Katika mfumo wa unyanyasaji au aina za unyanyasaji kuna unyasaji wa aina nyingi kwamfano physical abuse, sexual abuse, emotional / psychological abuse, gender abuse, financial abuse, power / position abuse na vile vile kuna “spiritual abuse” au kwa lugha ya Kiswahili unaweza sema ni unyanyasaji wa kiroho! Dini ni imani, na imani huwa kila mtu anauwamuzi wake wakuamini au kuto kuamini dini au maandiko bila kulazimishwa au kushurutishwa na mtu yoyote yule. Hii ni kwa dini zote waislamu kwa wakristo, sisi wajibu wetu ni kuwafundisha watu neno la Mungu lakini hatuna haki ya kuwalazimisha au kushurutisha mtu aamini kile wewe unacho kiamini hata kama wote ni wa dini na dhehebu moja. Wokovu ni wa mtu mmoja mmoja na kila mtu kwa wakati wake. Kama mtu hajaamini kile kitu ambacho wewe unadhani ni sahii na anahitaji kuamini basi muache, wewe bado utahesabiwa thawabu Mbinguni kwani umefanya sehemu yako. Ipo siku katika njia ya pekee roho atamwingia na kuamini (kama kweli ni sahii hicho unachotaka aamini) lakini siyo kwa kulazimishwa.
Turudi kwenye mada yetu ya unyanyasaji wa kiroho “spiritual abuse.” Kuna baadhi ya watu ambao kwasababu zao binafsi au kutokana na roho mchafu kuwatawala huwa wanatumia neono la Mungu kunyanyasa wengine na hiyo ndiyo inaitwa unyasaji wa kiroho. Yani hawa si wengine bali ni Mbwa Mwitu walio vaa ngozi ya Kondoo! Mtu anatumia kifungu fulani au neno fulani kutoka kwenye maandiko matakatifu kunyanyasa wengine au wale walio karibu naye. Kwa mfano; Biblia katika kitabu cha Wafeso 5:21 kinasema “Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu” sasa basi unakuta mwanaume fulani mwenye roho ya Farao (roho ya kishetani) amebahatika kujua hilo fungu sasa basi anatumia kumnyanyasa mkewe eti kwa madai Biblia imesema umtii?! Mfyuuuuu! Kumtii mtu siyo kuwa mtumwa wake, kumtii mtu siyo kujivua utu wako kwa ajili yake, kumtii mtu siyo kumgeuza Mungu wako! Eti kama mimi leo hii niwe na mume ambaye atanikataza nisiende kanisani siku ya Sabato (Juma Mosi) na anataka nimtii kwasababu yeye ni muwe wangu?! Ishiii! Umenitowa wapi mpaka uje unikataze nisiabudu siku ya Sabato? Mara nyingi unakuta yule anayefanyiwa huu ukatili hana nguvu au ujasiri wa kumwambia huyo katili hapana hivyo si sahii kwahiyo huwa wanaendelea kukaa katika unyanyasaji huo mpaka wanakuwa psychologically affected. Mtu anakuwa anaishi kimwili lakini kiroho amekufa kabisa! Kunamifano mingi sana ya unyanyasaji wa kiroho, na mwingine ndo huu ambao hawa watu wanaojiita “conservatives” yani watu wenye msimamo mkali kuhusu neno la Mungu. Hawa wenyewe wanatumia kipengele kile cha Biblia kisemacho ‘nendeni mzaliane muijaze dunia’ (Mwanzo 9:7) kutaka wanawake waache kutumia uzazi wa mpango eti ni dhambi kwasababu wanatakiwa waijaze dunia! Yani huu ni mfano hai wa typical spiritual abuse ambayo inafanywa na baadhi ya watu haswa wanaume. Wewe kama unaamini kwamba mwanamke anatakiwa kuzaa kila Christmas basi jaribu wewe kubeba mimba na ufanye hivyo sio watoto wa wenzio! Wote tunajua Mungu anataka tuijaze dunia lakini hakusema wanawake wawe wanabeba mimba kila mfungo wa Ramadhani!! SMH! Na ndio maana Mungu aliumba wanawake wote lakini sio kila mwanamke anauwezo wa kuzaa mtoto au watoto wengine wamezaliwa ni tasa au wagumba na hawa wote wameumbwa na kuletwa duniani na Mungu huyo huyo aliye tuagiza tuijaze dunia! Sasa wewe ni nani wa kulazimisha watu kuzaa bila kikomo? Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu, ni Mungu wa mipangolio sasa kanini wewe unataka wanawake waishi bila mpangilio wa uzazi?
Wajibu wetu kwa sisi ambao tunamwamini Mungu ni kufundisha neno la Mungu, lakini uwamuzi wa kuamini na kufuata maagizo ya Mungu ni ya mtu binasfi! Na kwasisi wakristo kitu kikubwa ambacho Mungu ametuhasa tufanye ni kufundisha upendo na ukuu wa Mungu hayo mengine ni kazi ya Roho Mtakatifu. Kama watu wangekazania kufundisha upendo, tupendane kwa dhati bila kubaguana kama jinsi Yesu Kristo alivyo tupenda sisi basi hii dunia ingekua ni mahala pazuri na salama sana kwa kila kiumbe kuishi. Lakini binadamu wa leo wameamua kuwa wachungaji na watoa hukumu kama vile wao ni Mungu! SMHH! Watu wanaotumia neno la Mungu na imani zao vibaya wapo sana wengine ni dungu zetu, rafiki zetu, jirani zetu, au niwatu tunaowasoma na kuwaona kwa mbali hata kwenye Biblia wapo na Mungu huwa apendezwi nao hata kidogo. Umeshawahi soma kisa cha Mfarisayo na mtoza ushuru? Kama bado nenda kasome Luka 18: 8-14. Yap! Sio wote waniitao Bwana Bwana watakao uwona ufalme wa Mungu! Unaweza ukaona mtu kama mimi hapa ni mdhambi sifai kwasababu tuu labda nipo free kuongea kile ninacho kiwaza au maoni yangu bila woga bila kujua kuwa wale wanao onekana wapole na wanyeyekevu mbele za watu nyuma ya pazia ni wachawi, wezi, waseng’enyaji, wachonganishi, waongo, n.k kwahiyo tusilazimishe watu wawe kama sisi kwasababu hakuna aliye na huwakika kuwa yeye ni mkamilifu. Na wengi wanaonekana weupe kumbe ni kwa inje tuu ndani mmh!
More readings: “Spiritual abuse occurs when someone in a position of spiritual authority–the purpose of which is to ‘come underneath’ and serve, build, equip and make God’s people more free–misuses that authority by placing themselves over God’s people to control, coerce or manipulate them for seemingly godly purposes which are really their own.”
Emotional Abuse and Your Faith: “Both men and women are called to submit to God first and then to each other (Eph. 5:21; James 4:7). This submission to God and one another constitutes the biblical basis of the marriage covenant. In evangelical circles, the neglect of this teaching, or the misinterpretation of it, has led to an erroneous view of submission. The submissive role is assigned to the wife, while the husband fails to submit to Christ in his role as the head of the home. Headship is then defined as the man being in a higher position in the home, apart from the teaching of Christ, and in practice gives him the authority to rule as he desires. When a woman is not seen as being equal to her husband in dignity and is not treated with love and respect, people have distorted the scriptural view of marriage“
Great blog you have here but I was wondering if you hav any forums that cover the same topics discussed in this article? I’d really love to be a part of group where I can get feedback from other knowledgeable people that share the same interest. If you have any recommendations, please let me know.
Bless you!
Not yet my dear but eventually I will. Just stay tuned!