Baadhi ya watu haswa sisi Watanzania huwa tunatabia yakutokupenda kuwa wadadisi wa jambo au mambo matokeo yake our ignorance is very High! Yani tupo radhi tuamini katika uongo au majungu / umbea kuliko kuchukua muda wako na kukisoma / chunguza kitu wewe mwenyewe ili uwe na huwakika wa kile unachokiongea. Utakuta mtu anahadithia kitu wewe utaamini ni kweli ameiona mwenyewe kwa macho yake au amesikia yeye mwenyewe kwa masikio yake kumbe naye kasimuliwa na rafiki yake ambaye nae huyo rafiki kasimuliwa na mtu mwingine ?♂️?♂️
Hii tabia kutopenda kuchukua muda wetu na kujifunza jambo fulani au kufatilia habari fulani bila ya wewe kuweka uongo wowote ndio imefanya Watanzania wengi wanapenda majungu sana, wanaamini ili uweze fanikiwa basi lazima umuharibie mwingine haswa kama yupo kwenye biashara au jambo ambalo na wewe unafanya! Inasikitisha sana kwani kwa hii tabia maendeleo ya taifa letu yatahitaji dictator!! Juzi niliamua kwenda kuangalia hili 'karai' kubwa ambalo limeletwa hapa Houston, Texas kwenye chuo cha sanaa. Hili karai limetengenezwa Ulaya likaletwa hapa. Ni urembo wa aina unao vutia sana. Katika mji wa Chicago nao wanao 'karai' kama hili limetengenezwa na mtu mmoja. Ila la Chikago limeinamishwa (kama inavyo onekana kwenye picha ya pili kutoka juu) hivyo watu wanaweza ingia katikati ya hili 'karai' nakupiga picha nzuri sana kama anavyoonekana mwanangu hapo pichani ☝ na pia tizama picha ya mama yangu na mdogo wangu hapo chini ? Hizo picha zilipigwa miaka 6 iliyopita kwenye hilo karai la Chicago. Kwa maoni yangu binafsi mimi napenda ya Chicago zaidi kwani imewekwa vizuri kwa watu kupiga picha na kitendo cha kulazwa chini imefanya hiyo sehemu iliyoingia ndani kuwa sehemu ya kivutionzaidi cha kupigia picha. Halafu maua na urembo ulioko pembezoni unahakisiwa na hiyo karai ambayo pia nikivutio. Nilichotaka kuwaambia Watanzania wenzangu ni kuwa usiogope kushangaa! Hakuna njia nzuri ya kujifunza kitu kama kushangaa. Tena ukimpata mtu anayekupa maelezo basi wewe zidisha kushangaa ili akupe maelezo zaidi. Wanaopenda kushangaa ndio wajanja!