Ilikuwa kawaida yake kulala na nyoka wake, na haya ndiyo yaliyomkuta. Hii ni hadithi ya kweli kuhusu mwanamke aliyekuwa na nyoka wake aina ya chatu aliyempenda sana. Nyoka alikuwa na urefu wa mita 4, aliishi naye kwa muda mrefu na siku zote nyoka yule alionekana mwenye afya. Hata hivyo, nyoka alianza kukosa hamu ya kula kwa wiki kadhaa jambo lililomnyima raha mama yule kwani alihisi nyoka wake ni mgonjwa. Mama alijaribu kumpa kila kitu alichoweza ambacho nyoka wangependa kula lakini haikusaidia kitu, mama yule alikata tamaa na aliumia zaidi kwakuwa alimpenda sana nyoka wake. Hatimaye mama yule aliamua kumpeleka nyoka wake kwa daktari wa mifugo. Daktari alimsikiliza yule mama kwa makini kisha akamuuliza , ” Je, unalala na nyoka wako wakati wa usiku? anapenda kulala karibu zaidi na wewe na kujipimisha urefu wake na wako? “
Mama kwa matumaini makubwa alisema, “Ndiyo! Ndiyo! anafanya hivyo kila siku na inanipa huzuni kwa sababu nahisi kuna kitu anatamani kuniambia lakini hawezi na Mimi pia nashindwa kumuelewa hivyo nakosa namna ya kumsaidia ili ajisikie vizuri kama siku zote “
Daktari akampa jibu la kushtusha moyo ” Mama, chatu wako si mgonjwa ; … “Ndiyo, chatu hakuwa mgonjwa, amekuwa katika maandalizi ya kumla mama yule. Daktari akaendelea, “Kila wakati anataka kukaa karibu na wewe, kujikunjakunja mwilini mwako na kukutambaa kila muda, lengo lake ni kupima ukubwa wako na kuangalia namna gani utakuwa mzuri mlo wake. anajilinganisha kujua jinsi gani utawa mlo mkubwa kwake hivyo anajipanga kwa mashambulizi. Na ndio maana hataki kula sasa ili kulipa tumbo lake nafasi ya kutosha kwaajili yako pindi atakapokugeuza kitoweo chake “.
FUNDISHO– Watu wako wa karibu zaidi unaowaamini, wapole na wanaoonyesha kukupenda wanaweza kuwa wabaya zaidi kwako. Upendo wa dhati na dhamira nzuri haitokani na namna watu wanavyo Kukumbatia na kukuchekea. Unafiki huambatana na Upendo wa kujilazimisha. Usiogope mashambulizi yanayopangwa na maadui zako juu yako Bali ogopa rafiki mnafiki anayekukumbatia na kukuchekea huku anakumwagia sumu kali. Adui wa MTU ni wa nyumbani mwake.
Mbarikiwe.
Source: Unknown