Wahenga wanasema ukiona kwako kwaungua basi jua kwamwenzio kwa teketea! Yani kama wewe unafikiri unamatatizo au umepitia shida na vizingiti katika maisha basi kajaribu kummwambia jirani yako akusimulie yakwake! Utabaki mdomo wazi! …….Embu sikiliza history ya maisha ya Wasia Maya jinsi alivyokuja hapa Marekani, mambo yalimkuta na mitihani aliyopitia utachoka mwenyewe! Kuna wakati alikuwa kwenye koma kwa siku 30, kafungwa jela kwa miezi 27, na tamaa ya kufanikiwa kwa njia za mkato ambazo zilipelekea kutaka kuuza madawa ya kulevya!
Yani the devil! Wewe mwenzio katoka kutumikia miezi 27 jela bado tu unamuweka kwa wishawishi vya madawa ya kulevya?!! Lakini kama roho wa Mungu bado yupo ndani yako kwakweli hawezi kukuacha ukaangamia. Atakugusa kwa mguso wa pekee ambao utatosha kubadili njia zako!
“Sasa nina amani……… Nipo comfortable with my life”! Hongera sana kaka Wasia Maya, najua hii story yako itagusa vijana wengi na kuangalia maisha katika njia tofauti. Ubarikiwe sana.