa na Alpha Igogo**
**#TBT #Sept.2017**